babalao 2
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 5,398
- 3,244
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemshukia Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi maarufu Sugu kikimtaka asijisumbue kuchukua fomu ya kutetea nafasi hiyo mwaka 2015 kwasababu anachezea ubunge wake kutokana na kutumia muda mwingi kuchochea vurugu na maandamano badala ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Jiji la Mbeya.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (Nec), Sambwee Shitambala, amesema hayo jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari ikiwa ni siku mbili baada ya Sugu kumshambulia Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillip Mulugo kwa madai kwamba ana elimu ya kuungaunga.
Shitambala ambaye kabla ya kujiunga na CCM alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya, alisema Sugu tangu achaguliwe kazi yake kubwa imekuwa ni kuchochea vurugu, maandamano na kukashifu viongozi wa CCM na serikali na kusahau jukumu lake la msingi la kuwaletea maendeleo wapiga kura wake.
"Sugu anajisahau kuwa ubunge Mbeya amepewa kama zawadi kwa muda, mimi ndiye baba yake niliyempigia kampeni hadi akapata ubunge, elimu yake ya darasa la 12 asiitumie kukashifu viongozi wa CCM na serikali ambao wana elimu zaidi yake," alisema Shitambala.
Alisema hata hivyo hamshangai Sugu kujikita katika kuchochea vurugu kwasababu uwezo wake wa kufikiri mambo ya kuwaletea maendeleo wananchi waliomchagua umefikia kikomo sababu ubunge ameupata kama zawadi. Shitambala alisema kipimo kizuri kwa mbunge wa Mbeya mjini ni kuangalia katika kampeni za chaguzi ndogo alizoshiriki kupiga kampeni katika wilaya za Chunya, Kyela na Mbozi, zote Chadema wameshindwa.
"Sugu ameshafeli kisiasa sababu ameshindwa kutumikia wananchi, asiwe na haja ya kuchukua fomu kuwania mwaka 2015 atapa aibu, CCM Mbeya mjini tunatamani 2015 ifike hata leo Sugu ashuhudie tunavyompiga chini kwa kishindo,"alisema Shitambala.
Alisema mbunge wa Mbeya mjini lazima atambue kuwa wananchi walimchagua ili aweze kuwatatulia kero mbalimbali zinazowakabili lakini siyo kuchochea vurugu ambazo zinasababisha Jiji la Mbeya kukosa utulivu.
Hata hivyo Mbilinyi (CHADEMA), alisema hatishwi na kauli za viongozi wa CCM wanaodai majimbo yaliyoko mikononi mwa CHADEMA mkoani Mbeya, likiwamo la Mbeya Mjini yatarejeshwa mwaka 2015.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI