Mbeya long time kitambo

Mbeya long time kitambo

Kumbuka nonde juu ilikuwa si mchezo. Mmenikumbusha mbata primary. Mwangomile alifundisha pia. Alikua mkaaliiiii. Balaaa.
Mwangomile stiki zake si mchezo. Anafundisha Mbata fimbo anapiga Mbata nzima kisha anahamia Majengo Juu kisha Majengo Chini then Itiji Na Maendeleo anaenda kumalizia kuchapa wachelewaji
 
HII NDIO ILIKUWA MBEYA BWANA

1. Enzi hizo alikuwepo mtu anaitwa Jombi, kudhihirisha ubabe kwa wenzako lazima uwaambie Mimi ni "Jombi"

2. Kulikuwa na basi zinaitwa Kiswele..engine nyuma, Dar - Mby faster, Mafegi hii ilikuwa na vijihoni vya Ukweli,usisahau Mv Saratoga, Tunyande bus service, Zainabus

3. Kulikuwa na wavuta petroli, hawa jamaa walikuwa km 5 hivi, wachafu wanatembea pamoja mitaa ya BP uhindini wakiwa na makopo na vitambaa vilivyoloa petrol wanavuta.

4. kiwanja ngoma, hapa Soka lilipigwa bwana, timu yangu ya Mtaa Snow White chini ya Key, kina Baba Jeni. Basket ball ilikuwa pale Centre, tulikuwa na chama letu Mbeya Flames.

5. Town pale palikuwa na vichaa hatari kuna "Tiotio" huyu alikuwa anachapa ngeli balaa, Merry Kichaa alikuwa na alergy na watu weupe, akikuotea atakukimbizaa na stick utakula. Pale Mbeya Recto ndio ilikuwa km Makao makuu ya vichaa walikuwa kibao

5.Pale Bomani palikuwa na Mzee mmoja mfupi nakumbuka jina moja la Mwakifuna,nilifanya jitihada ili kumuona tu maana kutokumjua na kumuona ilikuwa ni weakness kubwa.

6. Kipindi hicho Disco lilikuwa Mount Livingstone na Rift valley, Soggy doggy enzi hizo akiitwa Wasape na Sugu- 2 Proud, hipop ilinoga bwana.

7. Mtakumbuka Mbeya tulikuwa na ukumbi Wa Sinema pale opposite na Ofisi za Posta Town, Muvy ya Hatya ilifunika sana enzi zile.

8. Miaka ile bwana mvua ilikuwa inapiga km gharika,sometimes ilikuwa inamwagwa barafu km ulaya,mlima Loleza ulikuwa ukifunikwa theluji kwa siku kadhaa. Radi sasa, hatariii mpaka nyumba ina Shake.

9. Siku ya Jumamosi ilikuwa ya kuosha mbwa,mbwa wote walikuwa wanapelekwa josho pale Mifugo,nyuma ya Kanisa la Roman,mkishamaliza kuogesha mnaanza kugombanisha Mbwa,mbwa Wa kizungu walikuwa wanaogopwa kupambanishwa na Wa kienyeji ikiaminika wananguvu balaa.

10. Uzunguni enzi hizo kulikuwa na matunda ya aina mbalimbali,watoto walikuwa wanatoka maeneo kadhaa ikiwemo Isanga kuja kuchuma maparachichi,mang'ang'a,mafyulizi,mapohora,mapera nk.

11. Mwanjelwa.enzi hizo iliitwa Doksi au Njelii, mitumba viwango,raba Kali,msela ukitupia vya doksi umemaliza.

12.Enzi zile ukisoma Sisimba na Azimio unafunika,Shule ya International ilikuwa Umoja primary school, waliosoma hapo hata kupishana nao unaogopa

13. Kuruka ukuta Wa Uwanja Wa Sokoine au kuingia uwanjani kupitia Bomba la maji ya mvua wakati Wa mechi ilikuwa ujanja balaa.

14. Ukisikia Shule za Sekondari Iyunga, Sangu, Loleza, Mbeya Day zilikuwa na kila aina ya sifa.Sangu kulikuwa na vichwa lazima uvitambue wababe km Simply na Kambosonic waliogopwa.

15. UMISETA sasa, dah, achaa..hapa Lutengano hapa Mwakaleli, boli lilitandazwa,kikinuka uwanjani ilikuwa km vita,makwanja na fimbo hujui vilipotokea,ukizubaa utakula mkono balaa

16. Kuna mdada walikuwa hatari alikuwa anatembeza kichapo kwa wanaume balaa walikuwa anatokea ilemi alifahamika kwa jina la Jeni.

17 Kuna jamaa alikuwa mtata sana mtaa Wa mafiati, makunguru, juakali alifahamika kwa jina la Daudi Masoke. Walikuwa balaa alikuwa anaiba Nyumba nzima hadi kitanda ulicholalia.

18. Ukisia mtaani Dunda, Kwendi, Shaban wanatembea mtaani wanaume wote kimya walikuwa hawaoni shida kukupiga dispiss ya tumbo. Wakitaka kupora walikuwa hawapati shida wanakuzunguka baada ya muda unaporwa ukipiga kelele hakuna Wa kukusaidia maana hadi wazazi wao walikuwa wanawaogopa.

19. Ukisikia obamka yaani ilikuwa full kwa watoto Wa mafiati, sinde, ilemi, isanga, ilolo ni sehemu ya kuchomea viazi mtoto walikuwa radhi asile nyumbani aende njelii kuokota viazi ili akachome obamka.

20. Uswahili tabu fresh food iligeuzwa jina na kuitwa Chakula barafu kiss vyakula vinahifadhiwa kwenye friiza. Expire date ya chakula hasa maziwa ilikuwa furaha kwa watoto Wa uswahili. Zaidi panaitwa city pub/century plaza.

21. Doxi waliwauzia wanyia blauzi na kuwaambia mashati. Ndio kisasi kikarudishwa unyiani na kuwaambia wamachinga Wa nguo Tumugoge tumuleshe...(tumuue tumuache).

NAIKUMBUKA MBEYA YA ZAMANI..
Buji, ile ibada ya kula nyama ulienda? Kulikuwa na wanyama aina ngapi?
 
Bila kusahau Black Belt Mwanjelwa to Soko matola
 
Umenikumbusha mwalimu mkuu wangu wa Azimio shule ya msingi alikuwa anaitwa mwangomile, aisee alikuwa anachapa bakora yaani ndugai haoni ndani kabisa
Uyo mwl mwangomile,,nahisi amewahi kufundisha Chunya..Alikua mwl wa somo la Hisabati..Anapiga bakora ni balaaaaa
 
Mi pia kanichapa mbata primary. Du siku hizo...

Mwaka 1986 pale Mbata kulikuwa na Mwl Peter naye alikua akichapa balaaa. Sema alikua na umbo na tako zuri. Sujui yuko wapi siku hizi...
Mbata mnamkumbuka Mwl mhina!? Alikua mwembamba na mdogo wa umbo lakini alikua mkali usipime. Ole wako awe mwalimu wa zamu halafu uchelewe 'namba'! Sijui kako wapi?!
 
Sie watoto wa Nonde tuliokuwa karibu na kanisa la Lutheran la mawe minuso safari zilikuwa zinaanzia pale tukiona tu! Harusi mnaunga inakoelekea kufanyikia baada ya ndoa
haaa mkuu kwa mzee gani mitaaa ile
 
Yalikuwepo kama kina bora imani, mwailubi bus, baby kapritan na father kapritan, sasa kazi yote haya yalikua mbalizi stand kuu

Post sent using JamiiForums mobile app
ha ha enzi hizo duub
 
Uyo mwl mwangomile,,nahisi amewahi kufundisha Chunya..Alikua mwl wa somo la Hisabati..Anapiga bakora ni balaaaaa

Halafu Mbeya day tukakutana na Mwl Mwandeko. It was hell. Tumesota sana guys...
 
Back
Top Bottom