Mbowe akiwa na vijana wake wa CHAUMMA

Mbowe akiwa na vijana wake wa CHAUMMA

Hawa wanamheshimu sana Mbowe hata kama yuko Chadema. Na mwenyewe anawaheshimu sana maana walimpigania sana wakati akiwa jela na wakati wa uchaguzi. Wanaipenda bado Chadema ndio maana huwasikii wakiwatukana viongozi wake pamoja na figisu kibao walizofanyiwa na wanazoendelea kufanyiwa. Ni wapinzani damu damu.

Amandla...
Wangeipenda Chadema wasingehama.

Wanampenda Mbowe kuliko Chadema.
 
Wangeipenda Chadema wasingehama.

Wanampenda Mbowe kuliko Chadema.
Ulitaka wavumilie kutengwa na wenzao na matusi waliyokuwa wakiporomeshewa? Kwa sababu tu walidiriki kutofautiana na msimamo wa Mwenyekiti wao? Sigrada alipigwa na msaidizi wa kiongozi wao na hamna mtu wa Chadema aliyediriki kumuomba msamaha. Wangebaki Chadema wangekuwa wenda wazimu.

Amandla...
 
WanaCHADEMA haitawasaidia kitu kumtukana Mbowe. Siasa za nchi hii hazitabiriki. Mwaka 2001 kina Lipumba na CUF yake walikuwa wa moto mno wakipambana na IGP katili Mahita kiasi kwamba Lipumba alikuwa anakutana na vipigo vitakatifu ila Lipumba huyohuyo akautangazia umma kuwa aliwasihi waislamu wenzake wamchague JK mwaka 2010 huku yeye pia mgombea urais.

Miaka 5 baadae yaani 2015 katibu mkuu bora wa muda wote CHADEMA Padri aliyeasi, Dr Slaa aliamua kujiweka kando na CHADEMA ambapo baadae alipata ulaji kwenye serikali ya JPM.

Nimetoa mifano miwili kuonyesha kuwa unaweza kumtukana Mbowe kumbe msaliti wenu anaweza kuwa Heche au Lissu. Cha muhimu mheshimiane.
Kinacho nishangaza vijana WA ccm ndo wamekuwa wsemaji WA mbowe na chauma. HIVI kile kitengo cha propaganda cha Chama chetu kilifia wapi.
 
Mwenyekiti wazamani wa CHADEMA Freeman Mbowe akiwa na vijana na makada wa zamani wa CHADEMA ambapo walihamia kwenye chama Cha CHAUMMA .

Vijana wanajichekesha tu wenyewee
Hawa ndio wamepotea kabisa kwenye siasa, sijui nani aliwarubuni kuwa wakienda chaumma watapewa ubunge!! Yaani hawana tofauti na waliosusia uchaguzi zaidi wameingia hasara ya fedha za kampeni na heshima imekufa.
 
Kwa nini uwe na haraka namna hiyo kuhitimisha mkuu 'zitto junior'?

Huoni bado wanatabasamu; unaijuwa mipango yao?
Hapo wapo kwenye kikao; hatujui waliongea kitu gani.

Mfadhili wao mkuu anatawala, na hajatimiza hata siku mia mbili; bado anapanga safu maeneo mbalimbali..

Kwa kundi hili "heshima" unayoizungumzia wewe inaishia kwenye kupewa ulaji mahali fulani, basi.
 
Nimetoa mifano miwili kuonyesha kuwa unaweza kumtukana Mbowe kumbe msaliti wenu anaweza kuwa Heche au Lissu. Cha muhimu mheshimiane.
Kama bado unayo matumaini juu ya hawa kuwa kama unavyodai wewe; akili yako itakuwa inafanya kazi kinyumenyume sana.

Katika hao akina Lipumba na wengine wa namna hiyo; hakuna hata mmoja aliyepitia katika tanuru la moto mkali kama unaowapika hawa akina Heche.
Sasa kama hata hilo halikupi akili ya kuona tofauti; wewe unazo sababu zako nyingine za kujifanya tiu, kuwa hujui, au unatumia sifa yetu jadi "uswahili" mwingi.
 
Katika ujinga unaowatafuna wapinzani wengi kama wewe ni kuweka matumaini yao yote kwa wanasiasa.. miaka michache iliyopita ni nyie mlikuwa mnasema "MWAMBA TUVUSHE".. Leo hii mnamtukana.
 
Katika ujinga unaowatafuna wapinzani wengi kama wewe ni kuweka matumaini yao yote kwa wanasiasa.. miaka michache iliyopita ni nyie mlikuwa mnasema "MWAMBA TUVUSHE".. Leo hii mnamtukana.
Hakuna anayetukanwa. Muda unatupa mafundisho na unaendelea kutuambia mbivu na mbichi ni zipi. Tofauti tunaziona.
 
Tatizo hamjawai kumuelewa huyu mwamba,ni kama Oukinyonga anabadilika kuendana na mazingira tu.
Kijani,kijani,njano njano,blue Blue,nyeusi yumo,nyekundu yumo.
Hapo mwenzenu atabeba mikoba ya Chama cha mkwewe huku mwenyekiti analumbana na maaskari magereza huko.
Mtu kamaliza darasa la 4-5, unamsomea vifungu vya sheria vya Oxford huku we mwenyewe huvijui atakuelewa?
Tundu atoke arudi kwa wanae na mkewe km ataweza.
 
Hapo anawaambia kuwa alishindwa kujoin huko
Kama wanasubiri pombe na nyama za bure , wanavyojichekesha.
CHAUMMA kwa vile alimuogopa Baba Mkwe wake Mzee Mtei sasa kwa vile mzee ameshatangulia mbele ya haki basi soon atawajoin ili kuimaliza kabisa Chadema na CHAUMMA itakuwa chama kikuu kama walivyopanga tangu awali.
 
Kweli wanaodai MADARAKA YANALEVYA tumewaelewa sana...
 
Ulitaka wavumilie kutengwa na wenzao na matusi waliyokuwa wakiporomeshewa? Kwa sababu tu walidiriki kutofautiana na msimamo wa Mwenyekiti wao? Sigrada alipigwa na msaidizi wa kiongozi wao na hamna mtu wa Chadema aliyediriki kumuomba msamaha. Wangebaki Chadema wangekuwa wenda wazimu.

Amandla...

Msiwe mnaokoteza maneno. Sigrada hakupigwa, alisukumwa na mlinzi wakati analazimisha kuingia ndani wakati alipokuwa ametolewa kwenye kikao kufuatia vurugu alizokuwa ameleta. Ufahamu kuwa wakati Sigrada aliposukumwa na kuanguka chini, kulikuwepo na polisi wanne hapo hapo. Kwa hasira akaondoka akaenda baa, akapiga kinywaji mpaka saa 8 usiku. Alivyoanza kutapika, akazusha kuwa amepigwa ndiyo maana anatapika.

Kwa akili yako tu ya kawaida, mtu apigwe mbele ya polisi wa CCM, wamwangalie tu, na wanavyotafuta upenyo wa kuwaonea CHADEMA, si wangeona wamepata sababu ya kuwatesa CHADEMA? Umewahi kumsikia yeyote ana kesi ya kumpiga sigrada?
 
Project ishafeli hiyo - naona wanaanza kujileta leta CDM tena. Kuna muda Mwanadamu huwa ni mtu wa hovyo kabisa.
 
Mwanasiasa atafanya lolote apate madaraka ili ale peke yake. Wabinafsi na wanafki sana hawa watu
 
Back
Top Bottom