Mbelwa Germano
JF-Expert Member
- May 7, 2011
- 789
- 293
CCM na shitmbara hawana jipya mbeya, ninanavyo wafahamu ndugu zangu wa mbeya wakisema no ni no
Wabunge wengine waliotangulia wamefanya nini.
Umeond eeh! Kwanza naona huyu mjinga shitambala bado hatujui vizur wana mbeya. Aje agombee aone.huyu jamaa shitambala naye si aligombea mbeya vijijini mbona alishindwa???? alimuwekaje sugu kama yeye mwenyewe alishindwa kujiweka??? acheni unafiki, plz muwage wakweli na unazi muwekage pembeni, huyo bwn anatwanga maji kwny kinu wanabaki kutapatapa.
kwa hiyo kura yake moja ndio iliyompa ubunge?Shitambala ninamweshimu sana. Hata mzee wa upako ikimuonaga Mwanasheria huyu hawez kusema lolote. Sugu kama anaweza amjibu mwanasheria huyo kama alivyo mjibu Mlugo. 96% huyu jamaa ndiye aliyemweka Sugu pale.
Nahisi kama mnaendelea kuchezea akili za watu hapa vile, Shitambala alikua anagombea Mbeya Vijijini na alikua akiendelea na kampeni zake ili naye aingie Bungeni, sasa hapo ilikuaje achangia hizo % ulizoweka hapo mkuu, unaweza kuwa busy na chungu cha mwenzio while huna hakika na chungu chako? Guys let us by serious for sometimes, Chitambala tunajua kua alishinda uchaguzi ule kule vijijini lakini kiu na tamaa ya pesa akamfikisha hapo alipo leo, mikutano ya Sugu na Mbeya yake wote huwa tunaiona, watu wa Mbeya waliisha tamka kuwa Rais wao ni Sugu, kama issue ya maandamano, mbona kila wakati hua yanasababishwa na serikali yenyewe, rejea maandamano ya wamachinga wakati ule, mkono wa Sugu pale ulikua wapi? Kwanza alikua zake Dodoma, nakumbuka hadi jeshi liliingilia kati lakini Sugu alipofika tu from dodoma, mambo yakawa sawa, Wasomi type ya Shitambala ndio janga lenyewe la taifa, hawaelezi kiini cha tatizo, huangalia matumbo yao then na ubongo wanahamishia huko huko tumboni, Bora Form 4 ya Sugu kuliko degree za akina Shitambala, Mchemba, Nape na hata Amini! Sijaona impact za elim zao kwa nchi au hata sehemu ambazo wanakotoka, Nendeni Singida anakotoka bwana Chemba mwone.
Shitambala ninamweshimu sana. Hata mzee wa upako ikimuonaga Mwanasheria huyu hawez kusema lolote. Sugu kama anaweza amjibu mwanasheria huyo kama alivyo mjibu Mlugo. 96% huyu jamaa ndiye aliyemweka Sugu pale.
njaa mbaya sanaChama Cha Mapinduzi (CCM) kimemshukia Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi maarufu Sugu kikimtaka asijisumbue kuchukua fomu ya kutetea nafasi hiyo mwaka 2015 kwasababu anachezea ubunge wake kutokana na kutumia muda mwingi kuchochea vurugu na maandamano badala ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Jiji la Mbeya.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (Nec), Sambwee Shitambala, amesema hayo jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari ikiwa ni siku mbili baada ya Sugu kumshambulia Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillip Mulugo kwa madai kwamba ana elimu ya kuungaunga.
Shitambala ambaye kabla ya kujiunga na CCM alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya, alisema Sugu tangu achaguliwe kazi yake kubwa imekuwa ni kuchochea vurugu, maandamano na kukashifu viongozi wa CCM na serikali na kusahau jukumu lake la msingi la kuwaletea maendeleo wapiga kura wake.
Sugu anajisahau kuwa ubunge Mbeya amepewa kama zawadi kwa muda, mimi ndiye baba yake niliyempigia kampeni hadi akapata ubunge, elimu yake ya darasa la 12 asiitumie kukashifu viongozi wa CCM na serikali ambao wana elimu zaidi yake, alisema Shitambala.
Alisema hata hivyo hamshangai Sugu kujikita katika kuchochea vurugu kwasababu uwezo wake wa kufikiri mambo ya kuwaletea maendeleo wananchi waliomchagua umefikia kikomo sababu ubunge ameupata kama zawadi. Shitambala alisema kipimo kizuri kwa mbunge wa Mbeya mjini ni kuangalia katika kampeni za chaguzi ndogo alizoshiriki kupiga kampeni katika wilaya za Chunya, Kyela na Mbozi, zote Chadema wameshindwa.
Sugu ameshafeli kisiasa sababu ameshindwa kutumikia wananchi, asiwe na haja ya kuchukua fomu kuwania mwaka 2015 atapa aibu, CCM Mbeya mjini tunatamani 2015 ifike hata leo Sugu ashuhudie tunavyompiga chini kwa kishindo,alisema Shitambala.
Alisema mbunge wa Mbeya mjini lazima atambue kuwa wananchi walimchagua ili aweze kuwatatulia kero mbalimbali zinazowakabili lakini siyo kuchochea vurugu ambazo zinasababisha Jiji la Mbeya kukosa utulivu.
Hata hivyo Mbilinyi (CHADEMA), alisema hatishwi na kauli za viongozi wa CCM wanaodai majimbo yaliyoko mikononi mwa CHADEMA mkoani Mbeya, likiwamo la Mbeya Mjini yatarejeshwa mwaka 2015.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Mkuu moja ya hoja ya kukosana na CDM huyu Advocate Shitambala ilikuwa ni kukubali matokeo ya jimbo alilogombea kupindishwa na hatimaye jimbo likachukuliwa na CCM,so kwa mujibu wa CDM Shitambala alishinda jimbo lile kiuhalali lakini akahongwa na ccm kukubali matokeo yapindishwe.
My take: Sugu alikosea sana kumzodoe Mulugo kwa kiwango chake cha elimu wakati yeye hata hiyo Digrii ya kuungaunga hana. Siasa za Bongo bana raha sana eti elimu ya darasa la 12 dah!!!!
njaa mbaya sana