Hivi karibuni tumesikia taarifa kutoka kwa mzee wa anga, bwana Mbowe, akiisifia rasimu ya katiba kuwa 'ipo poa' kwani imebeba mapendekezo mengi ya CHADEMA kama lile la serikali tatu.
Kauli hiyo ya mzee wa anga imezua kizungumkuti kwa watanzania wengi, kwani haijulikani kama kauli hiyo ni msimamo wa chama ama vipi.
Katika chimba chimba zangu, leo nimegundua kuwa, Dr Slaa kama katibu mkuu wa CHADEMA amewataka watanzania wawe na subira ili uongozi wa CHADEMA uweze kupitia kila kipengele katika rasimu hiyo ndipo itoe maoni.
Maelezo ya Dr Slaa kwa watanzania wenye kiu ya kusikia maoni ya CHADEMA kuhusu rasimu ya katiba ni haya hapa;
"Habari watanzania,
Nafahamu watanzania wengi wana hamu ya kusikia tamko la CHADEMA juu ya rasimu ya katiba mpya kwani CHADEMA ndio serikali yetu ya nguvu ya umma ambayo inasimamia uzalendo kwanza.
Uongozi wa CHADEMA utatoa maoni yake juu ya kupokea rasimu hii ili watanzania watambue na nguvu ya umma kupitia na kupitisha.
Ntapenda utulivu na kupitia kila vipengele vya rasimu ya katiba mpya kila mtanzania kufafanua vipengele mbalimbali. Mungu mkubwa kwa binadamu wake."
Source: Jukwaa la siasa, Facebook.
My take;
Kwa maelezo haya, mzee wa anga alikurupuka kutoa maoni yake kwa pupa wakati chama kama oganaizesheni hakijakaa na kuijadili rasimu hiyo. Je, ni vipi kama chama kikija na moni tofauti na yale aliyo yatoa Mbowe?
Mzee wa anga hemu uwe na subira na uzitambue 'protoko' za chama, kwani unapoongea wewe kama Mbowe ujue una wakilisha CHADEMA kwa nafasi yako ya uenyekiti wa chama hicho.
Mzee wa anga mambo ya chama hayaendi hivyo.