Mbowe atolewa nje ya bunge

Mbowe atolewa nje ya bunge

Mbowe alidhani hupo kwenye kampen ambapo huwa anaropoka hadi mishipa ya shingo inamsimama kama kakabwa na vibaka.toa nje kilaza huyo kanuni za bunge lazima ziheshimiwe asilete udj wake

Chuki
 
kwetu wametuzimia TV mara tu lile fujo kuanza., sijuwi ni kutoka bungeni wamefanya kusudi ama mitambo.,
 
There are currently 3555 users browsing this thread. (257 members and 3298 guests)
 
Kwani tatizo la Mbowe limeanzia kwenye kupiga kura au kuomba mwongozo?
Tatizo la Mbowe hajui kanuni za bunge na mvivu wa kuzisoma anafikiri kuomba muongozo ni kama kubadilisha santuri?
 
Kila mmoja wetu mwenye nia njema naTanzania anapaswa kusimama kidete kuhakikisha tunapata katiba bora kwa maslahi ya Watanzania wote. Tusiwaachie wabunge wa CDM, CUF na NCCR peke yao hapana. Tanzania ni yetu sote na wala si mali ya ccm, hakuna mwenye haki miliki na Tanzania awe ccm au chama kingine chochote. Katiba ya leo itaamua hatima ya miaka mingi ijayo ya kizazi hiki na watoto, wajukuu, vitukuu na hata vilembwe na vilembwekeze.
Chama cha Mapinduzi hakiwezi kutuamulia katiba ya Tanzania kwanza hawana nia ya dhati kwani nia yao ni kuimarisha utawala wao wa ki-ccm, tusikubali.
Kwa haya yanayotokea bungeni ni ushahidi tosha kwamba ccm hawana nia ya kuwa na katiba inayozingatia maslahi ya watanzania wote. Kila mmoja ana haki ya kusikilizwa na pale inapoonekana kuna kasoro zirekebishwe, kama wenzetu wa Zanzibar hawakushirikishwa washirikishwe tena vya kutosha kwani haraka ni ya nini? Na je tunakimbilia wapi na kwa maslahi ya nani zaidi yetu sisi wananchi? Zanzibar ni nchi mshirika wa Muungano anapaswa kuwa na haki sawa na Tanzania bara(Tanganyika)Hakuna aliye bora zaidi katika hili si Bara wala Zanzibar.
Rai yangu ni kuwataka kila mwenye nia njema na taifa hili azinduke, aamke, aamue hatima ya Tanzania na vizazi vijavyo.
Mawazo unayotoa utadhani umenunuliwa chadema wanataka kutumia katiba mpya nchi isitawalike kamwe hawataweza tuwapuuze hawana jipya ni mipango yao ya kitoto sana.
 
Kwa mtazamo wangu tatizo siyo Mh. Job Ndugai bali ni mfumo wa bunge letu linaloendeshwa na kanuni za kidikteta zilizopitwa na wakati zinazotoa madaraka yaliyopitiliza kwa kiti cha spika kiasi kwamba tumekuwa na IMPERIAL SPEAKER (kama ambavyo tayari tuna IMPERIAL PRESIDENT) ambaye anaweza kuamua jambo lolote bila kuhojiwa.

Huwa mara nyingi nashangazwa sana na maamuzi ya ajabu ajabu yanayofanywa na hawa viongozi wanaopewa kuongoza mijadala (Spika na Wenyeviti) mbalimbali vya bunge kiasi cha kulifanya Bunge ligeuka kuwa kama Primary School enzi zetu ambapo mwalimu wa zamu alipokuwa akiongea mwanafunzi hakutakiwa kuhoji vinginevyo anatembelea kichapo. Siku hizi ukisikia tu wenyeviti wa mijadala wanaongelea hiki wanachokiita BUSARA YA KITI ujue kuna uamuzi wa kipuuzi unafuata. Thank God am not a politician.
 
Du!!! ubabe huu wa wabunge unaliabisha sn Taifa,kwa nn wasifuate taratib za bunge?
 
Sitta - Kauli yako imetimia rasmi, ulisema watu watalikumbuka bunge lako la kwa VIWANGO vya kimataifa; kwa kweli wengi tumeanza kukukumbuka kwa hekma zako hasa mimi.

Bunge linapofikia pahala linaongozwa kama kijiwe ni hatari kwa ustawi na usalama wa nchi.
 
mmh bunge letu linakaribia kuwa kama lile la urusi.ni misuguano kwa kwenda mbele.tunachosubiri sasa ni kuona wakichapana makonde!

Nadhani wakichapana makonde siku moja heshima itakuwepo. Watu watakuwa wakifikiria mara mbili kabla ya kutoa kauli za kejeli au amri za kidikteta.
 
Kunatofauti gani kati ya mbowe na watoto wa sekondari walioko shuleni make anafanya vituko na kutia aibu bungeni.

Wewe nawe boonge la mbulula. Watoto wa Sekondari ndio unawaona SI unit ya fujo wakati wana akili kukuzidi wewe mpuuzi unayeshinda humu kutetea wapumbavu wenzio CCM. Wewe endelea kutetea tonge lako kwa post za buku 7 watoto wa sekondari wanajiotambua acha kabisa kuwadharau wana akili kuliko wewe.

 
Afu mtu akisema jamaa wanafujo anatukanwa, Kanuni za bunge ziliwekwa kwa utaratibu mzuri kabisa, sijui ingekua ni Mbowe amekatishwa huku akiongea angejisikia vipi? Ila yeye kwenye kukatisha huku mwenzake anaongea huko ni kujaribu kuonyesha kua yeye ndio ana nguvu zaidi bungeni au? Hapa jamaa simuungi mkono kabisa, Lile ni bunge, kama mbunge tena kiongozi mkubwa haeshimu bunge, nani ataliheshimu sasa? Hiyo tayari ni proof ya kuonyesha kushindwa kabisa kufanya kazi vzr, emotion nyingi hadi mtu unafanya hivo, ukipewa urais si nchi ikikutibua kidogo tu utapigana vita...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom