Mazishi ya wanapinduzi wa Nyamongo, TARIME

Mazishi ya wanapinduzi wa Nyamongo, TARIME

wanamapinduzi? That is nonsense... Mwizi mwizi tuu, ata akimuibia shetani ( BARRICK) bado mwizi tuu..
 
Ni majambazi sio wanamapinduzi. hivi nyie hamuijui mara kwa ujambazi?

If that is true. kwanini serikali ilikua inawapa fedha za maziko/rambirambi?? Hapo ndio tunapomchanganya mwananchi wakawaida.
 
Acha kukurupuka Mahesabu nani kakuambia waliouawa ni wezi? hivi unajua kila mtu ni "innocent" kabla mahakama haijatoa hukumu? kwa mtu smart ulitakiwa useme "watuhumiwa" kwa hii post yako mimi nahisi wewe ni mwenda wazimu lakini sitokuita mwenda wazimu mpaka ushahidi wa kitabibu utolewe. Any way nilikuwa nakukumbusha tuu uwe makini na maneno yako ipo siku utakuwa na la kujibu.

Serikali ya Kikwete ilishatoa hiyo hukumu kupitia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tarime kuwa wale walikuwa ni majambazi. Ndiyo maana mwenzetu Mahesabu anashangaa kusikia kuwa familia ya majambazi watalipwa rambirambi ya Mil. 3 kwa kila familia.
 
Mimi siku zote husimamia haki na daima huwa upande wa wanyonge dhidi ya maovu. Ila kamwe siwezi kuunga mkono uvamizi wa mgodi wa North Mara na kuwaita waliouwawa wanamapinduzi -- hapa tunachezea maana halisi ya wanamapinduzi.

Wote hapa hatujui nini haswa kilitokea, lakini based on police statements ni kuwa kundi la watu 800 mpaka 1,000 walivamia mgodi wa North Mara wakiwa na mapanga, marungu na silaha zingine za jadi wakawa wanataka kuiba gold ore kwa lengo la kwenda kuiuza na kujinufaisha wao wenyewe.

Sawa, wananchi wa Nyamongo wana manung'uniko yao ya muda mrefu kuhusu mwekezaji kupewa eneo hilo lakini kisheria Barrick ni mmiliki halali wa mgodi huo. Hivyo watu 8 au watu 800 wakiingia ndani ya mgodi huo kinyume cha sheria kwa lengo la kuiba mawe ya dhahabu watu hao ni wezi au wavamizi tu, kamwe si wanamapinduzi.

Ni kama wewe ukiwa na shamba lako lenye hati umeuziwa na serikali ya kijiji, umejenga ukuta na kuweka geti. Sasa wakaja wanakijiji 800 na kuvamia eneo hilo kwa lengo la kuiba ng'ombe wako utawaita hao wanakijiji wanamapinduzi au wezi? Ndiyo maana wengine wameweka vibao kwenye mashamba yao kuwa "Trespassers will be shot!"

Kama wanakijiji wa Nyamongo wana malalamiko kuhusu mgodi huo ni vyema CHADEMA na wanasiasa wengine wakawafundisha utaratibu mzuri zaidi wa kudai haki zao, si kuvamia na kuiba mawe ya dhahabu kwani Barrick watakuwa na haki ya kulinda mali zao.

Nadhani polisi walitumia excessive force kama wanavyofanya kila siku wanapouwa watuhumiwa wa ujambazi au wananchi wasio na silaha kwenye maandamano kama ya Arusha.

Hatuwezi kuunga mkono uvunjaji wa sheria hata kama wananchi hawa wana madai halali, pia serikali itaonekana ni ya kipuuzi mbele ya wawekezaji wa kimataifa kama itashindwa kulinda mali za wawekezaji kutoka kwa wavamizi.

Ni lahisi ssana kuandika na kusema uyasemayo na kwa sababu si wewe au baba yako au mamayako mdogoyo au ndugu yeyiote wa damu yako huna uzalendo na una roho ya ukatili sana kwa vile unanufaika na minuso ya ikulu isivyo halali unafurahia jinsi watanzania walivyouuawa kinyama,hebu tuambie kuna sheria gani ya polisi inayomruhusu kuua mhalifu anayekimbia,ripoti ya postmortum ianonyesha wote wamepigwa kwa nyuma
Unasema Chadema watoe elimu ya wao kudai haki yao ,we zuzu serikali inafanya nini kwa nini wasianzishe elimu ya upatanisho na kusimamia haki za binadamu
Serikali ya Jakaya Kikwete ni katili kuliko serikali yeyote tangu uhuru wa nchi ,majibu ya sera zake za kuua wananchi zitampa majibu yake
 
Kasparov & Karpov, you remind me of some sweet moments in Sofia, Bulgaria in the 80's. R.I.P. Nyamongo's innocent souls, victims of stray bullets? Typical intra-natives conflict in Sub-Saharan Africa, cause and effects of neo-colonialism!
 
Ni majambazi sio wanamapinduzi. hivi nyie hamuijui mara kwa ujambazi?
Kweli we ni mwendawazimu, lazima utakuwa mpemba wewe... Osama mlikuwa mnamuita mwanamapinduzi lakini watanzania wenzio walionyang'anywa ardhi zao kwa lazima akapewa muwekezaji na kuwaacha ktk umaskini wa kutupwa wanapouwawa badala ya kukamatwa, tena na jeshi linaloendeshwa na kodi zetu unashadadia... We lazima utakuwa muislamu tu.
 
Taarifa za vyombo vya Dola zilisema walikuwa watu zaidi ya 800, katika hali ya kawaida hakuna majambazi wanoweza kufikia idadi kama hiyo, maana wataonekana hadharani ilhali majambazi wanatakiwa kujificha ili wasionekane. Ni kweli kwamba mgodi unatakiwa kulindwa kama mabenki au Kampuni yoyote yenye vito vya thamani. Lakini katika historia ya nchi yetu hakuna benki iliyowahi kuvamiwa na majambazi 800 au zaidi.

Kulingana na uelewa wangu hawa waliouwawa Nyamongo, ningeweza kuwaita wavamizi, lakini pia najiuliza kulikoni hadi watu 800 wavamie eneo ambalo wanafahamu kuwa lina ulinzi mkali? Kumbuka kuwa mgodi wa North Mara unalindwa na makundi mawili la kwanza ni Askari Polisi/FFU na la pili ni Askari wa Mgodi tena nao wana sila wanaoitwa "Mobile".

Nilipotafakari mambo yote hayo, nikaona kwamba hadi kufikia watu 800 kwenda kuvamia sehemu kama hiyo hata kama walitaka kuiba, maana yake ni kwamaba wamekata tamaa na wanaenda lolote liwe. Kwa maana nyingine ni kwamba wamefikia kikomo cha uvumilivu na hali ya eneo hilo, hivyo, wanahitaji kusikilizwa na mabadiliko kufanyika. KUFIKIA HAPO, NAMI NIKAWAITA WANAMAPINDUZI.

good point. jana MTM alisema binadamu anapoteswa na kufanyiwa vitu visivyostahili huondokewa na ubinadamu na kuvaa unyama. kwa hiiyo ni jukumu la serikali kuondoa hali ya unyama kwa kuleta ulinganisho (equity) katika umilikaji wa rasilimali asili (unapotoa mgodi kwa wageni bila kuzingatia locals unategemea matokeo gani mbeleni.. nasema tena serikali ijuelize inapotoa migodi kwa wageni bila kulinda maslahi ya wazawa wa eneo husika utegemee nini?????????????????
 
hizo ni akili za kizamani wewe, bila mzungu unafikiri ungekula leo?

mzungu ndio Mungu wako. Yaonekana u moja wao wanaoabudu miungu w2. Bwana Muzungu asifiwe sana.
 
Hawa ni wanamapinduzi na mashahidi wa haki. Damu ya ni sadaka na kupitia damu yao, ipo siku wanyonge watakombolewa.

Ukweli, siungi mkono wayafanyayo CDM lakini katika hili niko pamoja nao na hususani familia za wafiwa watanzania wenzetu. Imagine, kama kaka yako au mdogo wako angekuwa miongoni mwa waliouawa na kisha ukakukuta jeneza la mwili wake limetelekezwa barabarani.

Tuachane na ushabiki wa kisiasa tujadili hoja kama wanadamu, watanzania na wazalendo wapenda mabadiliko. Tanzania tunaelekea pabaya, sote tu masahidi......
 
Japo tumetoka nje ya "malengo" ya mtoa thread.
Pia na mimi nitatoka so Nyami2010 uniwie radhi,
Sababu sina taarifa ya maendeleo ya mazishi ya MASHAIDI wetu (Mungu awajalie haki yao, RIP).
Tungekuwa na serikali sikivu,
Huu ungekuwa muda muafaka wa kufanya maptio ya migogoro yote inayoendelea kwenye migodi mingine na mapitio ya sheria husika ili kunufaisha zaidi waliopembezoni.
Kama hilo lisipofanyika basi tujue mbegu iliyopandikizwa kwa unyama uliofanyika juu ya hao raia wenzetu, itaendelea kuota na kusambaa kwenye maeneo yote ya migodi kwani taarifa zinaonyesha maeneo mengi ya migodini yana migogoro kati ya wawekezaji na wanavijiji.
Na hili litakuwa baya zaidi kwa serikali yetu ombaomba sababu hao wawekezaji wao watapaona Tanzania pachungu.
 
wezi waitwa wanamapinduzi......! siasa bwana!

Mwizi nani kati ya Barrick + Serikali ya magamba na wanatarime? Acha hizo wewe je kwakuwa wanatarime hawana silaha na nguvu ya katiba kulinda mali yao ya asili wageuke kuwa wezi na wale ambao kwa kutumia sheria walizozitunga wao wenyewe na silaha zao nzito kuja kuibia watu ambao walipaswa kuwalinda ndiyo wanamapinduzi? Mungu akusamehe; unawasaliti ndugu zako (watanzania) kisa hayo makombo yanayodondoka chini yameza ya mfalme! Naona aibu kukuita wewe mtanzania mwenzangu, nadhani wewe huna asili na nchi yangu pengine ni mlowezi ama ni artificial race iliyokulia Masaki na Oiysterbey kwa garama ya kodi ya watanzania unaowasaliti leo.

Laana yako ni kubwa na aibu yako itaenda mpaka kizazi chako cha nne! Mungu hawezi bariki mbinafsi kama wewe usiye na shukrani dhidi ya watu wachache waliochangia mafanikio yako hadi ukafikia hatua ya kuweza kuwa na lap/desk top na pesa ya ziada kulipia connection service huku mamilioni ya raia wenzako wakiwa hawana hata uwezo wa kupata mlo mmoja kwa siku! You are a disgrace to this country and you better vanish than to live for ur survival is costing other peoples lives!

Umeni provoke wewe na kwa upako cheo changu cha prince haya niliyo kutabiria hayata acha kukupata!
 
wezi waitwa wanamapinduzi......! siasa bwana!

ndugu kwa iyo wezi wanapaswa kuuawa siyo? Ipo siku utagundua thamani ya mtu ijapokuwa utu wako kama mahesabu umekufa!
 
wezi waitwa wanamapinduzi......! siasa bwana!

Ni kweli kabisa ndugu, ndio maana serikali yako nimeshangaa siku hizi inatoa ubani wa millioni tatu kwa wezi wakati shule hazina vitabu wala madawati, inaonekana hawa wote ni wezi watupu wakiongozwa na mwizi mkuu KIKWETE.
 
Kazi kwei kwei, ati wanamapinduzi lol
Kila kitu sasa kinataka kugeuzwa siasa
 
Hata mimi nilikuwa na wasi wasi kama wewe, lakini taarifa za vyombo vya Dola zilisema walikuwa watu zaidi ya 800, katika hali ya kawaida hakuna majambazi wanoweza kufikia idadi kama hiyo, maana wataonekana hadharani ilhali majambazi wanatakiwa kujificha ili wasionekane. Ni kweli kwamba mgodi unatakiwa kulindwa kama mabenki au Kampuni yoyote yenye vito vya thamani. Lakini katika historia ya nchi yetu hakuna benki iliyowahi kuvamiwa na majambazi 800 au zaidi.

Kulingana na uelewa wangu hawa waliouwawa Nyamongo, ningeweza kuwaita wavamizi, lakini pia najiuliza kulikoni hadi watu 800 wavamie eneo ambalo wanafahamu kuwa lina ulinzi mkali? Kumbuka kuwa mgodi wa North Mara unalindwa na makundi mawili la kwanza ni Askari Polisi/FFU na la pili ni Askari wa Mgodi tena nao wana sila wanaoitwa "Mobile".

Nilipotafakari mambo yote hayo, nikaona kwamba hadi kufikia watu 800 kwenda kuvamia sehemu kama hiyo hata kama walitaka kuiba, maana yake ni kwamaba wamekata tamaa na wanaenda lolote liwe. Kwa maana nyingine ni kwamba wamefikia kikomo cha uvumilivu na hali ya eneo hilo, hivyo, wanahitaji kusikilizwa na mabadiliko kufanyika. KUFIKIA HAPO, NAMI NIKAWAITA WANAMAPINDUZI.


Well said and argued!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom