Mbona Dkt. Mwigulu haeleweki? Yaaani madeni ya sekta binafsi ni ya Serikali? Mmemuelewa Watanzania?

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Sep 13, 2020
3,166
4,581
Haeleki kabisa
Screenshot_20221211-171140.jpg
 
Mbona mimi nimemuelewa!...Yaani mfano mzuri ni huu let say deni la nyumba x=Sh 15 mpangaji namba 1 sh 5,mpangaji namba 2 ni sh 10,kila mpangaji atalipa deni linalomuhusu mwenyewe bila ya kujumlisha deni la mwenzie yaani ndio kama hivyo Serikali italipa deni lake na sekta binafsi italipa deni lake kwahiyo jumla ndio deni la taifa(deni la nchi ya Tz )
 
Duh aisee yako mengi siyajui kumbe...sasa nauliza wenyewe wakikopa wanaweka nini bondi au ndo vitu walivyowekeza?ebu wataalam wa masuala ya uchumi tutoeni tongotongo
Huwezi kuwaelewa mkuu wakiona unawabana wanakuchanganya zaidi.
Tulianza tutanunua behewa used mpya zitakuja 2023.
Ikaja behewa ni used
Ikaja behewa zimenunuliwa bei juu.
Ikaja behewa hizi ni mpya
Tukamaliza anayepotosha kuwa behewa si uswd atachukuliwa hatua.
Yani full kutuchanganya
 
Mbona mimi nimemuelewa!...Yaani mfano mzuri ni huu let say deni la nyumba x=Sh 15 mpangaji namba 1 sh 5,mpangaji namba 2 ni sh 10,kila mpangaji atalipa deni linalomuhusu mwenyewe bila ya kujumlisha deni la mwenzie yaani ndio kama hivyo Serikali italipa deni lake na sekta binafsi italipa deni lake kwahiyo jumla ndio deni la taifa(deni la nchi ya Tz )
Deni la mwenye nyumba linajumlishwa na la mpangaji? Wakati kila mtu ana deni lake?
 
Hapa kuna maswali ya kujiuliza.

Hayo makampuni ni yapi?

Na je, yamewekewa dhamana na serikalli?

Kama ndio, kwanini makampuni binafsi yakopeshwa kwa kudhaminiwa na serikali?

Kama CAG hakagui hesabu za mashirika binafsi, inakuwaje deni la makampuni binafsi kuingizwa kwenye deni la Taifa?

Je, huu ni utaratibu mpya au ulikuwepo tangu zamani?
 
Mkuu Kama shule ilikupiga kusho huwezi elewa chochote. Hii ni lecture ya mwaka wa pili wanaodoma B.A economics au finance.

National debt= public debt + private companies' debts.

Hivyo alichosema mwigulu ndoshule yenyewe.
Mkibanwa sana mtakuja na formula za uchumi utadhani deni la Taifa limeanzia kwa Mama enu.
 
Mfano wangu unaeleweka acha ligi!! Hitimisho la hapo ni kwamba kila mtu atalipa deni linalomuhusu bila kujali jumla iliyojumlishwa kwa wote
Mimi mfano wako siukubali. Twende taratibu. Mr. & Mrs. X wamekopa millioni mia nane benki kujenga nyumba za kupangisha. Wamewapangisha watu 20, na katika hao tuseme wote hawajalipa kodi ya miezi miwili na wanadaiwa millioni 6. Deni la millioni 6 ni la wapangaji wanaodaiwa na mwenye nyumba. Hili deni haliwezi kuongezwa katika deni la mwenye nyumba alilokopa benki. Ila linaweza kuongeza deni kama mwenye nyumba atashindwa kulipa pesa aliyotakiwa kulipa benki mwezi huo, na benki ikampiga faini ya 0.9% ya pesa aliyotakiwa kulipa.

Mikopo binafsi nayo iko kama nilivyoeleza juu. Kuna wakati, serkali inaweza kupata mikopo kutekeleza miradi fulani katika nchi. Hii miradi mara nyingi inatekelezwa na sekta binafsi (na mashirika ya umma). Mwisho wa siku sekata binafsi hutakiwa kuilipa serkali na serkali kulipa huko ilikokopa. Nakumbuka katika miaka ya 80/90 serkali ilipata pesa nyingi toka (nadhani) benki ya dunia kufufua zao la mkonge. Hiyo pesa ilipewa sekta binafsi ili kufufua kilimo cha mkonge. Hiyo mikopo ilichukuliwa, wakapewa mashamba mkonge, lakini badala ya kufufua hicho kilimo hiyo fedha yote iliingizwa kwenye shughuli nyingine. Tena hiyo pesa walipewa kama foreignm currency credit facility. Wahindi wengi waliipokea hii pesa na wengine walikimbilia Cana/Uingereza na wengine hadi leo wako TZ na ni mabillionea na hiyo pesa hawakulipa.

Pesa kama hiyo hapo juu ni mkopo wa serkali hata kama mtumiaji ni mtu binafsi na huwezi ukajumlisha hela waliopewa sekata binafsi kama mkpo unaojitegemea.
 
Duh aisee yako mengi siyajui kumbe...sasa nauliza wenyewe wakikopa wanaweka nini bondi au ndo vitu walivyowekeza?ebu wataalam wa masuala ya uchumi tutoeni tongotongo
Ndiyo akina Chavda wa kitambo hiki
 
Back
Top Bottom