Tuweke siasa kando, this is a wake up call to opposition parliamentalians. Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii na vikundi vingine (rasmi na visivyo rasmi) wamekuwa wakihoji utendaji kazi wa wabunge kadhaa hapa nchini, sugu ni mmoja wapo.
Najua inaweza ikawa ngumu kumeza kwa wapenzi wa vyama, Sugu alipata mteremko pale Mbeya Mjini kutokana na udhaifu wa mgombea aliyesimamishwa na CCM.
Kwa haya ninayosoma na kusikia, kama CCM itakuwa kweli imejifunza kupitia makosa iliyofanya mwaka 2010 katika michakato ya ndani kutafuta wagombea wa kukiwakilisha chama hicho kwenye chaguzi mbalimbali za mwaka 2010 ambapo chama kiliwaengua kimizengwe wagombea wengi waliokuwa wanakubalika kwa wananchi na kuwapitisha wagombea waliowaamini wao kuwa wangepeperusha bendera ya chama vizuri basi upinzani utatakiwa ujidhatiti sana katika kutetea au hata kuongeza viti vingine vya udiwani na ubunge.
Kwa namna yoyote ile, uchaguzi ujao hautokuwa mwepesi kwa mgombea ama chama chochote kile. Wapiga kura na wananchi kwa ujumla wanazidi kujielewa, mwamko waliokuwa nao mwaka 2010 ni wazi utakuwa mara dufu ifikapo mwaka 2015 na utachagizwa sana na uwepo wa Katiba mpya.