Mbowe ashikiliwa Central Police

Mbowe ashikiliwa Central Police

Haya maneno tu hayatasaidia chochote nimuda muafaka wakumobilize watu wakutane wapi kesho asubuhi kupinga hii dhuluma nakupanga wafanye nini coz kama ni dharau hii imezidi mipaka Viongozi waliopo Dar wafanye hii kazi natuitumie hii forum pamoja na facebook tukitumi wall ya Mnyika na Dr.Slaa kupeana Taarifa tutakapo kutania.
 
Hatukuogopa juzi, hatukuogopa jana, hatutaogopa jeshi la polisi leo na kesho, nimesema tunawakoloni weusi nchi hii (polisi) tukitaka uhuru wa kweli lazima tufight, hawa polisi ni maskini wakubwa wa kutupwa ktk nchi hii lakini ndio wakwanza kushika wakombozi wa taifa hili. hii inanisikitisha sana ila ipo siku moja tu, tena siku ya siku kuu huu upuuzi na ubabe wa watawala wetu utapotelea mbali kabisa common..
 
Hili nibaraza la vijanaa au Baraza la Vijana au Baraza la Vichaa(BAVICHA) Mbona wanapenda kukurupuka!Muda mfupi vijana na wadau wa CDM Wame2ma sms za k

Ni heri kufa umesimama kwa miguu yako kuliko kuishi miaka mingi ukiwa umepiga magoti. mbuzi we!
 
Hili taifa linateketea kwa mikono ya wakoloni weusi na watawala wasio na maono. Dr Slaa kiongozi wa watanzania tunaomba Muongozo wako kamanda. Watanzania tumechoka kulaghaiwa,Tulisikia ari mpya iko wapi??? tulisika kasi mpya iko wapi?? tulisikia maisha bora yako wapi??kamanda tuongoze baba tukutane wapi saa ngapi ili kielewekee.Tumechoka na ubabe wa watawala wenye mawazo ya kindumilakuwili
 
jtatu mahakamani na chupa za maji kupoza mabomu ya machozi na ramba kwa ajili ya mbio
 
Hebu nielezeni TBC1 kwa nini hawajatoa tarifa ya kukamatwa kwa Mbowe wanaogopa nini,ITV wametangaza
 
JAMANI HUKU ARUSHA TUNA HITAJI MWONGOZO KUTOKA chadema MAKAO MAKUU DAR.

Je tupite barabara zipi mpaka mahakama kuu?
 
Tukumbushane Ahadi za Jk
1.Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
2.Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
3.Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
4.Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
5.[NENO BAYA]liza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
6.Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
7.Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
8.Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
9.Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
10.Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
11.Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12.Mtukula kupa[NENO BAYA] umeme kutoka Uganda - Kagera
13.Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
14.Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
15.Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
16.Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
17.Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18.Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
19.Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
20.Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
21.Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
22.Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
23.Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
24.Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
25.[NENO BAYA]liza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26.Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
27.Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
28.Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
29.Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
30.[NENO BAYA]liza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
31.Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
32.Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
33.Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
34.Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
35.Kulinda amani nchini kwa kuzuia [NENO BAYA][NENO BAYA] za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
36.Kulinda haki za walemavu - Makete
37.Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
38.Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
39.Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40.Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
41.Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
42.Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
43.Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45.Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
46.Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
47.Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
48.Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
49.Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
50.Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
51.Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
52.Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
53.Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
54.Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
55.Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
56.Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
57.Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
58.Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
59.Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
60.Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
61.Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
62.Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
63.kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
64.Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
65.Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
66.Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
67.Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
68.Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
69.Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha

Quote
 
this is a tipical sign that ccm is no longer; all the best ccm for ur preparation of new life out of leading party
 
SERIKALI NI NINI? SERIKALI YA ARUSHA NI YA CHAMA CHA MAGAMBA?........! Bunge ni serikali? mahakama ni serikali? nini maana ya eneo kuwa na serikali ya chama cha ......CHADEMA/CUF/CCM/CHAUSTA/TLP?
KUFUATA SHERIA NI KUPI.....? JE SHERIA IFUATWE KWA WOTE AU BAADHI?
WANA-JF? GREAT THINKERS.....OR GREAT TINKERS?

Nice questions!..
 
.............Mara zote mapinduzi ya kweli yalichochewa na watawala kutumia nguvu ya dola bila kuzingatia kuwa nguvu ya dola ni dhaifu sana kwa nguvu ya umma,watatumia njia nyingi sana za kuwavunja nguvu wanamapinduzi wa kweli....but time will tell

CHADEMA FOR CHANGE...FREEDOM IS COMING NOT TOMORROW BUT SOON...
 
Nadhani Tundu Lissu alishatoa mwongozo...tuanzie hapo sasa!!
 
Hivi sisi hapa jf tuna msaada gani hadi sasa hivi kuhusu kukamatwa kwa mbowe?
 
mbowe kuwa kafara kuwezesha ubabe/umungu mtu wa mahakama ukome wananchi wanaziogopa mahakama wakati ni eneo la wao kudai haki kisa usumbufu unaenda mahakamani unakaa siku nzima ukijua kesi ni ya kutajwa na kuahirishwa , hakimu anakupa ruhusa usije mahakamani hlf anataka mdhamini wk afike siku ya kesi kumkumbusha na ukiritimba mwingine mwingi usio na tija kwa taifa
 
Walipomuua Yesu,walidhani wamemkomesha,na kumbe wameuwasha moto,utakaoteketeza.ndicho walichofanya Ccm,watajuta na TUSILAUMIANE ,

Mkuu kwa hiyo unamfananisha Mbowe na Yesu? Du!! Kweli ni ngumu sana kutofautisha Kanisa na Chadema, hivi kwa nini wanachadema wengi wanapenda sana kumtumia yesu katika mambo ya Chadema. Juzi tulimsikia Dada Mtema, leo tena wewe
 
Acha anyee debe, kwani anajifanya mjeuri sana utadhani hii nchi ni yake. Slaa anagwaya mahakama kwani makosa wanayo na wamesha ona sheria inawabana, sasa Slaa amebaki kivuri chake ni Mimba ya Hawala wake. Tunaomba sheria ifanye kazi, kwani nchi inaongozwa kwa utawala wa sheria.

Hapo kwenye red: Magamba wathubutu kumuweka ndani kama 2015 haitakiwa instant coffee!
 
ohhh wamefanya makusudi wakijua leo ni Jumamosi.wanataka kumkomesha Mbowe!!! Kama kawaida itakula kwao. Mbowe atatoka huko bigger than ever. nadhani ccm bila kujijua wamekuwa wanajenga CHADEMA! goood work ccm, I say good work!


Kwa maoni yangu, linapokuja suala la kutii na kuheshimu sheria ushabiki wa kisiasa tuweke pembeni maana utiii wa sheria ndio msingi wa utawala wa sheria, demokrasia na amani. Mheshimiwa Mbowe kama alivyo Mh Doctor Slaa walifikishwa katika chombo cha sheria kwa tuhuma na kwa kuzingatia taratibui za kisheria. Wakapewa dhamana bila usumbufu wowote. Wakavunja masharti ya dhamana kwa kutohudhuria mahakamanai. Mh DR Slaa na Mh. Lema kwa kujuwa matokeo ya kukiuka masharti ya dhamana wakajisalimisha wenyewe mahakamani na kutoa sababu ya kutohudhuria. MH. MBOWE yeye akaamua kukiuka masharti ya dhamana kwa mara nyingine. Kama kwamba haitoshi akaanza kulumbana na mahakama kwa kutumia majukwaa ya kisiasa na vyombo vya habari. Kali hali kama hiyo jeshi la polisi lisingemkamata tungelielewa vipi? Hiyo si ingekuwa kudhalilisha mfumo mzima wa sheria na uhuru wa mahakama?

Kama MH. MBOWE angekuwa na utetezi kwamba yuko bungeni au ana kinga, angepaswa kujisalimisha mahakamani na kutoa utetezi huo badala ya kulumbana na mahakama katika vyombo vya habari. Pia angeweza kushauriana na wanasheria wake kuona uwezekano wa kupinga amri hiyo katika mahakama kuu kama aliona hakimu mhusika alishawishiwa na serikali.

Picha tunayoipata wananchi ni mbaya sana. Kama waheshimiwa wabunge ambao wenyewe wanaheshimika kwaajili ya kazi yao ya utunzi wa sheria wanakuwa wa kwanza kuzarau sheriia sisi walala hoi itakuwaje?
 
Back
Top Bottom