Mbingu na ardhi vimejitenga rasmi, kelele nyingi na propaganda uchwara avichezi mpira uwanjani!

Majok majok

JF-Expert Member
Aug 3, 2023
618
1,565
Nafikiri Sasa jibu limepatikana ya kwamba ukija kucheza na yanga usije kichwa kichwa Kama vile unaenda harusini, unaweza kupigwa kipigo Cha mbwa mwizi kwa maana wanao wachezaji wenye ubora mkubwa sana hasa hasa viungo wao ni hatari kuliko corona!

Simba wameingia kucheza Kama vile wanacheza na jkt Tanzania, na walivyopata goli la kibu Denis ndio wakaona kabisa kwamba wamemaliza mechi lakini Master gamond alikuwa ashawasoma na anajua beki zao ni majanga makubwa alichokifanya ni kuwaambia waongeze Kasi viungo na timu ipeleke moto na akafanikiwa!

Robertinho anahojiwa anasema mchezaji wake muhimu kibu Denis alitoka ndio maana mambo yakabadilika, nimeshindwa kumuelewa kwa maana timu nzima inamtegemea kibu? Kasajili wachezaji 30 Ina maana hao wote ni maboya? Anashindwa kuukubali ubora wa mpinzani wake kwamba ni wa viwango vikubwa, kupoteza kwao kule tanga na kupigwa na ihefu sio kipimo Cha kuiondolea yanga ubora wake, ubora unabaki pale pale na unapoleta dharau ndio unakula kipigo Cha Rukaya Kama ivyo!

Sijawai Kuona mvua inacheza mpira lakini mashabiki wa mwakarobo badala ya kupiga kelele kuitengeneza timu yao wao walikuwa wamebaki na Imani za kishirikina ya kuwa mvua ya kwao utafikiri wao ndio mwenyezi mungu!

Sasa basi yanga kashinda mechi zake zote 3 dume kwa 100% , kamgonga Azam 3, kampiga singida 2, kamtwanga Simba 5, huo ndio ukubwa na kipimo Cha timu Bora, hizo mechi 3 mfululizo Simba asingetoboa na BODI ya LIGI ilizipanga makusudi ili yanga adondoshe point lakini Mungu sio selemani Wala kibu Denis mbinu zao zote zimeferi totally!

N;B NIMESHUSHA BEI YA PARACETAMOL NA DAWA TATU KWA AJILI YA WATEJA WANGU NINAOWAPATA LEO KWA WINGI🤣🤣📌📌
 
Hadi Barbra na professional yake alipost eti kisa mvua imepigwa + jumapili basi makolo watashinda

Walichokosea makolo ni kuruhusu mchezo wa kupishana na viungo wa Yanga
Propaganda zao zitaizika iyo timu yao, Msemaji wao anawaaminisha ujinga na wao wanaamini upuuzi, anachokiongea na uhalisia uwanjani ni vitu viwili tofauti, nafikiri Sasa watakuwa na adabu!
 
Simba imekutana na timu isiyofanya makosa mengi mbele

Al Ahly walikua vizuri ila walikua wanapoteza umakini wakifika lango la simba.
Na tuliwatonya Lunyasi hii timu yenu ikikutana na washambuliaji mahiri mtatoboka, wakabisha, kiko wapii??

Hata mmoja wa wachezaji wa Power Dynamo aliwahi kusema Simba ina makosa mengi ni vile tu haikua bahati yao. Bado hawakutaka kurekebika.
 
Back
Top Bottom