Mazishi ya wanapinduzi wa Nyamongo, TARIME

Mazishi ya wanapinduzi wa Nyamongo, TARIME

hivi ukimwibia mzungu ni kosa? wakati wao walituibia mali zetu na bado wanatufata kutuibia, hawa vijana walikuwa wakijaribu kujikwamua kimaisha kwani wao ndio waliogundua madini, ifike hatua kwamba wananchi wakigundua madini wapewe kipaumbele wafaidi mali zao . Hata hivyo inasemekana ilikuwa dili la polisi na baadhi ya wananchi police huwapa magwanda polisi ili waingie wachimbe alafu wagawane dili lilipokufwa ili wasipoteze ajira ilibidi wawaue wpoteze ushahidi
hizo ni akili za kizamani wewe, bila mzungu unafikiri ungekula leo?
 
wamevamia mali yenye wenyewe sasa ulitegemea wapewe matofali ya dhahabu? mbona nyie wake zenu wakisemeshwa mnakua wakali? Kila mtu lazima alinde chake na wewe kwa akili zako unafikiri kwanini waliwekwa walinde polisi hapo? Hakuna cha wanamapinduzi hapa. Siku zote wanaiba hapo mgodini lakini safari hii walitaka wachukue yote.

Narrow mind!
 
Siasa kazi kweli kweli............

Hadi inafika 2015 sijui............
 
Eti 'WANAMAPINDUZI',kumbe ukiiba ckuiz unakuwa mwanamapinduz?you must be kiddin'

Mkare_wenu,Mahesabu na Fareed hamna uzalendo hata kidogo, wazungu wanavyoleta ndege kila wiki kuiba madini yetu bila hata kuhakkikiwa na TRA mnaona sawa lakini Mtanzania akichukua udongo ambao ni mali ya nchi yake anakuwa mwizi.

Mgogoro huu ni zaidi ya wizi wa mchanga wa dhahabu bali ni harakati za wananyamongo kudai haki zao zilizochukuliwa na Barrick kiujanja ujanja. Kwanini hamtaki kujielimisha vyanzo vya migogoro kabla hamachangia?
 
Kwa mtazamo wangu ni mapema sana kuwaita "wanamapinduzi" au "wezi" kwani ukweli wa tukio naona bado haujawekwa wazi na wahusika!
 
Idadi ya watu 800 kwa vijiji vya Mara, ukiondoa wanawake, wazee na watoto? Hicho kijiji kina watu wangapi.....

Kama ilivyotangazwa marehemu wanatoka vijiji vya Kewanja, tarafa ya Ingwe; Nyakunguru, Inchage; na Komaswa, Inano. Ina maana hawakutoka kikiji kimoja. Kwa maoni yangu watu hawa wameungana dhidi ya Barick North Mara. Natumaini hata wameacha vita wenyewe kwa wenyewe iliyokuwepo.
 
Kwa mtazamo wangu ni mapema sana kuwaita "wanamapinduzi" au "wezi" kwani ukweli wa tukio naona bado haujawekwa wazi na wahusika!

Hata mimi nilikuwa na wasi wasi kama wewe, lakini taarifa za vyombo vya Dola zilisema walikuwa watu zaidi ya 800, katika hali ya kawaida hakuna majambazi wanoweza kufikia idadi kama hiyo, maana wataonekana hadharani ilhali majambazi wanatakiwa kujificha ili wasionekane. Ni kweli kwamba mgodi unatakiwa kulindwa kama mabenki au Kampuni yoyote yenye vito vya thamani. Lakini katika historia ya nchi yetu hakuna benki iliyowahi kuvamiwa na majambazi 800 au zaidi.

Kulingana na uelewa wangu hawa waliouwawa Nyamongo, ningeweza kuwaita wavamizi, lakini pia najiuliza kulikoni hadi watu 800 wavamie eneo ambalo wanafahamu kuwa lina ulinzi mkali? Kumbuka kuwa mgodi wa North Mara unalindwa na makundi mawili la kwanza ni Askari Polisi/FFU na la pili ni Askari wa Mgodi tena nao wana sila wanaoitwa "Mobile".

Nilipotafakari mambo yote hayo, nikaona kwamba hadi kufikia watu 800 kwenda kuvamia sehemu kama hiyo hata kama walitaka kuiba, maana yake ni kwamaba wamekata tamaa na wanaenda lolote liwe. Kwa maana nyingine ni kwamba wamefikia kikomo cha uvumilivu na hali ya eneo hilo, hivyo, wanahitaji kusikilizwa na mabadiliko kufanyika. KUFIKIA HAPO, NAMI NIKAWAITA WANAMAPINDUZI.
 
Sawabho umenena wacha nitoke kwanza nitarudi ila magamba wasome mistari yako mwanzo hadi mwisho.:mod:
 
Katika hali yoyote ila, hawa marehemu (5) waliouawa kinyama huko Nyamongo hawakuwa wezi wala wavamizi.

Jiulize, ni wapi duniani kundi la wezi likawa na watu wapatao 800? Kwa vyovyote kuna tatizo ambalo wadau wote, hususani serikali, wananchi wa Nyamongo (tarime) na Barrick lazima wakae katika meza ya majadiliano. Barrick wanatekelezaji mpango wake wa wajibu wa kampuni kwa wananchi "Corporate social responsibility". Sharti, ushabiki wa kiasa lazima tuuweke pembeni katika hili.

Kwangu mimi, hawa marehemu ni WANAPINDUZI, MASHAHIDI, na WAPIGANAJI wa kweli...(R.I.P)
 
Kama walikua 800 basi hao polisi hana shabaha, msitake kuleta uzushi hapa, hakuna cha mia nane, ni majambazi wacheche tu walivamia na wamekula shaba.
 
Taarifa za vyombo vya Dola zilisema walikuwa watu zaidi ya 800, katika hali ya kawaida hakuna majambazi wanoweza kufikia idadi kama hiyo, maana wataonekana hadharani ilhali majambazi wanatakiwa kujificha ili wasionekane. Ni kweli kwamba mgodi unatakiwa kulindwa kama mabenki au Kampuni yoyote yenye vito vya thamani. Lakini katika historia ya nchi yetu hakuna benki iliyowahi kuvamiwa na majambazi 800 au zaidi.

Kulingana na uelewa wangu hawa waliouwawa Nyamongo, ningeweza kuwaita wavamizi, lakini pia najiuliza kulikoni hadi watu 800 wavamie eneo ambalo wanafahamu kuwa lina ulinzi mkali? Kumbuka kuwa mgodi wa North Mara unalindwa na makundi mawili la kwanza ni Askari Polisi/FFU na la pili ni Askari wa Mgodi tena nao wana sila wanaoitwa "Mobile".

Nilipotafakari mambo yote hayo, nikaona kwamba hadi kufikia watu 800 kwenda kuvamia sehemu kama hiyo hata kama walitaka kuiba, maana yake ni kwamaba wamekata tamaa na wanaenda lolote liwe. Kwa maana nyingine ni kwamba wamefikia kikomo cha uvumilivu na hali ya eneo hilo, hivyo, wanahitaji kusikilizwa na mabadiliko kufanyika. KUFIKIA HAPO, NAMI NIKAWAITA WANAMAPINDUZI.

iMimi nipo tofauti na wewe.

haiwezekani watu zaidi 800 walikuwa wanakwenda kuiba. Labda walikuwa wanaandamana kuelekea mgodini kwenda kudai haki zao kama wanakijiji.
Kwani inaonyesha watu hao waliujua vizuri sana ulinzi ndani a mgodi huo nao walikuwa na silaha za jadi. Tunajua sote tarime AK 47 ni nyingi tu nkama walitaka kuiba basi nao wangekwenda kamili kamili
 
Hata mimi nilikuwa na wasi wasi kama wewe, lakini taarifa za vyombo vya Dola zilisema walikuwa watu zaidi ya 800, katika hali ya kawaida hakuna majambazi wanoweza kufikia idadi kama hiyo, maana wataonekana hadharani ilhali majambazi wanatakiwa kujificha ili wasionekane. Ni kweli kwamba mgodi unatakiwa kulindwa kama mabenki au Kampuni yoyote yenye vito vya thamani. Lakini katika historia ya nchi yetu hakuna benki iliyowahi kuvamiwa na majambazi 800 au zaidi.

Kulingana na uelewa wangu hawa waliouwawa Nyamongo, ningeweza kuwaita wavamizi, lakini pia najiuliza kulikoni hadi watu 800 wavamie eneo ambalo wanafahamu kuwa lina ulinzi mkali? Kumbuka kuwa mgodi wa North Mara unalindwa na makundi mawili la kwanza ni Askari Polisi/FFU na la pili ni Askari wa Mgodi tena nao wana sila wanaoitwa "Mobile".

Nilipotafakari mambo yote hayo, nikaona kwamba hadi kufikia watu 800 kwenda kuvamia sehemu kama hiyo hata kama walitaka kuiba, maana yake ni kwamaba wamekata tamaa na wanaenda lolote liwe. Kwa maana nyingine ni kwamba wamefikia kikomo cha uvumilivu na hali ya eneo hilo, hivyo, wanahitaji kusikilizwa na mabadiliko kufanyika. KUFIKIA HAPO, NAMI NIKAWAITA WANAMAPINDUZI.

Mimi siku zote husimamia haki na daima huwa upande wa wanyonge dhidi ya maovu. Ila kamwe siwezi kuunga mkono uvamizi wa mgodi wa North Mara na kuwaita waliouwawa wanamapinduzi -- hapa tunachezea maana halisi ya wanamapinduzi.

Wote hapa hatujui nini haswa kilitokea, lakini based on police statements ni kuwa kundi la watu 800 mpaka 1,000 walivamia mgodi wa North Mara wakiwa na mapanga, marungu na silaha zingine za jadi wakawa wanataka kuiba gold ore kwa lengo la kwenda kuiuza na kujinufaisha wao wenyewe.

Sawa, wananchi wa Nyamongo wana manung'uniko yao ya muda mrefu kuhusu mwekezaji kupewa eneo hilo lakini kisheria Barrick ni mmiliki halali wa mgodi huo. Hivyo watu 8 au watu 800 wakiingia ndani ya mgodi huo kinyume cha sheria kwa lengo la kuiba mawe ya dhahabu watu hao ni wezi au wavamizi tu, kamwe si wanamapinduzi.

Ni kama wewe ukiwa na shamba lako lenye hati umeuziwa na serikali ya kijiji, umejenga ukuta na kuweka geti. Sasa wakaja wanakijiji 800 na kuvamia eneo hilo kwa lengo la kuiba ng'ombe wako utawaita hao wanakijiji wanamapinduzi au wezi? Ndiyo maana wengine wameweka vibao kwenye mashamba yao kuwa "Trespassers will be shot!"

Kama wanakijiji wa Nyamongo wana malalamiko kuhusu mgodi huo ni vyema CHADEMA na wanasiasa wengine wakawafundisha utaratibu mzuri zaidi wa kudai haki zao, si kuvamia na kuiba mawe ya dhahabu kwani Barrick watakuwa na haki ya kulinda mali zao.

Nadhani polisi walitumia excessive force kama wanavyofanya kila siku wanapouwa watuhumiwa wa ujambazi au wananchi wasio na silaha kwenye maandamano kama ya Arusha.

Hatuwezi kuunga mkono uvunjaji wa sheria hata kama wananchi hawa wana madai halali, pia serikali itaonekana ni ya kipuuzi mbele ya wawekezaji wa kimataifa kama itashindwa kulinda mali za wawekezaji kutoka kwa wavamizi.
 
Bottomline ni kwamba serikali siyo makini lakini wapande washuke wanabidi wakubali moja kati ya haya mawili:

1. Marehemu waliuwawa kwa vile walikuwa wanataka kuvunja na kuiba dhahabu - na hili la kuzika wezi na kutoa rambirambi ni sera mya kwa kujali watu wetu

au

2. Waliuwawa bila kosa na taarifa tuliyopewa ilikuwa ya uongo ndiyo sababu wanataka wawazike na wawape rambirambi

Njia ya muongo ni fupi hivyo ukitaka kudanganya lazima uwe na kumbukumbu na pia uweze kuforesee utacheza kete gani baada ya round kadhaa za hii chase(Uwe kama Kasparov na Kapov)
 
Polisi wapuuzi sana hawa hawajui mishahara yao inatokana na kodi zetu?

Habari nilizonazo pesa na rambi rambi za Mil 3 kwa kila familia zimetolewa na barrrick...what a shame jamani!!
 
Back
Top Bottom