Mbeya long time kitambo

Siku hizi watu wameacha vurugu shuleni na vyuoni. Tulikuwa na ndugu yetu pale, Tulikuwa tunamtembelea jpili tupige na mpunga. Walikuwa wanapikiwa fresh sana.
Hahah mwenyewe mpunga nimeula sana..maana jamaa wanachukua sado zima..kuja kula na wana wa mtaa

Sent from my GT-I9500 using JamiiForums mobile app
 
Umenikumbusha enzi za ngenge na wali moto mchuzi moto pale Jua kali kwenye 1997.

Sent from my HUAWEI Y300-0100 using JamiiForums mobile app
Sie watoto wa Nonde tuliokuwa karibu na kanisa la Lutheran la mawe minuso safari zilikuwa zinaanzia pale tukiona tu! Harusi mnaunga inakoelekea kufanyikia baada ya ndoa
 
Sie watoto wa Nonde tuliokuwa karibu na kanisa la Lutheran la mawe minuso safari zilikuwa zinaanzia pale tukiona tu! Harusi mnaunga inakoelekea kufanyikia baada ya ndoa
Utakuwa megonga sana minyofoo chinji.
 
MOHAMED%2BKASSANDA%2BRAPHAEL%2BMAPUNDA%2BNA%2BKANZA%2BMRISHO%2BTUKUYU%2BSTARS%2B1987%2BSOKOINE%2BMBEYA.jpg


Wachezaji wa Tukuyu Stars ya Mbeya kutoka kushoto, Mohamed Kassanda, Raphael Mapunda na Kanza Mrisho wakiwa Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya mwaka 1987 kabla ya moja ya mechi zao za Ligi Daraja la Kwanza (sasa Ligi Kuu) Tanzania Bara. Tukuyu ilikuwa bingwa mwaka 1986 na baada ya msimu nyota wake wakachukuliwa na Yanga na Simba nayo ikashuka daraja mwaka 1987
 
Duh, enzi hizo kila basi ina carrier. Basi za mwisho mwisho za dizaini hiyo walikuwa nalo rufaa na MTC. Basi za mstatili.

Land alienation

Forced Labour

Low wages

Poor technology

Poor infrastructure

Lack of education

Unemployment

Taxation

Yan hizi point zimewafikisha watu chuo kikuu, huwa hazikataagi swali hata kama unaelezea issue ya Kibiti
 
siku moja tulienda kucheza boli Rungwe sec basi kulikua na mawe ya kufa mtu dah ile match inaisha aisee walituvunjia vioo bus let, ila kweli Rungwe mlikua mnavuta sana bangi aisee.

Kama ile ajali ya kuanguka miti inayozunguka uanja wa Sokoine aisee nilinusurika nilikosa siti sikupanda, kuna mshkaji ni mlemavu hadi leo................

Mbeya bwana dah nina miaka mingi sijaish Mby ya wasafwa, wanyiha, wanyakyusa, wandali, mwagona mwe
Ile ajal ya miti hata mm nikuwepo

Sent from my Infinix NOTE 3 Pro using JamiiForums mobile app
 
naskia ile barabara ya kutoka Rift valley kwenda chunya ina lami, na lile soko la Isanga limefutwa,hv uwanja ngoma upo bado?
Saiz lami mpaka chunya mjin siku hz usafil ni wa costa tu

Sent from my Infinix NOTE 3 Pro using JamiiForums mobile app
 
HII NDIO ILIKUWA MBEYA BWANA

1. Enzi hizo alikuwepo mtu anaitwa Jombi, kudhihirisha ubabe kwa wenzako lazima uwaambie Mimi ni "Jombi"

2. Kulikuwa na basi zinaitwa Kiswele..engine nyuma, Dar - Mby faster, Mafegi hii ilikuwa na vijihoni vya Ukweli,usisahau Mv Saratoga, Tunyande bus service, Zainabus

3. Kulikuwa na wavuta petroli, hawa jamaa walikuwa km 5 hivi, wachafu wanatembea pamoja mitaa ya BP uhindini wakiwa na makopo na vitambaa vilivyoloa petrol wanavuta.

4. kiwanja ngoma, hapa Soka lilipigwa bwana, timu yangu ya Mtaa Snow White chini ya Key, kina Baba Jeni. Basket ball ilikuwa pale Centre, tulikuwa na chama letu Mbeya Flames.

5. Town pale palikuwa na vichaa hatari kuna "Tiotio" huyu alikuwa anachapa ngeli balaa, Merry Kichaa alikuwa na alergy na watu weupe, akikuotea atakukimbizaa na stick utakula. Pale Mbeya Recto ndio ilikuwa km Makao makuu ya vichaa walikuwa kibao

5.Pale Bomani palikuwa na Mzee mmoja mfupi nakumbuka jina moja la Mwakifuna,nilifanya jitihada ili kumuona tu maana kutokumjua na kumuona ilikuwa ni weakness kubwa.

6. Kipindi hicho Disco lilikuwa Mount Livingstone na Rift valley, Soggy doggy enzi hizo akiitwa Wasape na Sugu- 2 Proud, hipop ilinoga bwana.

7. Mtakumbuka Mbeya tulikuwa na ukumbi Wa Sinema pale opposite na Ofisi za Posta Town, Muvy ya Hatya ilifunika sana enzi zile.

8. Miaka ile bwana mvua ilikuwa inapiga km gharika,sometimes ilikuwa inamwagwa barafu km ulaya,mlima Loleza ulikuwa ukifunikwa theluji kwa siku kadhaa. Radi sasa, hatariii mpaka nyumba ina Shake.

9. Siku ya Jumamosi ilikuwa ya kuosha mbwa,mbwa wote walikuwa wanapelekwa josho pale Mifugo,nyuma ya Kanisa la Roman,mkishamaliza kuogesha mnaanza kugombanisha Mbwa,mbwa Wa kizungu walikuwa wanaogopwa kupambanishwa na Wa kienyeji ikiaminika wananguvu balaa.

10. Uzunguni enzi hizo kulikuwa na matunda ya aina mbalimbali,watoto walikuwa wanatoka maeneo kadhaa ikiwemo Isanga kuja kuchuma maparachichi,mang'ang'a,mafyulizi,mapohora,mapera nk.

11. Mwanjelwa.enzi hizo iliitwa Doksi au Njelii, mitumba viwango,raba Kali,msela ukitupia vya doksi umemaliza.

12.Enzi zile ukisoma Sisimba na Azimio unafunika,Shule ya International ilikuwa Umoja primary school, waliosoma hapo hata kupishana nao unaogopa

13. Kuruka ukuta Wa Uwanja Wa Sokoine au kuingia uwanjani kupitia Bomba la maji ya mvua wakati Wa mechi ilikuwa ujanja balaa.

14. Ukisikia Shule za Sekondari Iyunga, Sangu, Loleza, Mbeya Day zilikuwa na kila aina ya sifa.Sangu kulikuwa na vichwa lazima uvitambue wababe km Simply na Kambosonic waliogopwa.

15. UMISETA sasa, dah, achaa..hapa Lutengano hapa Mwakaleli, boli lilitandazwa,kikinuka uwanjani ilikuwa km vita,makwanja na fimbo hujui vilipotokea,ukizubaa utakula mkono balaa

16. Kuna mdada walikuwa hatari alikuwa anatembeza kichapo kwa wanaume balaa walikuwa anatokea ilemi alifahamika kwa jina la Jeni.

17 Kuna jamaa alikuwa mtata sana mtaa Wa mafiati, makunguru, juakali alifahamika kwa jina la Daudi Masoke. Walikuwa balaa alikuwa anaiba Nyumba nzima hadi kitanda ulicholalia.

18. Ukisia mtaani Dunda, Kwendi, Shaban wanatembea mtaani wanaume wote kimya walikuwa hawaoni shida kukupiga dispiss ya tumbo. Wakitaka kupora walikuwa hawapati shida wanakuzunguka baada ya muda unaporwa ukipiga kelele hakuna Wa kukusaidia maana hadi wazazi wao walikuwa wanawaogopa.

19. Ukisikia obamka yaani ilikuwa full kwa watoto Wa mafiati, sinde, ilemi, isanga, ilolo ni sehemu ya kuchomea viazi mtoto walikuwa radhi asile nyumbani aende njelii kuokota viazi ili akachome obamka.

20. Uswahili tabu fresh food iligeuzwa jina na kuitwa Chakula barafu kiss vyakula vinahifadhiwa kwenye friiza. Expire date ya chakula hasa maziwa ilikuwa furaha kwa watoto Wa uswahili. Zaidi panaitwa city pub/century plaza.

21. Doxi waliwauzia wanyia blauzi na kuwaambia mashati. Ndio kisasi kikarudishwa unyiani na kuwaambia wamachinga Wa nguo Tumugoge tumuleshe...(tumuue tumuache).

NAIKUMBUKA MBEYA YA ZAMANI..
*umemsahau shetani na Yesu*

Sent from my Infinix NOTE 3 Pro using JamiiForums mobile app
 
ha ha haaa Kifwamba Rangers .....ilikuwa timu ya tajiri mmoja mnene enzi hizo.....mara moja moja alikuwa akipewa namba tisa aingie kupiga soka .....ilikuwa vituko....nasikia alikufa huyo mwenye kifwamba
Kwenye timu yake ukiwa namba saba hupat namba maana hyo namba ilikuwa yake akichoka alikuwa anaingia shemeji yake alikuwa anaitwa mawazo.ukitokea penart yupo nje bas anaomba kuingia ili akapige yeye uwanja wa magereza ilikuwa vituko

Sent from my Infinix NOTE 3 Pro using JamiiForums mobile app
 
55 Reactions
Reply
Back
Top Bottom