124.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya123 ya Katiba hii,wananchi watakuwa na haki ya kumuondoa Mbunge wao madarakani,endapo Mbunge atafanya mojawapo au zaidi ya mambo yafuatayo:
(a) kuunga mkono sera ambazo zinaenda kinyume na maslahi ya wapiga kura au kinyume na maslahi ya Taifa;
(b) kushindwa kuwasilisha au kutetea kwa dhati hoja zinazotokana na
kero za wapiga kura wake;
(c) kuacha kuishi au kuhamisha makaazi yake kutoka eneo la Jimbo la Uchaguzi kwa zaidi ya miezi sita bila sababu za msingi;
(d) kutohudhuria vikao vya Bunge vitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika;
(e) kuajiriwa au kufanya kazi nyingine na kuacha kuzingatia kazi yake ya kuonana na wapiga kura wake;
(f) kufanya biashara, kumiliki makampuni au kuwa na hisa katika makampuni ambayo yana mikataba au mahusiano ya kibiashara na taasisi za umma kwa namna ambayo inaleta mgongano wa kimaslahi;
(g) kutiwa hatiani kwa kosa linalohusiana na rushwa au kosa jingine la jinai;
(h) kutenda kitendo ambacho ni kinyume na maadili au kukosa uaminifu; au
(i) mambo mengine yatakayoainishwa kwenye sheria ya Bunge.
(2) Bunge litatunga sheria kuweka masharti ya namna ya kuendesha uchunguzi kwa Mbunge atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa wapiga kura wake na utaratibu wa kumuondoa mbunge.