Mbeya DC: Walimu wanaotaka kuhama CWT na chama chochote wafuate taratibu watapewa uhamisho

Mbeya DC: Walimu wanaotaka kuhama CWT na chama chochote wafuate taratibu watapewa uhamisho

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya (Mbeya DC) imetoa ufafanuzi kuhusu hoja ya Mwanachama wa JamiiForums.com kuwa Walimu wa Wilaya hiyo wanapata changamoto wanapotaka kuhama kutoka Chama cha Wafanyakazi cha CWT, ambapo Wilaya imetoa maelezo kuhusu kinachotakiwa kufanyika.

Awali, Mdau huyo alidai Walimu wamejaza fomu ya kujitoa lakini wahusika wamegoma na kwamba wanapohoji wanaambiwa watulie kwa kuwa huu ni Mwaka wa Uchaguzi, akahoji Mkurugenzi (DED) na Meneja Rasilimali Watu wana mkataba gani na CWT?

Kusoma hoja ya Mdau bofya hapa ~ CHAKAMWATA kwenda Mahakamani kuzishtaki Halmashauri nchini kwa kutowalipa Walimu Tsh. Bilioni 12

Taarifa ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya (Mbeya DC) kuhusu hoja hiyo imeeleza: “Suala uhamisho wa Mtumishi kuhama chama linafanyiwa kazi kwa yeyote ambaye anahitaji na sio kweli kwamba wanaoleta maombi wanaambiwa wasubiri huu ni Mwaka wa Uchaguzi, waombaji wanatakiwa kufuata taratibu zinazotakiwa na watapata uhamisho.

“Wapo baadhi wameshapata uhamisho na wengine wapo kwenye mchakato inawezekana huyo au hao wanaotoa hoja hizo hawajafuata taratibu au wamewasilisha maombi yao kwa mdomo bila kuwa na maandishi kwa maana ya barua.

“Uhamisho unaendelea na sio kwa Walimu tu hata taaluma nyingine wanapata ihamisho ikiwa tu watafata taratibu zinazotakiwa, wafike kwa Mkurugenzi au Afisa Rasilimali Watu.

“Waombaji wote wawawasilishe maombi yao Ofisi ya Utumishi kwa maandishi kwa kuwa baadaye anaweza kutugeuka na kusema hakuomba, hivyo kama yupo ambaye ameomba kwa mazungumzo ya kirafiki anatakiwa kutambua anatakiwa kufuata utaratibu uhamisho utapatikana.”

Kuhusu utaratibu
Mbeya DC inaeleza kuhusu utaratibu wa kujiunga na vyama vya Wafanyakazi “Ajira mpya wanapokuja vyama huwa vinapewa mwaliko wa kuja kueleza sera zao, baada ya hapo Watumishi wanachagua chama cha kujiunga nacho kwa kujaza fomu, hivyo inawezekana akiwa katikati ya safari akibaini hayupo sehemu sahihi ni ruksa kuhama chama, lakini hilo linawezekana kwa kufuata taratibu zinavyotakiwa.”

Pia soma ~ CHAKAMWATA kwenda Mahakamani kuzishtaki Halmashauri nchini kwa kutowalipa Walimu Tsh. Bilioni 12
 
Back
Top Bottom