kimbendengu
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 6,175
- 10,632
Jamani wanamichezo wenzangu hapa Tanzania michezo ya Olympic inaendelea huko Japan swali langu mbona watanzania sijawaona kwenye hiyo michezo?
Wakiweka medali za “most liked posts or most viewed videos” tutashiriki. Michezo yetu ni kwenye social media.Jamani wanamichezo wenzangu hapa Tanzania michezo ya Olympic inaendelea huko Japan swali langu mbona watanzania sijawaona kwenye hiyo michezo?
AiseeeWakiweka medali za “most liked posts or most viewed videos” tutashiriki. Michezo yetu ni kwenye social media.
Walioenda nadhani wote ni wa Marathon ambayo watakimbia tarehe 7 na 8
Walienda?Jamani wanamichezo wenzangu hapa Tanzania michezo ya Olympic inaendelea huko Japan swali langu mbona watanzania sijawaona kwenye hiyo michezo?
naam bila shaka marathon atashinda Eliud Kipchoge ndugu yetu toka KenyaMarathon itachukuliwa na ama wakenya au waethiopia au waganda.
Kuna michezo mingi sana ambayo watanzania wangeweza kushiriki iwapo wangeandaliwa vizuri shule za msingi na sekondari. Miaka ya nyuma wachezaji wazuri wengi walikuwa wanatokea huko kwenye mshaindano ya shule za sekondari, siyo mitaani kama ilivyo siku hizi.
Michezo kama kuendesha baiskeli, kupiga kasia, kupiga upinde, kuogelea, volleyball, mbio fupi, relay, mbio za kati, mbio za masafa marefu, kuruka chini, kuruka juu, kuruka kwa upondo, kutupa mkuki, kutupa tufe, ni michezo ambayo watanzania wangeweza kushiriki na kushinda iwapo wangekuwa wameandaliwa kuipenda tangu utotoni.