Kila mmoja wetu mwenye nia njema naTanzania anapaswa kusimama kidete kuhakikisha tunapata katiba bora kwa maslahi ya Watanzania wote. Tusiwaachie wabunge wa CDM, CUF na NCCR peke yao hapana. Tanzania ni yetu sote na wala si mali ya ccm, hakuna mwenye haki miliki na Tanzania awe ccm au chama kingine chochote. Katiba ya leo itaamua hatima ya miaka mingi ijayo ya kizazi hiki na watoto, wajukuu, vitukuu na hata vilembwe na vilembwekeze.
Chama cha Mapinduzi hakiwezi kutuamulia katiba ya Tanzania kwanza hawana nia ya dhati kwani nia yao ni kuimarisha utawala wao wa ki-ccm, tusikubali.
Kwa haya yanayotokea bungeni ni ushahidi tosha kwamba ccm hawana nia ya kuwa na katiba inayozingatia maslahi ya watanzania wote. Kila mmoja ana haki ya kusikilizwa na pale inapoonekana kuna kasoro zirekebishwe, kama wenzetu wa Zanzibar hawakushirikishwa washirikishwe tena vya kutosha kwani haraka ni ya nini? Na je tunakimbilia wapi na kwa maslahi ya nani zaidi yetu sisi wananchi? Zanzibar ni nchi mshirika wa Muungano anapaswa kuwa na haki sawa na Tanzania bara(Tanganyika)Hakuna aliye bora zaidi katika hili si Bara wala Zanzibar.
Rai yangu ni kuwataka kila mwenye nia njema na taifa hili azinduke, aamke, aamue hatima ya Tanzania na vizazi vijavyo.