Majangaaa Mbona Majangaaa! - 4-
Rehema alimpiga jicho kali Irene kwa kumshusha na kumpanisha kisha akaenda zake kuelekea
uwani hali iliyomfanya Irene kufadhaika, moja kwa moja akajua kuwa ameingia kwenye vita na
malkia wa nyumba hiyo.
Irene alijaribu kufikiria ni nini kimetokea kati yake na Rehema lakini hakuambua kitu. Alifikiria
labda jana yake alikuwa amemkosea, pia hakukumbuka kutokea kitu kama hicho.
Hivi huyu brother men anaweza kuwa chanzo? alijiuliza akimfikiria Eddy.
NINI KILIENDELEA? POROMOKA NAYO
Irene akiwa katika mawazo hayo akasema kama kweli chanzo ni huyo kijana, basi atahakikisha kwamba anakula naye sahani moja ili kuzidi kumvimbisha mashavu Rehema.
Malkia malkia
wala sitajali kama ni malkia wa nini, watu tumewaona mamalkia wa maana atakuwa yeye malkia wa vichochoroni, alisema Irene na kisha akaachia msonyo wa nguvu uliosikika hadi nyumba ya pili.
Wakati huo alikuwa ameshaingia chumbani kwake na kuanza kujikwatua kwa kuupara uso wake kwa mapambo ya kila aina ambayo yalipaswa kuingia usoni pake.
Wakati akiendelea kujipamba kila dakika ilivyokatika ndivyo alivyokuwa akikikumbuka kitendo alichofanyiwa na Rehema.
Alikasirika sana kuona anamsalimia halafu anamvimbishia mashavu bila ya kujua sababu, kila alivyokumbuka kitendo hicho aliachia msonyo na kuendelea na shughuli zake.
Asubuhi asubuhi mtu anakuharibia siku, alijisemea peke yake Irene wakati akijiangalia kwenye kioo kisha akaachia msonyo mwingine.
****
Kwa upande wake, Rehema roho yake ilikuwa imemchafuka, ikimchonyota kwa kumuona Irene akitoka chumbani kwa Eddy, moja kwa moja akajua kuwa wawili hao watakuwa wamelimenya tunda la mwituni asubuhiasubuhi.
Haiwezekani lazima watakuwa wamepeana kile kitu roho inapenda, iweje atoke chumbani kwake asubuhi yote hii? alijihoji na kukosa jibu la uhakika.
Rehema alikuwa amechukia kwelikweli na moyo wake ulimuuma kwa kuona kwamba Irene anaanza kuwa na uhusiano na mwanamme huyo mgeni kabla yake.
Atakuwa ameingia asubuhi ileile au atakuwa amelala chumbani kwake? alijiuliza tena Rehema huku donge likiwa limemnasa rohoni mwake.
Yaani atakuwa ameshanizidi kete? aliwaza Rehema ambaye aliamini kabisa kwamba mitego aliyomtega Eddy siku ya kwanza ilikuwa ni lazima amnase kwanza kabla ya kinyangaratika kingine ndani ya nyumba yao.
****
Kwa upande wake Eddy ambaye alitoka baada ya kujipulizia utuli uliouteka ukumbi wa nyumba hiyo, alikwenda moja kwa moja kwenye shughuli zake kubaingiza, kwa kuwa bado hakuwa na kazi ya kufanya.
Alikuwa akifanya kazi yoyote ambayo aliamini kuwa ingeweza kumwingizia kipato.
Siku hiyo alikwenda moja kwa moja hadi kijiweni kwake maeneo ya Kariakoo ambako vijana wengi hukutana na kuuza maneno kwa watu wengine ili wapate chochote kitu.
Moyoni mwake Eddy hakuwa salama hata kidogo, kwa kuwa vitendo viwili vilikuwa vikimchanganya akili yake kwani moyo wake ulikuwa ukiripuka kila alipokuwa akikumbuka jinsi alivyomuona Rehema akisugua kisigino chake ilhali amevaa khanga moja iliyokuwa imelowana sehemu za makalioni.
Moyo ukitulia unaripuka tena kwa kitendo cha Irene kuingia chumbani kwake akiwa na khanga moja ambayo nayo ikiwa imelowana, Eddy alivuta taswira za mabinti hao wawili na kubaki akiwa hana la kufanya.
Kila mmoja ana uzuri wake
Eddy aliambia nafsi yake na kubaki na dukuduku moyoni mwake. Mpaka wakati huo hakuwa akijua kama amesababisha songombingo kati ya wasichana wawili hao.
Hilo hakulijua kwa kuwa hakuliona wakati likitokea, kwa sababu alikuwa chumbani kwake, laiti kama angeliona angejua cha kufanya, asingekuwa na budi kuchagua upande mmoja.
Lakini moyo wa Eddy ni kama wa wanaume wengine, haukulidhika na mmoja, unataka kumi na moja kwa kutaka kuonja kila sehemu ili kujua radha yake.
Eddy alikuwa akitaka kujua utamu wa Rehema lakini pia alikuwa akitaka kujua utamu wa Irene kwa kuwa damu yake ilikuwa ikichemka, kikubwa alikuwa akijiuliza itawezekanaje ndani ya nyumba moja!
Hilo ndilo lililokuwa likimitia mashaka, vinginevyo alikuwa akiwataka mpaka wengine waliokuwa wakiishi ndani ya nyumba ile kwani aliamini kuwa kila mti una tunda lake na kila tunda lina utamu wake.
Eddy alikwenda mjini na kuzugazuga kwa jamaa zake maeneo ya Shule ya Uhuru Karikooo, huko alikutana na marafiki zake Spider au Raha na John Tupatupa na kuongea nao kile kilichomkuta katika nyumba ile aliyohamia.
Hapo lazima ucheze kama Pele lakini kwa jinsi unavyonihadithia kitu hapo ni Rehema
alisema Raha.
Mmmh mwana usipepese macho wala kuuma meno, hapo kitu ni Irene
aliongeza John Tupatupa ambaye alimlaumu Eddy kwa nini hakumaliza mchezo wakati mzigo ulipoingia chumbani.
Washikaji sasa mnanichanganya
niacheni nitumie akili yangu, Eddy aliwaambia baada ya kuona kila mmoja akiwa na mtazamo wake kuhusiana na mabinti hao.
****
Rehema hakuwa ameridhika, alipofika uwani alipishwa kwenda msalani na mabinti waliokuwa katika foleni kwa kuwa yeye ni malkia wa nyumba hiyo.
Akaoga na kumaliza haja zake muhimu, kama kawaida alipotoka alisugua miguu yake huku akiwa na hamu ya kutaka kujua Irene aliingiaje chumbani kwa Eddy.
Alipomaliza shughuli zake akamchukua mmoja wa mabinti waliokuwa wakisubiri kwenda kuoga na kumwambia amfuate chumbani kwake.
Binti akajua labda ametafutiwa mtu wa kuduu naye, akawa na wasiwasi wakati alipokuwa akiambiwa kuingia chumbani kwa malkia.
Usiogope kaa hapo kwenye sofa
alisema na binti akiwa na wasiwasi akaketi.
Ulimuona Irene leo?
Ndi
ndi- yoooo, nilimuona dada
Ulimuona wakati gani?
Alipokuwa akitoka kuoga
Hukumuona alipoingia chumbani kwa yule mgeni
?
Wala sikumuona lakini kama aliingia atakuwa alikwenda kumrudishia sabuni yake
Kwani alichukua sabuni kwake?
Eeeh wakati akiwa anatoka kuoga yule mkaka, dada Irene akamuomba sabuni ya kuogea
alisema binti yule na kuifanya roho ya Rehema kuanza kupona kidonda cha wivu kilichokuwa kikimkereketa.
Oke nenda, usimwambie yeyote nilichokuuliza.
Sawa.
Baada ya binti yule kutoka nje, Rehema alifurahi sana, akajua kuwa Irene hakuwa ameambulia kitu. Akafurahi na kujitupa kitandani na kukumbatia mito.
Je nini kiliendelea? Usikose kufuatilia Alkhamisi ijayo...................