MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi

MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi

Ubaya Ni Kuwa Mimi Naishi Kwa Raha USA, Na Wakati Mwingine Nasafiri Duniani kwa Raha zangu, Lakini Tangu Utoto Najisikia Huzuni ya Kufa Nikiona Mtu akionewa, Maisha ya Mtu Ni Mafupi sana, Kwanini Unamvuruga Mwanadamu Mwingine na Kuyafanya Maisha yake kuwa hasara, Huzuni na Mateso? Is it really necessary? Inaniuma sana, sana Niseme Ukweli, Hata Chama Kingine Kingelikuwepo Madarakani wakawafanyia CCM Unyama huu, Ningeumia Vilevile. Kutesa Mwanadamu Mwingine kwa Makusudi, Ni dhambi Kubwa Kuliko zote Ni tangazo la Dharau, na Chuki juu ya Mungu mwenyewe!
Hongera sana mpendwa kumbe wenzetu waafrica mnaishi kwa raha huko USA!
 
Hongera sana mpendwa kumbe wenzetu waafrica mnaishi kwa raha huko USA!
Sio Wote, Na hakuna Cha Bure Duniani, Lazima Uepuke anasa, Ufanye Kazi wa Bidii, Na Upange Mipango Mizuri ya Kujiboresha, Inachukuwa Muda Kufikia hatua Nzuri Kimaisha, Lakini Yote kwa Yote, Wa Kumjali zaidi Ni Mnyonge, asiye na sauti! Ukiwa Na Uwezo na Nguvu, hilo tu sio Nguvu, Nguvu Ni jinsi Unavyotumia Uwezo wako na Nguvu zako Kutenda haki!
 
Kuna Mamoderator Washenzi sana Jamii Forums, Wanapounganisha Mada wanakuwa na Nia Chafu ya Kuzima Hoja! Lengo Langu Lilikuwa Kuonyesha Unyama Upande wa Polisi ambao kwa Waalimu waliwashukia Lakini wao na wanaowatuma wanadhani wana uhalali wa Kufanya yaleyale na mabaya zaidi. Nimefikia wakati natafakari Kama JF ni Wafagizi wa CCM, Nifikiri Niiachane na Kupoteza Muda wangu hapa.

...kweli mkuu, wanatakiwa waliangalie hili... otherwise slogan ya "where we dare to talk openly" haitakuwa na maana...
 
Ngumi na matusi hutumika pale mtu anapoishiwa hoja au majibu muafaka, usinielewe vibaya, wakati mwingine nguvu ya ziada inatumika kama kinga au kujihami. Lakini kwa yaliyotokea MBEYA DAY SEKONDARI ni utamaduni ulio jengeka katika jamii yetu kwa muda mrefu sana, kwamba watoto au watu walio kuzidi umri wana haki ya kukuadhibu watakavyo pindi unapo tenda kosa. Huu ni utamaduni uliopitwa na wakati na hauna maana yoyote katika jamii ya kitanzania. Kama tuliweza kubadili utamaduni wa kuvaa mgolole na kubeba sime, huu utamaduni unaweza kuondolewa kwenye jamii yetu.

Naelewa watoto au vijana wanaweza kuwa changamoto kwetu, na sisi kama binadamu tuna viwango vyetu vya uvumilivu, lakini kama kuchapa au kupiga watoto sio sehemu ya maisha yako sidhani kama utakimbilia silaha hiyo pindi unapokumbwa na hasira.

Kuna baadhi ya wachangiaji wamedai kuwa tusipo waadhibu watoto kwa njia ya kuchapa au kupiga basi tutakuwa tuapandikiza mbegu ya kiburi na majigambo kwa vijana wetu. Mimi na swali moja, nchi ambazo zimetuzidi kielimu wao wanaweza vipi kufundisha vijana watiifu na waadilifu bila kuwachapa au kuwapiga? Walimu ni watu wasomi, naimani wanajuwa kuwa sio lazima mtoto A kuwa na uwezo au uweleo kama mtoto B. Kama mtoto A anaelewa haraka, mtoto B anaweza kuhitaji kazi ya ziada. Binadamu wote tunaishi kutokana na mvuto, unavutiwa na kitu fulani ndio maana uko radhi kutumia muda wako kukitafuta au kukifuatilia. Haitakuwa rahisi kwa kijana kupenda somo au kupenda kufundishwa kama huyo mwalimu hana mvuto. Mwalimu inabidi awe mbunifu katika kazi yake ilikujenga mvuto kwa vijana anao wafundisha kuliko kulazimisha vijana kuvutiwa na mwalimu.
 
jamaa alitaka kuonesha umwamba mbele ya ma madam..ingekua enzi zangu hao washenziiii wangeondoka siku ioioo mbeya.
 
hawa walimu si wamepita jkt!! wameonekana wakakamavu vijana ambao hawakupita jkt wanaweza kupiga vile mwanafunzi. Unaweza ukawapeleka jkt wakasaidie ulinzi na usalama!!
 
"hao walimu ni washenzi kiwango cha lami"

ki ukweli hapo unaweza kuta mnagawana majengo bila kupenda maana hiyo clip huangalii mara mbili asee
 
Ninayo nyingine wameipost fb waalimu wanambutua mtoto analia mpolee inabidi waalimu tuwatolee macho kodo
 
Dogo ni mkaidi na akishazingua anaenda kutamba kwa wenzake,hii kitu ni lazima ili ajue kwamba akileta uhuni anazinguliwa kihuni.Saafi sana walimu,saaafiiiii kabisaaaaa
Yaani wewe unawadanganya wenzio ili waendelee kuasi sheria, sio?? Hivi wanatafutwa na polisi unajua hatima yao..?? Hivi unajua huko waliko wamekosa amani kiasi gani..?? Hujui kama sasa hivi wanajuta kuijaribu sheria..?? hivi hujui kama sheria haijaribiwi..?? TAFAKARI CHUKUA HATUA.
 
14595807_151696881955977_3219049678899893624_n.jpg



NAWAOMBA WOTE WANAO TETEA UPANDE WA MWALIMU WAJE WAJIBU BAADA YA HII PICHA TENA WAKIWA NA FACTS SIO KELELE TU


[HASHTAG]#NOTE[/HASHTAG] WALIMU.....UKIMFANYIA HIVI MWANANGU NAKUUA
 
Tukiliangalia tukio hili tangu awali muhusika mkuu anatajwa MWALIMU na kunawakati tunaambiwa ni wanachuo wote yaani mchukua video,pamoja na wale wanaopiga.....kwa vyovyote vile tukio hilo siyo zuri na nilakuhudhunisha ila naligawanya katika sehemu tofauti

SEHEMU YA KWANZA
Kwa vyovyote vile ili uwe mwalimu kuna sifa lazima uwenazo kama vile upate mafunzo(nadharia na vitendo)ya ualimu. Ufanye mtihani(nadharia na vitendo)ya ualimu kwa kipindi hichi tunakuita MWANACHUO.Majibu ya mafunzo hayo yakitoka utakuwa labda umefeli au umefaulu.....Na mara baada ya majibu kutoka ukifaulu(nadharia na vitendo)

Jina la kwanza kuitwa ni MWALIMU TARAJALI kwa kuwa ni mwalimu anayesubiri kupangiwa kituo cha kazi.Ukishaanza kazi tu tunakuita MWALIMU KAMILI kwakuwa upo kazini tena mwaka nakadri muda unavyoenda mbele tunakuita MWALIMU MWANDAMIZI kwa kuwa unamuunamudae......

Swali hao walio mpiga mwanafunzi kwa hatuo hizo hapo unawaitaje???...Sisemi kwa kuwa mimi mwalimu nasema ili tusiuchafue ualimu

SEHEMU YA PILI
Kunamatukio matatu lazima tuyaangalie vizuri:~
(1)Inavyooneka huyo anayesemekana mwalimu akimpiga mwanafunzi anaonekana kama alikuwa na JAZBA ya muda mrefu iliyosababishwa na kitu fulani...NDIYO MAANA NASEMA HAO SIYO WAALIMU BADO

(2)kwamujibu wa majibu ya mwanafunzi aliyepigwa nikuwa alipo ulizwa kwanini hajaandika alijibu "Nilikuwa naumwa" kwa mujibu wa maelezo mwalimu akamkunja mtoto naye akamkunja mwalimu.....swali kunauhusiano gani jibu na kukunjwa mtoto???? Kunatukio gani kabla ya kukunjwa mtoto????kwanini mtoto alipata ujasiri wa kumrudishia mwalimu kumkunja?????

MAJIBU YA MADHANIO:
Inawezekana kunajibu lililotoka kwa mtoto kwenda kwa huyo anayeitwa mwalimu likamfanya ajihisi kadharauliwa hivyo alipandwa najazba kushindwa kujizuia hatimae kumkunja KWAKUWA SI MWALIMU.....

Nakwakuwa mwanafunzi teyari alimdharau kwakuona kuwa si mwalimu kamili hivyo alihisi kama vile yupo na mwenzake wakawaida na hatimae kurudishia

Jibu la mtoto siyo rahisi mtu kumkunja hivyo inawezekana huyo anayeitwa mwalimu alikuwa na jazba kabla au kunakitu kilipelekea hivyo.UFANYIKE UCHUNGUZI
 
Katika tania ya uandishi wa habari kuna mambo ambayo huwezi kutengeneza habari KWA haraka kuliko mengine.mambo hayo yanaweza kuwa umaarufu, cheo, umuhimu wa jambo, mihemko ya jamii(prominent and proximity)

Katika falsafa tunasema....."Mbwa kumuuma mwanadamu haiwezi kutengeneza habari ila mwanadamu kumuuma mbwa ndo hutengeneza habari".

Akipigwa mwalimu wazazi hufunga vibwebwe na kushangilia

Akipigwa mwanafunzi wazazi hao hao huandamana kuwalaani walimu na kutoa hukumu midomoni.

Jana polisi walikuja chuoni mwalimu nyerere kuchukua faili la mwanachuo huyo ili hatua za upelelezi ziweze kufanyika na hatua zaidi kuchukuliwa. Kwahiyo tuviachie vyombo vya dola vifanye kazi yake na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma dhidi yake na bado ni watuhumiwa tu na sio wakosaji.

Hawawezi kushitakiwa kwa kula njama kwani hawakuvamia shule bali ni matumizi mabaya ya adhabu zinazotolewa kwa mujibu wa sheria.

Jana hiyo hiyo walifukuzwa chuo kwa tamko la waziri wa elimu japo kisheria ni mapema mno kuwaadhibu kabla ya mahakama kutoa uamuzi dhidi yao kama wana hatia au la.

Mwenye mamlaka ya kumfukuza mwanachuo ni bodi ya chuo husika baada ya mwanafunzi kutiwa hatiani na mahakama na kuhukumiwa kifungo jela kinachozidi miezi 6 kwa kosa lolote.

Walimu tarajali hao hawajafikishwa mahakamani bado lakini jamii na waziri wameshawahukumu nje ya mahakama na sheria kanuni na taratibu za elimu ya juu.

Kuna kesi kama hii iliwakumba wanafunzi 75 wa chuo kikuu cha DSM wakafukuzwa chuo na kufikishwa mahakama ya kisutu DSM mahakama ikawaona hawana kesi ya kujibu hivyo hawana cha kujitetea na kuwaachia huru. Baada ya hapo wakafungua kesi mahakama kuu kupinga kufukuzwa chuo na walishinda na kurudishwa chuoni.

Jambo jingine ni pale ambapo tunakamata vibaka mtaani na kuwaweka ndani na kutokomea bila kwenda kutoa ushahidi dhidi yao na baada ya saa 24-48 wanaachiwa na jamii kubaki kuwalaumu polisi kwamba wamekula rushwa na kuwaachia watuhumiwa Wakati hatujaenda kuthibitisha tuhuma dhidi yao.

Albert Mnali aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Bukoba aliwachapa fimbo walimu wa shule ya msingi kanazi na wazazi na jamii za kijinga jinga hadi leo wanakenua meno kusifia kitendo kile.

Singida mwalimu kachomwa kisu na wanafunzi na kufa halafu hio haikufanywa kuwa habari.

Juzi kanda ya ziwa mwalimu Mkuu kachapwa fimbo na sungusungu kwa sababu eti hakuwapigia makofi na bado serikali na wazazi wakaona ni sawa.

Juzi tandika Temeke DSM mwalimu kapigwa ngwala na mwanafunzi na bado ikanyamaziwa.

Kile Isevya katavi walimu wameng'olewa meno 3 na wanafunzi lakini bado haikutengeneza habari.

Wanafunzi wamefikia hatua ya kuwabaka walimu wa kike na kuwadhalilisha kama ilivyotokea kibiti sekondari lakini haikutengeneza mshindo wa habari wala hatua za kisheria kuchukuliwa.

Pamoja na mifano msingi ambayo sijaitoa hapa bado vibaka, wabakaji na majambazi, wakabaji na wauwaji hawakuzaliwa wakiwa hivyo bali ni matokeo ya malezi mabaya.

Jamii inawatetea watukutu lakini wakija kuwa wabaya wanasema watoto wa siku hizi hawana adabu, je wazazi na walezi walikosea wapi hadi kufikia hali hiyo?

Je kuna watoto wanazaliwa mtaani ama huzaliwa nyumbani na kwenda kuishi mtani?

Hata Mimi niliwahi kurushiwa jiwe na wanafunzi nikiwa mstarini. Mwalimu mwingine akamwagiwa mchanga na wanafunzi akiwa darasani.

Mzazi mmoja aliwahi kuja shuleni akawapiga wanafunzi ngumi wakiwa darasani tukamfungulia kesi lakini kesi ikafutwa baada ya Mwenyekiti wa mtaa na jamii kumtetea.

Kwahiyo tusilaumu kwanini vijana wameharibika Wakati hatuangalii tulipokosea bali tunasngalia matokeo yake.
 
KWENU NYINYI AMBAO SIO WALIMU,NA KWA WALIMU WENZANGU.,nasadifu kilichotokea mkoani MBEYA.

Kitaaluma mimi ni mwalimu na nimewahi pia huko nyuma kufundisha shule kadhaa za serikali na za watu binafsi.Nimeamua kuandika kaandiko haka nataka kushare na nyinyi baadhi ya changamoto za kinidhamu nilizowahi kukutana nazo wakati huo nikiwa nafundisha shule mbalimbali na nyingine kuhadithiwa na walimu wenzangu .

Lengo la kaandiko haka si kutetea kilichofanywa na walimu wa mazoezi huko mkoani Mbeya,lakini ni kuonesha kuna mambo mengine yanapaswa kufanyika zaidi ya kuwafukuza walimu kwa hatua wanazozichukua dhidi ya utovu wa nidhamu kwa baadhi ya wanafunzi.

Mwaka 2009 nikiwa nafanya elimu kwa vitendo(Teaching practise) mkoani Morogoro wilaya ya Kilombero katika shule flani ya serikali,nikiwa mwalimu wa zamu nilipewa agizo na mkuu wangu wa shule kuhakikisha wanafunzi wote wanaovaa ma-sweta yasiyoruhusiwa na shule nawaadhibu.

Katika kutimiza agizo hilo nikakutana na mwanafunzi mmoja wa kidato cha nne amevaa sweta lisiloruhusiwa,ni "giant" hasa kama unavyojua wanafunzi wa zamani,mrefu na alikua na dalili zote kua ametoka kuvuta au kunywa pombe asubuhi ile.

Nilipomsimamisha akakataa kusimama ,nilipoajaribu kutumia mbinu nyingine kumhoji niliishia kutukaniwa mama yangu na mikwara mingine.Kwakua ilikua ni wiki mbili tu tangu nilipoti shule ile sikuripoti kwa mwalimu yeyote tukio lile lakini baadae nikaja kugundua ni mwanafunzi mwenye nidhamu mbovu kuliko wote kwenye shule ile,walimu wote wanalalamika kuhusu nidhamu ya mwanafunzi yule.

Nilimaliza field na nilikua na hamu ya kujua matokeo yake ya mtihani wa kidato cha nne ALIPATA "DIVISHEN" ZERO( Div 0)

Mwaka 2012 nikiwa nimeajiriwa shule flani ya serikali mkoani Iringa wilaya ya Mufindi nikakutana na tukio lingine,mwanafunzi mmoja alipuliza mpira wa kondom ukajaa kiasi cha mpira unaochezewa kwenye soka na kurusha darasani muda wa vipindi.

Tukio lile lilisababisha kelele nyingi sana darasani kiasi cha kuharibu kabisa utulivu wa shule nzima na kuhathiri vipindi vilivyokua vinaendelea kwenye madarasa mengine.

Nakumbuka mimi na mwalimu mmoja( jina limeifadhiwa)ambao tuliajiriwa pamoja tuliamua "kushumghulikia" mwanafunzi aliyefanya tukio lile ambaye kwa wakati huo alikua ananuka harufu ya pombe ya asili aina ya ulanzi..Lakini kabla ya kuamua kufanya hivyo tulijaribu kuwashirikisha walimu wengine kuhusu nidhamu ya mwanafunzi husika.

Tukaambiwa na walimu tuliowakuta kwamba kwanza mwanafunzi yule ni mchawi,aliwahi hata kukamatwa juu ya paa la nyumba akiwa anaroga,pili ana nguvu za ajabu za asili ,hata mkimkamata watu watano anawabwaga kama John Cena wa W.W.F,kubwa zaidi tukaambiwa alishawahi kumchoma kisu ubavuni mwanafunzi mwenzie huko nyuma.Huyu nae ALIPATA "DIVISHENI" SIFURI(Div O) kwenye matokeo yake ya mwisho.

Mwanzoni mwa mwaka huu Iringa mjini mwanafunzi wa kike wa kidato cha Pili wa shule mojawapo iliyopo manispaa ya Iringa alikutwa akifanya mapenzi mchana kweupe kabisa kwenye bustani za manispaa(POSTA) .Sina uhakika kama mwanafunzi yule amefukuzwa shule.Kama hajafukuzwa ninaamini matokeo yake mwaka 2018 hayatofautiana na hao wawili nilioanza nao.

MAMBO MUHIMU NINAYOTAKA YAELEWEKE.

,Shule nyingi za serikali zinaendeshwa mno kisiasa.Haiwezekani mtoto anayefikia hatua ya kumchoma kisu,au kurusha kondom darasani akaachwa kuendelea kusoma bila kufukuzwa au kupewa uhamisho mpaka anamaliza kidato cha nne

Mimi binafsi nikiwa mwanafunzi wa kidato cha pili nilikufukuzwa shule(seminari) kwa makosa mawili moja kuua paka wa shule na la pili kushindwa kuhudhuria vipindi darasani kwa siku tano mfululizo.BADO UNASHNGAA KWA NINI SEMINARI ZINAONGOZA KWA UFAULU NCHINI?

Kwa upande wa shule zetu za serikali siasa zimekua nyingi mno hasa shule za kata .Wanasiasa hawapo tayari kuona shule "zao' zina idadi ndogo za wanafunzi ili wakati wa kampeni wataje idadi za wanafunzi kwenye majukwaa zenye kuvutia wapiga kura (basing on Quantity rather than Quality).

Mimi binafsi kwenye tukio la pili hapo juu mkuu wangu wa shule alinieleza namna ambavyo ni vigumu kumfukuza mwananfunzi shuleni japo sheria za shule zimeainisha makosa yanaweza kumfukuzisha shule mwananfunzi na makosa hayo hayo mwananfunzi akayafanya na asifukzwe shule

Hawa walimu nao ni binadamu pamoja na taaluma zao,wana viwango na mipaka ya uvumilivu kama binadamu wengine.Wkifika kwenye mipaka hiyo(point of no return) .Katika ubinadamu wao wanakasirika,wanaumia,wanachukia,wanafurahi.Hawana tofauti yoyote na binadamu wengine

Natambua lipo neno "kujidhibti" lakini Kiisaikolojia binadamu yoyote akifika hapo ni vigumu kuamua nje ya hisia zake za wakati huo.NAMNA PEKEE YA KUWAZIA WALIMU WASIFIKE HAPO NI KUONDOA/KUWAFUKUZA MASHULENI WATOTO WALIOSHINDIKANA.

Kwa walimu wenzangu ni muda wa kujua sasa ili kutengeneza uhalali wa kuonekana adhabu tunazotoa licha ya kupitiliza lengo lake hasa ni kuboresha nidhamu za wanafunzi na tuanze sisi kua na nidhamu hizo kwa kuchagua adhabu za kuwapa.

Nje ya mavazi,lugha zetu,mahusiano yetu na wanafunzi hata ADHABU TUNAZOTOA PIA zinaakisi viwango vyetu vya nidhamu dhidi ya taaluma zetu.Katika changamoto za mishahara tulizonazo,mazingira magumu ya kazi tuanze kutambua pia tupo kwenye kipindi kibaya cha ukuaji na matumizi makubwa ya teknolojia TUNAANGALIWA MNO kwakua tunaaminika.

Kwa kesi ya Mbeya kinacholalamikiwa na kupigiwa kelele sio KUPIGWA KWA MWANAFUNZI ,NI NAMNA MWANAFUNZI HUYO ALIVYOPIGWA.Kwa namna ambavyo amepigwa inathibitisha hata walimu wenyewe hatuna au nidhamu.Natamani kufananisha na upigaji wa SCORPION wa Buguruni.

NGUZO NOEL .R.
 
Lakin hata wewe pia unaweza kuwa mbwa kwa maana unacho kisema pia si cha kibinadamu kina dalili za uumbwa ,huna tofauti na hao walimu maana wao walishindwa kuzuia hasira zao na wewe umeshindwa kuzuia kinywa chako maana yake hata wewe ungekuwa pale na wale walimu ni dhahiri ungeshiriki kupiga maana umeshindwa kujizuia kwa kutambua kuwa wao ni binadamu walio fanya kosa na sio mbwa.
Ni mjinga na mwenye akili za kimmbwa ndo anaeweza kuona binadamu mwingine akinyanyaswa akaamua kukaa kimya ili baadae waende mahakamani. Huna tofauti na nyumbu. Mwenzao analiwa yenyewe yamebung'aa
 
Si bure, huyo mwalimu mpigaji ana kitu kinamuudhi kuhusu huyo kijana. Wamegombea mwanamke? Imeniumiza sana video hii...
yaani hata mimi nilihisi hivyo aisee homework tu ndo kipigo hicho halafu wanaume wote hao bila aibu duh...walitakiwa watumie hekima tu jamani wao ni watu wazima yaani nashangaa hata mwalimu mkuu naye hajafuatilia ni kwamba hakujua au vipi? na huyo mtoto wiki nzima alienda hospitali au? maana kwa kipigo hicho na kuangukia kichwa anaweza akawa na tatizo serious eti dah nimeumia sana yani angekua ndugu yangu huyo dogo cjui tu ningekuwa wapi saa hizi
 
Ni mjinga na mwenye akili za kimmbwa ndo anaeweza kuona binadamu mwingine akinyanyaswa akaamua kukaa kimya ili baadae waende mahakamani. Huna tofauti na nyumbu. Mwenzao analiwa yenyewe yamebung'aa
Kila kitu kina sababu ni mjinga pekee anaye thani jambo hutokea bila sababu mwalimu ni tittle but she/he is a human being , ndio maana hata wewe umeshundwa kuzuia jazba zako ukaamua kuita wenzio mbwaa na hii ni tafsiri kuwa laiti wewe ndiye ungekuwa mwalimu wa mbeya day basi unge mchinja kabisa kijana yule maana hata wewe pia huna staha na una mihemko zaid ya wale walio fanya tukio mbeya
 
Back
Top Bottom