Mbeya: CCM na Shitambala wamshukia Sugu

Mbeya: CCM na Shitambala wamshukia Sugu

tuweke siasa kando, this is a wake up call to opposition parliamentalians. Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii na vikundi vingine (rasmi na visivyo rasmi) wamekuwa wakihoji utendaji kazi wa wabunge kadhaa hapa nchini, sugu ni mmoja wapo.

Najua inaweza ikawa ngumu kumeza kwa wapenzi wa vyama, sugu alipata mteremko pale mbeya mjini kutokana na udhaifu wa mgombea aliyesimamishwa na ccm.

Kwa haya ninayosoma na kusikia, kama ccm itakuwa kweli imejifunza kupitia makosa iliyofanya mwaka 2010 katika michakato ya ndani kutafuta wagombea wa kukiwakilisha chama hicho kwenye chaguzi mbalimbali za mwaka 2010 ambapo chama kiliwaengua kimizengwe wagombea wengi waliokuwa wanakubalika kwa wananchi na kuwapitisha wagombea waliowaamini wao kuwa wangepeperusha bendera ya chama vizuri basi upinzani utatakiwa ujidhatiti sana katika kutetea au hata kuongeza viti vingine vya udiwani na ubunge.

Kwa namna yoyote ile, uchaguzi ujao hautokuwa mwepesi kwa mgombea ama chama chochote kile. Wapiga kura na wananchi kwa ujumla wanazidi kujielewa, mwamko waliokuwa nao mwaka 2010 ni wazi utakuwa mara dufu ifikapo mwaka 2015 na utachagizwa sana na uwepo wa katiba mpya.

una maanisha 2015 ccm ili ishinde itasimamisha watu wasiokubalika kwenye chama? Bali wanaokubalika kwa wananchi, ivi waelewa maana ya mtu hasokubalika kt chama?
 
Hata kwa ndumba Shitambala asahau ndoto ya kuwa mbunge wa Mbeya iwe mjini au vijijini. Ni msaliti mkubwa. Alisababishwa watu wakakosana na wazazi wao kisa kumuunga mkono akiwa Chadema. kwasasa huku anakodai ni kujibu mapigo ya Sugu si lolote sana sana ni jinsi ya kuanza kujitambulisha kwa wananchi ili waaanze kumzoea kuwa yeye ni gamba kwa sasa
 
ubunge kweli pipi hata sugu kaupata huyo hata ukisikiliza michango yake bungeni hamna kitu ni utumbo tu kweli CHADEMA mnatuchezea watanzania

Wee acha hizo Sugu anaongea utumbo gan?au wewe ndo huelew?sasa wabunge wa CCM kama Mwiguru huwa anaongea logic?
 
Hata kama CCM ikiwasimamisha (Nape+Mshua+Mulugo) kwa pamoja vs Sugu,bado Sugu atashinda.Trust me!
 
Shitambala ninamweshimu sana. Hata mzee wa upako ikimuonaga Mwanasheria huyu hawez kusema lolote. Sugu kama anaweza amjibu mwanasheria huyo kama alivyo mjibu Mlugo. 96% huyu jamaa ndiye aliyemweka Sugu pale.

Kwa hiyo sugu hakupigiwa kura? Au kura zote alipiga shitambala?
 
CCM inatawala kwa miaka 50+ na imeshindwa kulete maendeleo, Sugu hana dola inakuwaje na yuko kwa kipindi cha miaka 3 sasa, wanataka afanye maajabu gani? Mpeni nchi kama muone kazi!
 
Hivi ni nini maana ya jina la huyu muungwana ? Elimu yake kama ya Nape na Mwigulu nini?Yeye kaingia CCM kwa kuwa wameleta maendeleo mahali alipo sasa leo anasema anataka maendeleo ina maana aliko hakuna maendeleo wanayo pita kuhubiri mitaani wenzake ?
 
Shitambala ninamweshimu sana. Hata mzee wa upako ikimuonaga Mwanasheria huyu hawez kusema lolote. Sugu kama anaweza amjibu mwanasheria huyo kama alivyo mjibu Mlugo. 96% huyu jamaa ndiye aliyemweka Sugu pale.
Kura ya ni moja tu! zingine ni wana mbeya wenyewe
 
Shitambala ninamweshimu sana. Hata mzee wa upako ikimuonaga Mwanasheria huyu hawez kusema lolote. Sugu kama anaweza amjibu mwanasheria huyo kama alivyo mjibu Mlugo. 96% huyu jamaa ndiye aliyemweka Sugu pale.

Asee!!! Hebu tumbie alimuwekaje?maana mimi nijuavyo watu waliowekwa ni kama Mbatia na wale wakina nanihiii.
 
Wapo wanasiasa wana degree,PhD na wengine ni Maprofessor wana chokifanya utafikiri watoto wa darasa la pili!
Mfano:Shitambala na degree yake ya sheria alishindwa kusaini inayomhusu na kula kiapo kwa wakili mwenzie!
Mulugo naye vilevile kafanya madudu south!
Sugu ataendelea kutikisha tu!
 
....amekuwa akijihusisha na kuchochea vurugu au kutuliza vurugu? Ni wapi ambapo Sugu alichochea vurugu?
Ni kweli kuwa, kwa kauli ya Sugu alipokuwa akimjibu Mulugo, binafsi niligundua mapungufu makubwa, maana Sugu alijibu kitu kitu ambacho hakuulizwa au alichangia mada ambayo haikuwepo mezani, lakini kauli ya Shitambala inanifanya nisimtofautishe na Sugu.
Anapojinasibu kuwa yeye ndiye alimfanikisha Sugu kuupata Ubunge, Je, kama ana influence kubwa kwa kiwango hicho, ni vipi sasa hivi tangu kuhama kwake ni kama emezimika kabisa, au kama ana uhakika na akiongeacho basi na ajithibitishe kwa kufanya mkutano wa hadhara ili wapimwe kwa mwitiko wa watu.
 
Wana JF heshima kwenu!!
Shitambala ni mmojawapo kati ya wale walio enda shule lakini kwa bahati mbaya hawa-kuelimika na kilichobaki ni kutumiwa na chama twawala kufanikisha malengo yao. Hivyo basi watu akina Shitambala hawajiamini wala hawa aminiki na wanakuwa driven na njaa zao.

Wanajanvi naomba kuwasilisha.
 
Sugu naye asubiri muda wake tu arudi kwenye bongo freva.
 
Back
Top Bottom