Mbeya: Wanafunzi wa Shule za Msingi za Umma waruhusiwa kuvaa Suruali

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,119
WAZAZI na walezi jijini Mbeya, wamepokea kwa mikono miwili, maamuzi yaliyotolewa na serikali, kwamba wanafunzi wa shule za umma, wasichana na wavulana waanze kuvaa suruali, kutokana na mazingira ya Mkoa huo uliopo nyanda za juu Kusini, kuwa na baridi kali.

Hayo yameelezwa na baadhi ya wazazi na walezi jijini humo, baada ya kikao kati ya wazazi, walezi katika shule msingi Mapinduzi, kwamba serikalikupitia vikao maalumu, waidhinishe aina ya sare, kulingana mazingira yao.
Mfumo wa shule za umma zilizo nyingi nchini, wasichana huvalia sketi za bluu na wavulana kaptura na wote shati nyeupe, lakini sasa ruhksa kuvaa suruali kutokana na hali ya hewa.

Martha Mwakilamo, mkazi wa jijini humo anasema: " Ni heri watoto wavae suruali hasa hawa wadogo, Mbeya ni baridi sana, hivyo hapo awali mwanangu alivaa kaptura na ilinibidi nimvalishe soski hata jozi tatu ili apate joto miguuni."

Kamishna wa Elimu nchini, Dk. Lyabwene Mtahabwa akizungumza na Nipashe kwa njia simu, hivi karibuni, amethibitisha hilo na kwamba mikoa, Wilaya kupitia vikao maalumu na kushirikisha jamii, wapange sare za kuvaa wanafunzi kulingana na mazingira.

"Mwongozo ulitoka, sare wanafunzi wa shule za umma inalingana na mazingira, waamue zivaliwe za mfumo gani, ila isitofautiane rangi," kamishna huyo ameiambia Nipashe.

Julai, mwaka jana, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ilisema kwamba hali ya baridi katika mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya baridi ilifikia viwango vya chini vya nyuzi joto 4°C.

NIPASHE
 
Mbona mikoa mingine ni jambo la zamani sana? Tangu naingia Arudha nimekuta wanavaaa suruali,
 
Unavaa kisketi kifupi na kishati cha mkono mfupi utaachaje kumtamani!! Waige mavazi ya shule za kiislamu, na sio za kimagharibi.

Kwanza shule za umma/kanisa/kikristo hazipo care kama za kiislamu, kupigwa mimba ni kugusa/kitu cha kawaida
 
WAZAZI na walezi jijini Mbeya, wamepokea kwa mikono miwili, maamuzi yaliyotolewa na serikali, kwamba wanafunzi wa shule za umma, wasichana na wavulana waanze kuvaa suruali, kutokana na mazingira ya Mkoa huo uliopo nyanda za juu Kusini, kuwa na baridi kali.

Hayo yameelezwa na baadhi ya wazazi na walezi jijini humo, baada ya kikao kati ya wazazi, walezi katika shule msingi Mapinduzi, kwamba serikalikupitia vikao maalumu, waidhinishe aina ya sare, kulingana mazingira yao.
Mfumo wa shule za umma zilizo nyingi nchini, wasichana huvalia sketi za bluu na wavulana kaptura na wote shati nyeupe, lakini sasa ruhksa kuvaa suruali kutokana na hali ya hewa.

Martha Mwakilamo, mkazi wa jijini humo anasema: " Ni heri watoto wavae suruali hasa hawa wadogo, Mbeya ni baridi sana, hivyo hapo awali mwanangu alivaa kaptura na ilinibidi nimvalishe soski hata jozi tatu ili apate joto miguuni."

Kamishna wa Elimu nchini, Dk. Lyabwene Mtahabwa akizungumza na Nipashe kwa njia simu, hivi karibuni, amethibitisha hilo na kwamba mikoa, Wilaya kupitia vikao maalumu na kushirikisha jamii, wapange sare za kuvaa wanafunzi kulingana na mazingira.

"Mwongozo ulitoka, sare wanafunzi wa shule za umma inalingana na mazingira, waamue zivaliwe za mfumo gani, ila isitofautiane rangi," kamishna huyo ameiambia Nipashe.

Julai, mwaka jana, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ilisema kwamba hali ya baridi katika mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya baridi ilifikia viwango vya chini vya nyuzi joto 4°C.

NIPASHE
To yeye hebu tupe taarifa ya hali ya hewa huko kwenu
 
Shetani yupo kazini hizi ni siku za mwisho!
Kumbukumbu la Torati 22:5
Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.
 
Back
Top Bottom