Nadhani kuna sehemu sisi kama watanzania tunakwama sana.
Nani alisema uwepo wa wapishi wazuri wa chakula ni miongoni mwa vigezo vya sehem kupandishwa hadhi kuwa jiji?
Mbeya hakuna nyumba nzuri, uzuri wa nyumba ni nini? utakuta unajisifia tu lakini unakotoka nyumba nzuri zilizopo sio zenu ni za mashirika ya serikali au hotel za kitalii na wewe kwenu na wazazi wako mnakaa nyumba za tembe.
Kila sehem ina umaarufu wake na Jiji la Mbeya maarufu si kwa Majengo au upishi wa chakula.
Muhimu ukifika sehem shughulikia lililokupeleka kuliko kuanza kuchunguza mambo ambayo hayana msaada kwako,, au wewe ni afisa mipango miji?
Tumechoka na thread zenu za kuisema Mbeya , sisi wenyewe wana Mbeya tumeridhika na jiji letu maana Kisoka tupo vizur , kielim tupo vizur, nguo na viatu vinapatikana kwa wing na ubora mzur. Chakula na matunda ndio usiseme.
Mwisho. Ukiona Mbeya kuwa jiji wewe inakuuma sana nenda Mahakamani fungua kesi ya madai ya kutaka Mbeya iondolewe hadhi hiyo ili wewe uridhike.