[h=1]Majangaaa Mbona Majangaaa! - 5-6[/h]Kisha akajitingisha mwili wake kuonesha kwamba alikuwa mpana na kuifanya khanga aliyoivaa kutikisika kutokana na mtikisiko uliosababishwa na ‘boksi' lake lililokuwa limetanuka kisawasawa nyuma ya mgongo wake.
Wakati Eddy alipokuwa akikaribia kumfikia akajikohoza ili kuweka sauti yake katika ile hali aliyokuwa akiitaka yeye.
Alikuwa amedhamiria kutoa sauti ile yenye mvuto ambayo ingeweza hata kumtoa nyoka pangoni.
Nini kiliendelea? POROMOKA NAYO…
"Mambo?"
"Powa," alijibu Eddy akiwa ameshtushwa sambamba na kupigwa na mshangao kutokana na bashasha alizokuwa ameoneshwa na Rehema.
"Pole na mihangaiko…" Rehema alimwambia tena Eddy aliyekuwa bado akili yake haijakaa sawasawa kujua ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea.
"Asa… Asante," alijibu bila ya kujiamini.
Muda wote huo Rehema alikuwa akiitumia siraha yake ya macho, pamoja na kwamba giza lilikuwa limeshaanza kuingia lakini machao yake makubwa na meupe ‘pee' yalikuwa yaking'aa kama nyota ang'avu.
Ghafla, Rehema akalipokea gazeti lililokuwa limeshikwa na Eddy, wakati kijana huyo akiendelea kushangazwa na ukarimu huo, alijikuta akishikwa mkono na kukaribishwa ndani.
Baada ya kufika ukumbini, moja kwa moja Rehema ambaye alikuwa ametangulia mbele, akabadilisha mwendo, akawa anatembea kwa kulitingisha boksi lake kama vile alikuwa akitaka kuliangusha.
Mbaya zaidi kuna wakati alikuwa akisimama ghafla na kumgusa Eddy kwa makalio yake na kumchanganya.
Eddy alikuwa kama nyoka wa kibisa hakuwa na sumu kabisaaa, makali yake yote yalikuwa yamekwisha na ujanja wake ulikuwa umetiwa mfukoni kwani kama ni shambulio basi lilikuwa la ghafla sana kumkumba, hivyo hakulitegemea.
Hakuweza kujihami kwa njia yoyote ile, alibaki akipelekwa kama gari bovu lililokuwa limekatika breki.
Bila ya kutarajia akajikuta akiingizwa chumbani kwa Rehema badala ya kuelekea chumbani kwake.
"Karibu…" alisema Rehema kwa sauti laini ya kuweza kumpagawisha mwanaume yeyote rijali.
Eddy hakuamini kile alichokiona chumbani humo, kilikuwa chumba kikubwa kilichokuwa katika mwanga hafifu wa rangi nyekundu na kumfanya ashindwe kukiona kila kitu katika uhalisia wake.
Alijaribu kuzungusha macho yake ndani ya chumba hicho kila pembe, alipomaliza akaanza kumwangalia mwanamke huyo ingawaje kwa kumwibia.
Eddy mbele yake kila kitu kilikuwa kizuri, alivutiwa na kila kitu, alivutiwa na macho ya Rehema yaliyokuwa yaking'aa, alivutiwa na rangi ya mwanamke huyo, akavutiwa na umbile lake.
Eddy alishangazwa na uzuri wa Rehema ambaye kwa wakati huo aliuona uzuri wake ulikuwa umezidi maradufu ya siku alipomuona kwa mara ya kwanza mchana.
"Karibu sana...." sauti laini iliyakatisha mawazo ya Eddy na kuyafanya arejee chumbani humo.
Pamoja na usiku huo kutaliwa na kibaridi cha haja lakini kijasho chembamba kilianza kumtoka nyuma ya mgongo wake kutokana na uti wa mgongo wake kupatwa na mshtuko.
"Utakunywa nini…?" Wakati Rehema akiuliza swali hilo tayari alikuwa ameshafika kwenye kochi alilokuwa amekaa Eddy na kuinama kwa heshima akiwa amepiga magoti akimwangalia kwa macho yake makali ambayo yalikuwa na uwezo wa kuyaona hata mapigo ya moyo ya mwanaume huyo yalivyokuwa yakienda kwa kasi.
"Nitakunywa chochote…" alisema Eddy akiwa amejiinua kidogo katika kochi na kisha kujirudisha tena chini.
"Usijali, nitakupa juisi ya ndimu…" alisema Rehema na kusimama kisha akainuka na kukifuata kijokofu kidogo kilichokuwa katika kona ya chumba hicho.
Pamoja na utoto wake wa mjini, Eddy hakujua kama duniani kulikuwa na juisi ya ndimu, hakuamini alipoambiwa kwamba analetewa juisi hiyo.
Kama kawa Rehema hakuacha kulitingisha boski lake pale alipokuwa akimpa mgongo kijana huyo na kufuata kile alichokuwa akikifuata, hali iliyokuwa ikimweka katika wakati mgumu sana Eddy.
***
Awali ‘paka' wa Eddy alikuwa akishindwa ‘kulia nyau' lakini kadiri muda ulivyokuwa ukisonga mbele ndivyo alivyoyazoea mazingira na paka wake akaanza kututumka na kuvimba huku akilia nyau baada ya kuona kwamba kulikuwa na kila dalili za kula ‘samaki'.
Rehema alirudi na juisi iliyokuwa ndani ya glasi, ambayo hakutaka kuiweka juu ya stuli wala hakutaka kuiweka juu ya meza iliyokuwa hatua chache kutoka alipokuwa amekaa Eddy.
Akakaa katika kochi sehemu ya kuwekea mikono na kuishika vyema glasi hiyo na kuipeleka kinywani kwa kijana huyo.
Eddy hakuwa na ujanja, akaachia mhemo wa nguvu na kisha akatanua kinywa chake na kuipokea juisi hiyo na akanywa funda moja.
Hakutegemea utamu wa juisi hiyo, akiwa anatafakari akapewa tena, naye hakijivunga akapiga funda lingine, hakutarajia kuipata radha aliyoipata, ilikuwa ni juisi nzuri iliyochangamsha mdomo na mwili wake kwa jumla.
Hali iliendelea hivyo mpaka juisi ilipoisha, mpaka hapo akawa ameshaelewa kwamba alikuwa ametekwa kimapenzi na Rehema.
Akajiuliza maswali mengi, hakuamini kama alistahili kufanyiwa yote aliyokuwa akifanyiwa lakini hakuwa na budi kukubali kila alichokuwa akifanyiwa na binti huyo mwenye umbile matata.
"Unaitwa nani vile…?" Rehema alijifanya hamjui vyema Eddy.
"Eddy… Eddy Manyara… mtoto wa pili kwa mzee Manyara…" kijana huyo alijikuta akishusha historia yake kwa ufupi. Kutokana na hali aliyokuwa nayo angeweza kusema kila kitu alichokifanya alikuwa amepagwa na mambo machache aliyokuwa amefanyiwa kwa muda mchache.
Eddy akaamini yale yote aliyokuwa akiyasikia mitaani kwamba wanawake wa Kitanga ni noma katika mahaba, akajua amepatikana ingawaje hakuwa akijua Rehema ni kabila gani.
***
Wakati yote hayo yakitendeka Irene alikuwa amelala chumbani mwake fikra zake zikipanga mikakati ya kumnasa Eddy ili kumdhihirishia Rehema kwamba yeye ni kiboko yake .
Akiwa amejilaza kitandani, ghafla mlango wake ulifunguliwa, akaingia mdogo wake aitwaye Patricia akionekana kama kuwa na ujumbe mahususi kwa ajili yake.
"Vipi?"
"Dada nimekuja…"
"Kwa heri au kwa shari…"
"Kwa kweli sijui kama ni kwa heri au kwa shari."
"Kwa nini?"
"Nataka nikwambie kitu cha ajabu nilichokiona…"
"Kitu gani?"
"Ni kuhusu dada Rehema na yule mgeni wa chumba…" Patricia aliposema hivyo tu, kwa kasi ya ajabu Irene aliinuka kutoka katika kitanda na kujikuta amekaa katika tendegu la kitanda.
Nini Kiliendelea? Utamu unaanza kukolea polepole, usikose kufuatilia Alkhamis ijayo................