Mbona harakati za kuidai Zanzibar huru ni kama zimekufa awamu hii?

Mimi nilikuwa naomba tupate muda at least wa miaka mitano ya mpito tutengane tujitafakari upya ili tukirudi tukae mezani vzr
 
Kwa muda mrefu tangu muungano wa Tanganyika na Zanzibar hawa ndugu zetu kutoka Zanzibar wamekuwa hawaridhishwi na huu muungano, inasemakena hadi Rais wa kwanza wa Zanzibar alishawahi sema muungano ni kama koti likikubana unalivua.

Pia nakumbuka awamu ya 4, Rais akiwa Kikwete kuliibuka wimbi kubwa sana la wanaharakati kutoka Zanzibar wakiongozwa na jumuia ya UAMUSHO wakidai Zanzibar inatakiwa kuwa huru eti kisa viongozi wao wanachaguliwa kutoka Tanganyika.

Lakini jambo la ajabu awamu hii ya sita ni kama hakuna tena hizi harakati za kuvunja muungano wetu mtukufu sasa najiuliza je, shida ilikuwa nini kwa hizi harakati na imekuaje awamu hii zisisikike tena? Au ulikuwa ni unafiki tu wa wanasiasa na sasa hivi wameona huu muungano unawanufaisha na wao!

Kwa mtazamo wangu muungano huu Zanzibar ndiyo wana manufaa kuliko Watanganyika hivyo wanapaswa kuupigania ili uendelee na wao wazidi kunufaika.

Mzanzibar ana haki ya kumiliki ardhi Tanganyika wakati Mtanganyika hana hiyo haki Zanzibar. Je, nani hapo ananufaika? Nawaomba tena Wanzanzibar waache unafiki huu muungano wao ndiyo wanufaika.

MUUNGANO UDUMU MILELE.
wakati unahoji kwanini hawalalamiki wakati huu tafuta majibu kwanini walilalamika wakati ule.
Methali: ukimtupia mtu mchanga jichoni machozi yatamtoka lakini ukimtupia punje za karanga atazitafuna taratibu...
 
Back
Top Bottom