Mbeya: CCM na Shitambala wamshukia Sugu

Mbeya: CCM na Shitambala wamshukia Sugu

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemshukia Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi maarufu Sugu kikimtaka asijisumbue kuchukua fomu ya kutetea nafasi hiyo mwaka 2015 kwasababu anachezea ubunge wake kutokana na kutumia muda mwingi kuchochea vurugu na maandamano badala ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Jiji la Mbeya.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Hapo kwenye red. Hivi kazi ya mbunge ni kuwaletea maendeleo wananchi??? Anapata wapi hizo pesa za kutekeleza miradi ya maendeleo? Au wabunge wanakusanya kodi kwenye majimbo yao siku hizi? Nadhani huu ni upotoshaji mkubwa ambao umekuwa ukifanywa kila siku na CCM. Serikali ndio inayokusanya kodi na ndio inawajibika kutekeleza miradi ya maendeleo katika nchi (including jimbo la mbunge).

Kazi ya mbunge inabaki ni kuhakikisha(kusimamia) serikali katika kuhakikisha inatekeleza mipango yake ya maendeleo na pia kukusanya kero za eneo husika na kuziwakilisha serikalini ili ziweze kufanyiwa kazi. Pia mbunge anawajibu kuhamasisha ushiriki wa wananchi wa jimbo lake(hata wale ambao hawakumpigia kura) kushiriki katika shughuli mbali mbali za maendeleo.

Nje ya hapo hata kama mbunge atakuwa mzuri kiasi gani lakini serikali ikaacha kutimiza wajibu wake basi hayo maendeleo itakuwa ndoto tu. Serikali haiwezi kujitoa katika kupeleka maendeleo kwa wananchi wake au kuurusha huu mzigo kwa mbunge.
 
Sugu naye asubiri muda wake tu arudi kwenye bongo freva.
Mkuu Ritz. Mbona wanasema ccm wanapenda wasomi ambao hawajaelimika kama shitambala na yule cjui ni nchemba ili wawaweke mstari wa mbele ni kweli hii ishu?
 
Itawachukua CCM miaka mingi kumng'oa Sugu Mbeya mjini,Watu pale wanapenda mtu (Sugu) na chama (CDM) ,jipangeni sana
 
huyu mzee arudie kazi yake ya uanasheria - watu hawaitaki ccm pamoja na yeye - Simple as that
 
Ukiwa mpinzani halafu ukaona ccm wanakuandama kwa kasi ujue umewashika penyewe. Kamanda Sugu kaza mkwiji hizi kelele za magamba ni dalili za wazi kwamba unawanyima pumzi huko Mbeya.

Sugu anawatesa sana ccm anauwezo wa kuwashambulia na kuwamudu magamba mkoa mzima wa Mbeya na bado akawashinda.
Shitambala alishindwa kupumua mbele ya mchungaji Mwanjale halafu leo anathubutu kujipiga kifua mbele ya Sugu!?
 
Kachanganyikiwa huyu Shitambala, yeye mwenyewe kashindwa kujiweka sasa atawezaje kumweka mwenzake ?.
 
Shitambala ninamweshimu sana. Hata mzee wa upako ikimuonaga Mwanasheria huyu hawez kusema lolote. Sugu kama anaweza amjibu mwanasheria huyo kama alivyo mjibu Mlugo. 96% huyu jamaa ndiye aliyemweka Sugu pale.

nachukia sana mtu mzima na akili zake kufukia kichwa mchangani kama mbuni.inawezekana vipi shitambala amuweke sugu kwenye ubunge wa mbeya mjini na wakati huo huo yeye afeli ubunge wa mbeya vijijini??msiwe mnatumika tu kipumbavu,ifike mahali muwe huru kweli kweli katika kufikiri kwenu.ana nini shitambala cha kumbeza sugu??na mfahamu fika,anashinda ibala uyole kuhamasisha vijana na kujipitisha makanisani lakini wana wa nchi wamem 'reject'.yeye anawaza ubunge wa mbeya mjini tuu,kajaa ukabila na ndio kete anayotegemea kutoka nayo ndani ya CCM hapo 2015.
 
Kachanganyikiwa huyu Shitambala..... ?.
Vita dhidi ya rushwa vinavyohimizwa na CDM,kama alivyokumbusha mbunge wake machachari SUGU jana kwenye mkutano mkubwa wa hadhara pale Kabwe-Mwanjelwa,ndivyo vinavyomtisha Shitambala.Anajua fika 2015 CDM wakiingia madarakani mshitakiwa wa kwanza atakuwa yeye,maana RUSHWA aliyoipokea mala mbili ili aachie ushindi wake wa ubunge wa Mbeya vijijini kwa mgombea wa CCM Mchungaji Mwanjali CDM wanaifahamu vema.Anamchukia sana SUGU maana alitegemea SUGU naye angeuza ushindi wake kwa Mpesya...."Kwa unyama uliyowatendea wapiga kura wa Mbeya vijijini na chama chako cha wakati ule CDM,kuuza kura zao,subiri adhabu yako 2015 CDM ikichukua nchi."
Badala ya kumfuatafuata Mbunge makini na mwadilifu SUGU,ingekuwa vema ukamsakama mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini aliyewatukana walimu wa jiji la Mbeya kuwa ni mambumbumbu,walimu wote na wanafunzi wao watapigia CDM 2015,Subiri uone anguko kuu na la aibu la CCM-2015.Mbunge (huenda asiwe SUGU maana kasema anataka awe MEYA),Madiwani na viongozi wa mitaa watatoka CDM.
Tunajua Shitambala baada ya kusikia SUGU kasema anataka awe Meya unaleta siasa ili uonekane wewe ndo umemshauri asigombee.Kumbuka wagombea wote toka CDM 2015 watashinda maana imani ya wakazi wa jiji la Mbeya kwa CCM IMEKWISHA.
 
Wee acha hizo Sugu anaongea utumbo gan?au wewe ndo huelew?sasa wabunge wa CCM kama Mwiguru huwa anaongea logic?

hiv unataka tubishane hata kwa mambo ya sugu?? sugu anaongeaga nini?? anapeleka hip jop bungeni CDM nyie mnafanya majaribio sana
 
Mkuu moja ya hoja ya kukosana na CDM huyu Advocate Shitambala ilikuwa ni kukubali matokeo ya jimbo alilogombea kupindishwa na hatimaye jimbo likachukuliwa na CCM,so kwa mujibu wa CDM Shitambala alishinda jimbo lile kiuhalali lakini akahongwa na ccm kukubali matokeo yapindishwe.

My take: Sugu alikosea sana kumzodoe Mulugo kwa kiwango chake cha elimu wakati yeye hata hiyo Digrii ya kuungaunga hana. Siasa za Bongo bana raha sana eti elimu ya darasa la 12 dah!!!!
suala co kumzodoa kwasabb yeye ni 4m4, issue ni je huyoMulugo amepitia njia sahihi ktk elimu yake???

kama ni kweli Amim ni jina lake, hilo Mulugo limetoka wapi??? sugu ni 4m4 ambayo haina meandering na wala yy hakatai
 
Shitambala naona kama zawadi ya NEC ndio ilikusababisha ukaasi chama cha CHADEMA leo hii unakuja na sera za kitoto kabisa yaani kwa sera hizi CCM naona kama mwisho umeshakaribia na 2015 CCM itakufa kifo cha mende na kamwe CCM itasambaratika kabisa
 
Shitambala naona kama zawadi ya NEC ndio ilikusababisha ukaasi chama cha CHADEMA leo hii unakuja na sera za kitoto kabisa yaani kwa sera hizi CCM naona kama mwisho umeshakaribia na 2015 CCM itakufa kifo cha mende na kamwe CCM itasambaratika kabisa

Huyu bwana hajatuambia wanakuja na mbinu gani kwani jimbo walikuwa nalo likawashinda.
 
Hapo kwenye hoja ya kumtaka SUGU afanye kazi ili aendelee kubaki kwenye nafasi hiyo ni pa kupaangalia vizuri si kwa SUGU bali wabunge wote cuz tuendako tutaanza kuuliza achievement za viongozi waliopita
 
Back
Top Bottom