Mbingu saba, siri na nguvu ya namba saba

Hakuna kitu kama hicho, dini unayozungumzia si ya mungu, ushahidi wewe mwenyewe unaona kinachoendelea duniani kwa sasa, kubisha ni ubinadamu tu.
Sio lazima uamini usichoamini ndio maana wengine wanaamini siku ya sabato na wengine hawaikubali
 
Nimegundua kitu kimoja naona tunaenda njia tofauti aidha hunielewi kama wengine ama hatuelewani au tunaweza kuwa tunazungumzia kitu kilekile kwa approach tofauti
Hali inapofikia hapa inabidi kukubaliana kutokubaliana ili tuweze kuendelea na mengine
Basi sawa lakini pia uchambuzi ni muhimu sana kwavile kupokea jambo bila ya kuhoji ni kama tuko kanisani vile padri akisema jambo nfo linakua hilo hilo hakuna kuhoji! Ila hili jambo nitaendelea kusimamia msimamo huu kwavile kuna mambo mengine ipo nje ya uwezo wetu.
 
"the most powerful man is the 7th son of the 7th son" 😀😀😀😀 movie tu
 
Asante upo sahihi na ndio maana ya kuwa na mijadala kama hii
 
Uzury wa jambo ni prouv sasa unaweza kutupa hiyo prouv? Maana mimi nachosema kuna moja anajua alipokua wakati hajazaliwa? Mnasema ndo kiza chenyewe sasa unajuaje kama uko kizani? Jamani [emoji3] [emoji3]

Hebu fikiria umefunikwa macho kwa kitambaaa kizito kisha ukapelekwa porini kabla hujafunguliwa unaweza ukawa unajua mahala ulipo? Na baada ya kufunguliwa unaweza ukahisi sasa kuwa haya mazingira niliyopo pasi shaka ni porini baada ya mwanga kuuona.
 
Mkuu Mshana alishasema, sio giza hili bali la kiroho.
 
Hebu elezea kidogo zaidi watu waste kuelewa hizi mambo .
Watanzania wake enlightened
 
Hebu elezea kidogo zaidi watu waste kuelewa hizi mambo .
Watanzania wake enlightened
Mungu aliumba dunia na vyote vilivyomo kwa siku tano kwa kutamka tu na ikawa.. Siku ya SITA akamuumba mwanadamu kwa udongo kisha akampulizia pumzi ya uhai
Katika ulimwengu wa roho wanyama na vingine vyote vyenye uhai vinawekwa kwenye kundi la hayawani, ufahamu wao utaishia siku ya tano, binadamu si hayawani ana utashi kwakuwa alipuliziwa pumzi ya Kimungu lakini akanyimwa siri ya siku ya saba Mungu alipopumzika
Je ni kweli Kuna Mungu alipumzika siku ya saba? Fumbo lile la Eden mambo ya Freemasons na Satanism yana mizizi kwenye hili
 
Mwanga upo Ndani ya Giza, na ndio maana mwanga hupotelea tena gizani ambako ndiko ulipotoka.
Kimoja lazima kiwepo ili nakingine kiweze kiwepo.. Asante
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…