Mbona harakati za kuidai Zanzibar huru ni kama zimekufa awamu hii?

Kwa muda mrefu tangu muungano wa Tanganyika na Zanzibar hawa ndugu zetu kutoka Zanzibar wamekuwa hawaridhishwi na huu muungano, inasemakena hadi Rais wa kwanza wa Zanzibar alishawahi sema muungano ni kama koti likikubana unalivua.

Pia nakumbuka awamu ya 4, Rais akiwa Kikwete kuliibuka wimbi kubwa sana la wanaharakati kutoka Zanzibar wakiongozwa na jumuia ya UAMUSHO wakidai Zanzibar inatakiwa kuwa huru eti kisa viongozi wao wanachaguliwa kutoka Tanganyika.

Lakini jambo la ajabu awamu hii ya sita ni kama hakuna tena hizi harakati za kuvunja muungano wetu mtukufu sasa najiuliza je, shida ilikuwa nini kwa hizi harakati na imekuaje awamu hii zisisikike tena? Au ulikuwa ni unafiki tu wa wanasiasa na sasa hivi wameona huu muungano unawanufaisha na wao!

Kwa mtazamo wangu muungano huu Zanzibar ndiyo wana manufaa kuliko Watanganyika hivyo wanapaswa kuupigania ili uendelee na wao wazidi kunufaika.

Mzanzibar ana haki ya kumiliki ardhi Tanganyika wakati Mtanganyika hana hiyo haki Zanzibar. Je, nani hapo ananufaika? Nawaomba tena Wanzanzibar waache unafiki huu muungano wao ndiyo wanufaika.

MUUNGANO UDUMU MILELE.

Mbona unasema usiyoyajua au kusudi ya mada yako ni kutafuta uchokozi tu? Suali la wazanzibari kudai uhuru wetu bado linaendelea kwa nguvu sana, na kwa taarifa yako hivi sasa kuna kesi umeshafikishwa UN (umoja wa mataifa) na umoja wa mataifa wame acknowldege kuwepo kwa madai yetu. Ukiwa unachouliza ni kuwa mbona hamjakamata ndugi zetu, mkawatesa na kuwaua toka awamu hii ya sita ni kwa sababu wazanzibari wameamua kubadili mfum wa kudai haki zao.

Tukija katika suali la manufaa ya muungano, umenishangaza sana sana kutowa mfano wa umilikaji ardhi tu na kusema kwa sababu hiyo wazanzibari wananufaika zaidi katika muungano. HIyo ni conclusion dhaifu sana na itanichukuwa muda mrefu kama nitakaa hapa na kuanza kukueleza uzito wa disadvatanges na wepesi wa advantages za muungano kwa zanzibar,

Hata hivyo, hebu nikupe mifano midogo tu, Kwa miaka yote aliyotawala magufuli kama rais wa tanzania (rais wa zanzibar na tanganyika) amefanya miradi chungu mzima kuanzia maji, maskuli, barabara, zahanati, mabasi ya mwendo kasi, ununuzi wa ndege na kadhalika, jee ni yepi kati ya hayo unadhani rais wa tanzania ameyafanya visiwani zanzibar kwa pesa za Tanzania? Kumbuka alikuwa raisi wa tanzania, akiongoza tanzania kwa manufaa ya watanzania. Hakufanya lolote kwa zanzibar! kajengesha uwanja wa ndege kwao ambako hakuna haja yeyote ile na kashindwa kuziba mashimo ya barabara za pemba! Kaleta ndege za shirika la ndege la Tanzania lakini alishindwa kupeleka hata ndege moja zanzibar ilhali bila ya zanzibar hakuna tanzania na bila ya tanganyika.... well hakuna tanganyika. Ajabu Samia alipopeleka ndege mbili Zanzibar nyooote mkaanza kulia. Sasa tizama hayo tu, wazanzibari hapo walinufaika na nini hasa?

Sitaki hata kusema lolote lile juu ya kikwete kwani taarifa ziko nje nje kuwa kwa muda wake wate wa utawala percentage ya misaada ya kifedha pamoja na mikopo kutoka nje za nje kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania (TANganyika na ZANzibar ia) ambazo zilivuka bahari ni ndogo mno kiasi cha kuwa unaweza kuwa hazikuwepo! Sasa hayo ndio manufaa ya muungano kwa zanzibar?

Mwisho naomba kurudi katika point yako ya umiliki wa viwanja, watu kama nyiyi sisi tunawahitaji sana katika kampeni zetu za serikali tatu. Kwa hivyo endeleeni kulipigia kelele suali hili. Lakini tu kwa sasa kwa vile kuna serikali mbili na uraia wa aina mbili tu usitegemee kubadilika kitu. Mimi ni mzanzibari nina haki ya kumiliki ardhi nchini kwetu, wewe si mzanzibari huna haki ya kumiliki ardhi nchi ya ugenini. Mimi ni mtanzania nina haki ya kumiliki ardhi popote katika nchi yangu ikiwemo sehemu yeyote ile ya tanzania bara. wewe ni mtanzania unahaki ya kumiliki ardhi popte katika nchi yako. Tatizo ni kuwa huwezi kumiliki ardhi zanzibar kwa sababu wewe si mzanzibari ingawa zanzibar ni sehemu ya tanzania. Nimekuchanganya? kwa muhtsari ni hivi mimi ni mzanzibari nina haki ya kumiliki ardhi, mimi ni mtanzania nina haki ya kumiliki ardhi tanzania, wewe si mzanzibari huna haki ya kumiliki ardhi zanzibar. Zanzibar ni nchi!!!! Ni nchi ndogo lakini still si mkoa wa tanzania. Usitulaumu sisi mlaumu Nyerere kwa namna alivyoufanya mfumo wa muungano, pia walaumu viongozi wa ccm wanaokataa kubadili mfumo wa muungano.
 
Tatizo kubwa la Wazanzibari ni ELIMU ELIMU ELIMU
Tatizo kubwa la wadanganyika ni UJUHA UJUHA UJUHA! Mmezoea kudanganywa na msakuwa summu bukmun fahum la yarjiuun. Mlianza kudanganywa toka enzi za maji maji na hadi leo hii hamjui kutumia akili kufikiri outside the box. Mume baki kushangiria lolote lile asemalo kiongozi wenu japo kuwa ni uongo au sio sahahi na deep down mnajua kuwa ni uongo au sio sahihi. As long as mkiambiwa ccm oyeee! tanzania oyeee! basi mnakwenda tu mazumbumbu!
 
Back
Top Bottom