Mbona Watanzania sijawaona Olympics?

Kama tulipeleka watatu unategemea nini? inawezekana walishachujwa siku nyingi wako vijijini kwao, kufika stage ya kutafuta medali huwa lazima muwe mmepunguzwa kwanza.
 
Hii nchi miaka ya nyuma ndio ilikua imeendelea kadri miaka inavyosonga tunazidi kudidimia
 
Unawatafutia wapi?Viwanjani?
Huko hatupo..
Nenda kwenye malls ..huko ndo tunawakilisha..
Wanamichezo watatu... Viongozi 18.
Ndo zetu
 
Inashangaza yaani bora Uganda wameshabeba medali jamani inakera muda wote unachungulia huoni bendera yako
 
Jamani wanamichezo wenzangu hapa Tanzania michezo ya Olympic inaendelea huko Japan swali langu mbona watanzania sijawaona kwenye hiyo michezo?
Wakiweka medali za “most liked posts or most viewed videos” tutashiriki. Michezo yetu ni kwenye social media.
 
Walioenda nadhani wote ni wa Marathon ambayo watakimbia tarehe 7 na 8

Marathon itachukuliwa na ama wakenya au waethiopia au waganda.

Kuna michezo mingi sana ambayo watanzania wangeweza kushiriki iwapo wangeandaliwa vizuri shule za msingi na sekondari. Miaka ya nyuma wachezaji wazuri wengi walikuwa wanatokea huko kwenye mshaindano ya shule za sekondari, siyo mitaani kama ilivyo siku hizi.

Michezo kama kuendesha baiskeli, kupiga kasia, kupiga upinde, kuogelea, volleyball, mbio fupi, relay, mbio za kati, mbio za masafa marefu, kuruka chini, kuruka juu, kuruka kwa upondo, kutupa mkuki, kutupa tufe, ni michezo ambayo watanzania wangeweza kushiriki na kushinda iwapo wangekuwa wameandaliwa kuipenda tangu utotoni.
 
naam bila shaka marathon atashinda Eliud Kipchoge ndugu yetu toka Kenya

Ila hata mTz mwenzetu Simbu yuko vizuri Olympics Za Rio alimaliza nafasi ya tano ,sasaivi nina uhakika atleast bronze atachukua
 
Back
Top Bottom