Mbinu ya Israel kuua viongozi wakuu wa kisiasa na kijeshi ina faida kimedani au ipo tu kujitwalia ujiko ?

Mbinu ya Israel kuua viongozi wakuu wa kisiasa na kijeshi ina faida kimedani au ipo tu kujitwalia ujiko ?

Mi mi

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
5,752
Reaction score
10,523
Israel imekua ikitumia mbinu wa kuua viongozi wa juu kisiasa au kijeshi katika serikali[ Iran ] na makundi hasimu kama Hamas,Hezbollah,Houthi je, mbinu hii ina faida kimedani kwao au ipo tu katika kujizolea ujiko kwa jeshi lake ?

Toka Israel imeanza kuua viongozi hao ni kipi kilicho badilika katika serikali[ Iran ] na makundi kama Hamas,Hezbollah na Houthi ?

Je, misimamo yao imebadilika juu ya Israel ?

Je, makundi hayo yameingia katika migogoro ya ndani ya kiutawala ?

Je, kumetokea kuto kuelewana katika utoaji wa amri za kimashambulizi katika makundi hayo ?

Israel katika vita vya siku 12 na Iran ilianza kwa kuua viongozi wa ngazi za juu za kiutawala katika jeshi na serikali ya Iran. Je, Israel ilipata faida gani baada ya kufanya hivyo ?

Mbinu ile ile wameirudia tena katika vita vya sasa kwa kumuua kiongozi mkuu wa kidini wa Iran. Je, shambulizi hilo limebadili nini mpaka sasa kwa Iran au limeipa faida gani Israel mpaka sasa ?

Bado Israel ina sisitiza itaendelea kuwaua viongozi wote wa kidini watakao chaguliwa Iran sasa je, Israel inapata faida gani kwa maamuzi haya kama wataendelea kuua kila kiongozi atakae chaguliwa je, maamuzi yao haya yana badili nini katika utawala wa Iran kiasi kwamba iwe faida kwa Israel.

Jambo la kukumbusha Israel imeua viongozi wa Hamas karibu wote lakini mwisho wa siku ili rudi mezani kuzungumza na Hamas juu ya mahitaji yao kwa maana nyepesi mbinu yao ya kuua viongozi wa Hamas imeshindwa kufanikisha wao kuyatimiza malengo yao yote katika vita vya Gaza mpaka sasa.

Hivyo hivyo kwa Hezbollah tunaiona Hezbollah leo ipo na inaendelea kupambana na Israel huko mpakani pamoja ya kwamba viongozi wao wakuu huuawa mara kwa mara.

Pia kwa Houthi licha ya kuuawa viongozi wao ila bado kundi hili lipo na misimamo yake ile ile.

Hiki ndicho nacho kiona kwa Iran mpaka sasa.

Sasa kwanini Israel inaendelea kuamini katika mbinu hii ambayo ijaleta matunda kwao mpaka sasa kwa makundi yote aliyo pambana nayo na kwa serikali ya Iran mpaka sasa ?
 
Kwa Israel Iran ikisambaratika kama Libya, Sudan au Somalia huwa kwao ni ushindi tosha
Hamas,Hezbollah,Houthi zimesambaratika ?

Tuanze kwanza kwa hawa sungura kabla hatujafika kwa tembo ili tujue mbinu yao Israel imeleta matokeo ama laah ?!.
 
Ni mbinu za kizamani,ukimuua mfalme umeshinda vita
Hii ni mbinu ambayo Ukraine aliitumia mwanzo katika vita vyake na Urusi alikuwa akilenga majenerali wa Urusi lakini haikuzuia jeshi la Urusi kuendelea ku kwapua maeneo yao Ukraine sijui baadae Ukraine aliona hakuna faida kwa hii mbinu maana ilipotea ghafla tofauti na mwanzo
 
Hii ni mbinu ambayo Ukraine aliitumia mwanzo katika vita vyake na Urusi alikuwa akilenga majenerali wa Urusi lakini haikuzuia jeshi la Urusi kuendelea ku kwapua maeneo yao Ukraine sijui baadae Ukraine aliona hakuna faida kwa hii mbinu maana ilipotea ghafla tofauti na mwanzo
Ni mbinu ya kuji-mwambafy tu
 
Naongolea Iran,
Gaza na Yemen zimesambaratika.
Baada ya Israel kuua viongozi wa juu wa Iran katika vita vya siku 12 kitu gani kili sambaratika ?

Hapo Gaza Hamas imesambaratika ? Na huko Yemen Houthi imesambaratika ?
 
Lengo ni kupiga kichwa kondoo watawanyike

Au kulazimisha succession ambapo huenda akaingia mtu katika kiti cha power kutoka katika chaina ya succession ambaye ni pandikizi lao.

Kutia hofu uongozi usarende
 
Kwa Israel Iran ikisambaratika kama Libya, Sudan au Somalia huwa kwao ni ushindi tosha
Hayo makundi tajwa hapo juu Yalisha wahi kusambaratika lini !? Kama haya jawahi kusambaratika ndio mtoa mada anahoji Israel hawaoni kwamba mbinu Yao Haina faida !?
 
Lengo ni kupiga kichwa kondoo watawanyike

Au kulazimisha succession ambapo huenda akaingia mtu katika kiti cha power kutoka katika chaina ya succession ambaye ni pandikizi lao.

Kutia hofu uongozi usarende
Toka ameanza kupiga vichwa vya Hamas,Hezbollah,Houthi na Iran kipi kimebadilika ?
 
Hakuna zaidi ya Ujinga wa kizayuni ndiomana hataki kuafiki Amani ya kweli na Palestine!!

yeye akijiona ni mwenye nguvu zaidi lkn Vita vinawafanya waishi kwenye mateso miaka kwa miaka!!!.

Chini ya juu hakuna Binadamu wenye haki zaidi ya wengine

Wapalestina wameteseka lkn kilio chao Dunia imekisikia wanapewa misaada!! Wengine wanaandamana kupinga wanachofanyiwa!!!


sawa tu na Mateso ya Makaburu kwa raia wenyeji wa Africa kusini mwisho kilio chao kilisikika na Dunia ikawasaidia wasiwe wanyonge ndani ya Dunia yetu pamoja..
 
Back
Top Bottom