Ben,
Tusiende kama vipofu wa sheria, jana niliweka maoni yangu humu na nikahoji kilevilevi kuhusu umakini wa Mhe. Lissu (post # 75) katika jambo hili. Niliona upotoshaji mkubwa katika namna ya kushughulikia shauri hili, bahati mbaya leo yametokea mabaya. Nauliza tena, was it an oversight on the part of Hon. Lissu?
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-la-kesi-ya-arusha;-mbowe-naye-alonga-4.html
Nachelea kusema kwamba kuna upotoshaji unafanyika na sijui ni kwa hasara ya nani.
Mhe. Mbowe ana Makosa ya wazi kabisa ya kudharau Mahakama, si jambo zuri kwa kiongozi Mkuu wa aina yake.
Mhe. Lissu ni Mwanasheria makini, hivi ana amini hilo tamko linatosha kuzuia utekelezaji wa Amri ya Mahakama?
Tusipumbazane hapa, kama sijasahau Sheria, Tamko hilo lingekuwa na Makali kama lingefuatana na Amri ya Mahakama ya juu kusitisha/kuzuia kwa muda utekelezaji wa Amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha.
I stand to be corrected!
Last edited by sikubaliki; Today at 07:21 PM.