Mbeya kuna nini leo? JWTZ watanda mji mzima

Mbeya kuna nini leo? JWTZ watanda mji mzima

Kitu ambacho sinahakika nacho ni iwapo zoezi hili ni endelevu na itahusisha mikoa yote ama ni MBEYA tu. Si unajua mambo mengi yanaanzia Mbeya.
 
Mkuuwote tunajua polisi hata vituoni tu hawatoshi.kuna vituo unakuta polisi mmoja tu kituo kizima wengine wote ni polisi jamii.na kama nilivyosema awal wakati wa uchanguz kuna pilipilika nyingi polisi na kipindi polisi wanakuwa hawatoshi kabisa

Acha kuongea tu bila hoja yenye mashiko. Kwanza mpaka askari waende kuwasumbua wananchi ni lazima kuwe na evidence ya ugaidi kwa kutumia intelligence. Huwezi ukakutupuka tu na kwenda barabarani kukagua watu. Pia hiyo siyo kazi ya jwtz. Ninakumbusha tu kuwa mwananchi wa sasa sio kama yule wa miaka ya 60. Ameamka na anijua haki yake. Hivyo kuweka majeshi barabarani haitabadilisha chochote zaidi ya kuongeza vuguvugu La majeuzi. Hata mtoto ukimtandika sana anakuwa sugu (simaanishi mbunge wetu).
 
Mida ya saa saba nilisikia milio na vishindo vya mabom kiasi kwamba nyumba imevibrate. Kama mara tatu vishindo vikubwa kwakweli.
 
Mbongo mbona hamna ugaidi, au tumeumiss tunauita

wiseboy

Kama utabakia kuwa PRIMITIVE katika KARNE HII wakati una bahati ya kuona TV; Internet etc...

Unakashifu MBONGO; Haujui nchi nyingi tu duniani huwa wanafanya DRILLS za SECURITY in PUBLIC

** SOMA Kidogo MBONGO... Ukiwa hivyo Wakenya; Waganda; Wanyarwanda na Warundi watabeba kazi zetu nchini...
 
wiseboy

Kama utabakia kuwa PRIMITIVE katika KARNE HII wakati una bahati ya kuona TV; Internet etc...

Unakashifu MBONGO; Haujui nchi nyingi tu duniani huwa wanafanya DRILLS za SECURITY in PUBLIC

** SOMA Kidogo MBONGO... Ukiwa hivyo Wakenya; Waganda; Wanyarwanda na Warundi watabeba kazi zetu nchini...


Hivi na enzi za JK Nyerere haya mambo mitaani yalifanyika au tunaenda nawakati yaan dunia ya utatandawazi?


Mazowea hujenga tabia, tusiwafanye raia kuiona bunduki kwenye kwapa na mabega ya wanajeshi kuwa jambo lakawaida.


-Tutajenga usugu wakiakili na kimwili

-Tusifanye watu wasihofie kufa.

Kwa wenzetu somalia, syria, Iraq, Libya nk hawahofii tena jeshi, mabom wala vifaru. Wao niwahanga wakutojifaham kiakili nakimwili baada ya mazowea yamuda mrefu kwa watawala kutumia jeshi kuendekeza utawala wa vitisho.

Tunaona nakushuhudia mtu huko kwa wenzetu anakimbiza kifaru kwa jiwe au fimbo! Tusiwapeleke raia huko maana itakuwa kilio nakusaga meno
 
Asubuhi nimetoka Tunduma kufika Songwe kuna magari zaid ya hamsini yamesimamishwa MP mmoja wa Jeshi akatuamuru tushuke huku mikono juu, tukapangwa mstari na kusachiwa unaambiwa kama unahela simu au pochi shika mikononi (wakati ikiwa juu)

Wanawake wanasachiwa na askari wa kike na wanaume kwa wanaume, huku unaulizwa maswali ya kizushi uraia wako kabila lako kitambulisho nak.

Tumetoka Songwe kufika Mbeya mjini mchezo ni uleule magari yote hasa ya abiria, abiria tumeshushwa kijeshi mikono juu na kusachiwa huku unaambiwa kimbia kwenda mbele kama mita miatano ndio unaenda kupanda gari lako.

Haijalishi wamama wazee au wenye watoto wote mchakamchaka, ukisema unaumwa wanakwambia wanaoumwa wako Hospitalini, ukileta utani unaambiwa ruka kichura kabla ya kuambiwa simama na kukimbia sana.

Licha ya nia ya mazoezi yao, ila kiasi kuna kuwajenga wananchi hofu isiyo ya lazima.

Nimegundua wananchi wanawaogopa sana Wanajeshi, kama wengekuwa polisi sidhani kama wananchi wangetii namna walivyowatii wao.

Na inasemekana zoezi ni la siku tatu usiku na mchana.
Jeshini hakuna Siasa ndio maana wananchi hawabishi.
 
Kwani Mbeya Cku Hz Sio Tena Mkoa Mpakani? Na Hapo Nanenane Sio Jirani Na Junction Ya Kwenda Malawi?

Takriban 2hrs kwa private car kuelekea mipakan, Malawi au zambia.

Hapa nikujengeana hofu tu. Kama kuhusu hofu, wangeenda Tanga, Mara, Arusha,Kmanjaro na Mwanza mpaka wa Kenya karibia na Alshabab.

Huku mbeya ilikuwa enzi za ubaguzi wa rangi na Makaburu kwasasa hilo halipo au ndo hofu ya banyamulenge?
 
Jeshini hakuna Siasa ndio maana wananchi hawabishi.


Kabisaa wale jamaa hakuna mjadala,

Ukifanya ujuwaji unaweza pata buti la tumboni hivihivi au kuogeshwa vumbi au tope.

We tii sheria na maelekezo tao utabaki salama.
 
Kabisaa wale jamaa hakuna mjadala,

Ukifanya ujuwaji unaweza pata buti la tumboni hivihivi au kuogeshwa vumbi au tope.

We tii sheria na maelekezo tao utabaki salama.

Kuna haja ya kuwashirikisha hawa Jamaa kwenye baadhi ya Matukio ya Ulinzi wa ndani ya Nchi ili kuwakumbusha Raia kwamba kuna wakati unatakiwa kutii Amri bila kuhoji.Polisi wamezoeleka sana kiasi kwamba hata Mhalifu anaweza kuwavimbia.
 
Usihofu ni mazoezi tu ya kukabiliana na Ugaidi mazoezi kama hayo yalishafanywa hata huko SONGEA Raia wengi endeleeni na kazi kama kawaida vijana wenu wako kazini.

hakuna jeshi duniani linalofanya mazoezi kamahaya ya kusachiwatu. kwa mtindo jambo lolote laweza tokea.nadhanikuna kitu wameplan na kuna siku kitajulikana.
 
Mkuu temea chin. Hawababaishwi hawa nimahodari wa majigambo tambo navitisho, usipoeleweka ukishushiwa adhabu hutosaham mpaka kwa God.

Uzuri ni kwamba hata wanasiasa hawana ubavu wa Kuwakemea.Nakumbuka walivyogomea Miito ya kujiuzulu wakati wa Milipuko ya Mbagala na Gongo la Mboto na wote wakanywea.
 
Back
Top Bottom