Uchaguzi 2020 Mbowe adhalilisha vyama vyote vya upinzani nchini, adai havistahili kupewa haki ya kunadi wagombea wao

Vyama uchwara vinavyotembea na masufuria , sijui masahani ya ubwabwa vina heshima gani kama vyenyewe vimeshindwa kusimama kwa miguu yao .
 
Mbowe kasema ukweli mchungu, ukweli vyama vinavyoonekana ni vinne tu yaani, cuf, ccm. act, chadema.vingine ni vyama hewa.
 
Leo Mbowe umeharibu kila kitu. Labda amelewa! Pamoja na Zitto kumuunga mkono Lissu anasema hivi vyama ni mkakati wa CCM kweli?
 
kwa kweli Mbowe amevidhalalisha mno na kuvidharau vyama vingine vya upinzani. siamini kama kweli chama cha upinzani ni CHADEMA tu!!
kauli ya Mbowe ina didimiza demokrasia ya vyama vingi vya upinzani, lakini pia inavikosea heshima vyama vingine
 
Leo mbowe umeharibu kila kitu. Labda amelewa! Pamoja na zito kumuunga mkono lissu anasema hivi vyama ni mkakati wa ccm kweli?
Ukweli unabaki palepale, vyama Vingi ni mkakati wa CCM kama NRA, ADC....ujinga mtupu, wako wapi wagombea wao?
 
Leo kwa mara nyingine CHADEMA imeidhihirishia umma kuwa ni chama cha kidikteta na isiyoheshimu misingi ya demkrasia, uhuru na haki ya kisiasa ya kila chama na kila mtanzania.​

Dunia yote imeshangaa tamko la Mbowe leo akisisitiza huku akitokwa na povu kwamba CHADEMA na CCM tu ndivyo vyama pekee vinavyostahili kupewa fursa ya kujinadi Tanzania bara kwa madai kuwa upinzani upo baina ya vyama hivyo viwili, Amedai vyama kama ACT, CUF, NCCR, TADEA na vingine havistahili hata kupewa fursa ya wagombea wao wa urais kujinadi kwenye ratiba ya TUME na kwamba vyama hivyo ni uzibe kwa CHADEMA.​

Kwa chama kinachojinasibu kuwa ni cha demokrasia na kinachodai kina sera ya uhuru na haki kutoa tamko kama hili limeshtua dunia. Hii ni dhahiri CHADEMA ni chama cha kidikteta na kama ndicho leo kingekuwa madarakani Mbowe angevifuta vyama vyote hivyo na kubakiza CHADEMA pekee yake. Duniani kote katika mfumo wa demkrasia vyama vitogovidogo vipinna vinapewa haki sawa ya kunadi sera zao.​

Hata Marekani, Uingereza, Ujerumani n.k kuna vyama vidogo vidogo. Chama kidogo leo kinaweza kuwa chama kikubwa miaka 10 ijayo. Kwa nini vinyimwe fursa? Nafikiria uchaguzi wa 1995 chama kilichokuwa na nguvu na upinzania mkubwa kwa CCM kilikuwa NCCR-Mageuzi, hivi Chadema kingefutwa leo kingekuwa wapi.​

Kwa nini leo Chadema inaona NCCR -Mageuzi haistahili kupewa haki ya kunadi sera zao na mgombea wao wa Urais?, Hivyo hivyo kwa TADEA na vyama vingine.​

Watanzania na dunia inazidi kufahamu sura halisi ya CHADEMA. Watanzania wenzangu na wapenda haki na demokrasia, pingeni chadema kwa nguvu zote na tuiadhibu kwenye kura ya Oktoba 28.​

Hatutaki chama cha kidikteta na chenye ubinafsi kama CHADEMA na mgombea wake Lissu anayetoa lugha za dharau kwa wagombea wa vyama vingine hata ndani ya upinzani. Tupilia mbali Chadema, Tupilia mbali Lissu. Tunakwenda na Rais Magufuli.​

Tunakwenda na maendeleo na demokrasia.​

Kazi ya mawakala wa shetani ni kufitinisha na kuchonganisha....ushindwe na ulegee we kibwengu wa lumumba
 
Sikiliza alichosema Mbowe kwenye hiyo clip kuanzia dakika 3: 33. Tena ameviita vyama vingine kuwa ni wabakaji wa demokrasia!!! Nategemea vyama vote vya upinzani vitatoa tamko na kulaani udhalilishaji huu na kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kuishitaki Chadema kwa udhalilishaji. CHADEMA inazidi kujimaliza kwa kauli zake
 
Back
Top Bottom