Mbowe atolewa nje ya bunge

Mbowe atolewa nje ya bunge

samaki ana mengi ya kuongea Lakini ndo ivo ana maji mdomoni! Lakini ipo siku maji yatatoweka ili samaki awezepaza sauti yake! MBOWE keep up!
 
Hivi bungeni kama kila mbunge akijiona hana haki na kuamua kusimama kuongea na akiambiwa aache na Spika agome............kweli kutakuwa na Bunge?

Siku tegemea mtu kama Mbowe anaweza kufanya aliyofanya

Kuna haja ya CDM kuangalia upya strategies zao za kisiasa................hizi siasa zenye elements za ubabe na vurugu itafikia mahali wataonekana kama kundi la vurugu
 
Hapa ndipo tunapokosa uzalendo wa kweli kwa Taifa la Tanzania, Katiba bora ni kwa manufaa yetu wote na vizazi vijavyo

CCM wanafanya mambo kama watoto, wanafanya mambo bilakujuwa kunakesho na keshokutwa, siku hazigandi na Tanzania si mali ya ccm.

Katiba kwa maana moja au nyingine ndiyo kiungo na tiba ya majeraha mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

CCM ni kama wamerogwa na ukitathimini kwa undani zaidi utagunduwa kashifa za ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka,

Madawa ya kulevya na utesaji ni jinamizi linalowaogopesha sana katika kuunda katiba.
Matokeo yake wanaharibu

matumain yawatanzania kwamba katiba itatoa majibu ya utata na kuweka misingi mizuri ya utawalabora.
 
Alafu hii ndiyo iwe Bunge ambalo Warioba na Tume yake wanataka sisi Watanganyika na Wazanzibar tuwaamini na kuwapa Mamlaka ya Kutunga sheria na Kanuni ya kuwajibisha pale watakapo enenda kinyume na Matakwa ya Katiba;
Yaani Paka amfunge kengele Panya!

Karibuni.Haya ni ya Warioba na Tume yake;

124.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya123 ya Katiba hii,wananchi watakuwa na haki ya kumuondoa Mbunge wao madarakani,endapo Mbunge atafanya mojawapo au zaidi ya mambo yafuatayo:

(a) kuunga mkono sera ambazo zinaenda kinyume na maslahi ya wapiga kura au kinyume na maslahi ya Taifa;
(b) kushindwa kuwasilisha au kutetea kwa dhati hoja zinazotokana na
kero za wapiga kura wake;
(c) kuacha kuishi au kuhamisha makaazi yake kutoka eneo la Jimbo la Uchaguzi kwa zaidi ya miezi sita bila sababu za msingi;
(d) kutohudhuria vikao vya Bunge vitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika;
(e) kuajiriwa au kufanya kazi nyingine na kuacha kuzingatia kazi yake ya kuonana na wapiga kura wake;
(f) kufanya biashara, kumiliki makampuni au kuwa na hisa katika makampuni ambayo yana mikataba au mahusiano ya kibiashara na taasisi za umma kwa namna ambayo inaleta mgongano wa kimaslahi;
(g) kutiwa hatiani kwa kosa linalohusiana na rushwa au kosa jingine la jinai;
(h) kutenda kitendo ambacho ni kinyume na maadili au kukosa uaminifu; au

(i) mambo mengine yatakayoainishwa kwenye sheria ya Bunge.
(2) Bunge litatunga sheria kuweka masharti ya namna ya kuendesha uchunguzi kwa Mbunge atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa wapiga kura wake na utaratibu wa kumuondoa mbunge.


Mimi na maoni tofauti;

124.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya123 ya Katiba hii,wananchi watakuwa na haki ya kumuondoa Mbunge wao madarakani, endapo Mbunge atafanya mojawapo au zaidi ya mambo yafuatayo:
(a) kuunga mkono sera ambazo zinaenda kinyume na maslahi ya wapiga kura au kinyume na maslahi ya Taifa;
(b) kushindwa kuwasilisha au kutetea kwa dhati hoja zinazotokana na kero za wapiga kura wake;
(c) kuacha kuishi au kuhamisha makaazi yake kutoka eneo la Jimbo la Uchaguzi kwa zaidi ya miezi sita bila sababu za msingi;

(d) kutohudhuria vikao vya Bunge vitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika;
(e) kuajiriwa au kufanya kazi nyingine na kuacha kuzingatia kazi yake ya kuonana na wapiga kura wake;
(f) kufanya biashara, kumiliki makampuni au kuwa na hisa katika makampuni ambayo yana mikataba au mahusiano ya kibiashara na taasisi za umma kwa namna ambayo inaleta mgongano wa kimaslahi;
(g) kutiwa hatiani kwa kosa linalohusiana na rushwa au kosa jingine la jinai;
(h) kutenda kitendo ambacho ni kinyume na maadili au kukosa uaminifu; au

(i) mambo mengine yatakayoainishwa kwenye sheria ya Bunge.

(2)Kwa ajili ya usimamizi nzuri wa Demokrasia Tume ya Haki za Binadamu kwa kushirikiana na wapiga kura itaandaa Kanuni na Masharti yatakayosimamia shauri dhidi ya Mbunge kwa;


(a)watu wanaoweza kufungua shauri na;
(b) sababu na nyakati za kufungua shauri na;

(c )utaratibu wa kufungua shauri na;
(d)masharti yanayotakiwa yatimizwe kwa kila shauri kama hilo na ;
(e)namna na nani wa kuendesha uchunguzi dhidi ya Mbunge atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa wapiga kura wake na ;
(f)utaratibu wa kumuondoa mbunge.

(3) Baada ya kukamilisha Kanuni na Masharti kwa mujibu wa ibara 124(2) ya Katiba hii Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Bunadamu atawasilisha nakala kwa Spika wa Bunge na Spika baada ya kupokea Kanuni na Masharti yaliyotajwa katika ibara ya 124 (2) ya Katiba hii ataitisha Kikao cha Bunge nzima,na atawapatia Wabunge wote nakala ya Kanuni na Masharti tajwa kabla ya Kikao na Bunge litapigia kura ya ndiyo au hapana kifungu kwa kifungu ya Masharti na Kanuni husika na zaidi ya asilimia hamsini ya kura za ndiyo za Wabunge za ndio utakuwa uamuzi wa mwisho wa mswada huo na baada ya hapo utapelekwa kwa Raisi kupata saini yake kuwa sheria.

(4) Kwa vyovyote vile Masharti na Kanuni iliyorejewa ibara ya 124(3) kama yamepita kwa kura za ndiyo chini ya ibara hiyo na kwa namna yoyote ile haijapata saini ya Raisi na siku kumi na Nne zimepita basi itahesabika kuwa Sheria.
(5)Mbunge yeyote atakayeondolewa kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii anaweza kukata rufaa Mahakama ya Juu na uamuzi wa Mahakama utakuwa wa mwisho.
 
time will tell;upumbavu wa ndugai na shosti makinda utaisha.
 
Leo bunge lilikuwa katika wakati mgumu kidogo,wakati wabunge wakikinzana juu ya mswada ya serikali kuhusu muundo wa bunge maalum la katiba na nani haswa apewe nafasi ya kuwateua wajumbe ambao wataungana na wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania..kwa kutumia kanuni za bunge Mh ndugai aliwahoji wabunge kunaokubali mswada utolewa au uendelee,kwa njinsi sauti zilivyotoka ilikuwa ngumu kidogo kujua wapi wengi wamekubali au kukataa mswada huo,ndipo mbunge wa ubungo mh John Mnyika alipoomba kura zipigwe,kura zimepigwa na wabunge waliowengi wakakubali mswada huo uendelee kujadiliwa. Ndipo Ndugai aliruhusu mjadala uendelee kwa kumruhusu mchangiaji wa kwanza mh Lyatonga mlema..KIONGOZI wa kambi wa upinzani mh Freeman Mbowe alisimama kuonesha ana hoja mbele ya bunge, mh Ndugui kwa kebei na kutojali wadhifa wa Kiongozi wa kambi ya upinzani alitoa amri kwa mh Mbowe kuketi ili mswada uendelee kuchangiwa, Mh mbowe aligoma kuketi kwani sheria na kanuni za bunge zinamlinda kama kiongozi wa kambi ya upinzani pia mbunge halali wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania. Kwa kustahajabu mh ndugai alitoa kauli ambayo ni tata kwa kuwaandaa askari kwa dk 5 waje wamtoe Kiongozi wa kambi ya upinzani! Baada ya kauli hiyo aliruhusu maaskari kuingia na kuanza kuvutana na kambi rasmi ya upinzani waliojitokeza mbele kupinga dhuruma,unyanyasaji na ukandamizaji wa haki na democrasia uliofanywa na kada huyu wa CCM na naibu spika wa bunge. Swali Je kama angetoa nafasi kwa mbowe kutoa hoja yake kungekuwa na ubaya gani? Je mbowe amevunja sheria gani kwa kuomba muongozo wa spika? Je kwa nini ndugai hajampinga Mbowe kwa kanuni za Bunge lakini akabaki kutapatapa na maaskari ambao hawakuwa sehemu ya majadiliano hayo? Je kwanini ajaribu kuzima hoja za upinzani wakati Mh lukuvi alipewa nafasi kama hiyo kuongea na kutoa yake ya moyoni? Je kwanini Ndugai anakosa hekima na shime kwa viongozi wa upinzani? Je angekuwa Anne Makinda angetoa uwamuzi kama wa Ndugai ? IMENISIKITISHA SANA NA KUNIFANYA NIKUMBUKE KAULI NYINGI ZA VIONGOZI WAKOMBOZI WA BARA LETU KWAMBA: ukiona mtawala anakubana hata kukusikiza basi tambua tayari anawoga na hoja zako,hivyo ukombozi unakaribia,
 
Zitto nae kama kawaida akakurupuka na maoni haya kwenye facebook:
Usituhukumu.Elewa "@YusuphKamote: @zittokabwe sioni msingi wa ujinga uliongozwa na Mh Mbowe wa kugombea kuaribu Msingi ya demokrasia"
 
Hivi bungeni kama kila mbunge akijiona hana haki na kuamua kusimama kuongea na akiambiwa aache na Spika agome............kweli kutakuwa na Bunge?

Siku tegemea mtu kama Mbowe anaweza kufanya aliyofanya

Kuna haja ya CDM kuangalia upya strategies zao za kisiasa................hizi siasa zenye elements za ubabe na vurugu itafikia mahali wataonekana kama kundi la vurugu

Mkuu Mbowe katia aibu sana.

Aelewi maana ya kupiga kura. Sasa sijui kwanini walikubali kushirikia upigaji kura kama hawako tayari kupotea matokeo yake.

Wabunge wa Chadema ni kama Mbuzi wa Vingunguti...

Ndio maana kuna mdau alileta thread hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/436964-mbuzi-wa-vingunguti-bungeni.html
 
Camera man wa TBC 1 mjinga kweli badala ya kutuonyesha kinachotokea yeye antuonyesha job ndugai

Mkuu yaani angethubutu kumulika kamera zake tu kwenye hicho kisanga, basi siku inayofuata kibarua chake kingeota nyasi
 
Ndugai jana alisema kuwa upinzani utamtambua na leo ameanza kutumia mabavu,silly ndugai
 
Job Ndugai kwa leo ametenda haki sana tu. Wengi humu mnasimuliwa na kudanganywa sana.
 
Ndugai anaifanya kazi ya uspika ionekane nyepesi sana ambayo hata kilaza anaweza kuifanya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom