Mazishi ya wanapinduzi wa Nyamongo, TARIME

hv wazir wa mambo ya ndani kwa nini ajaenda tarime mbona waziri mkuu kimya hv yupo?
 
Tangu zamani enzi za utumwa wageni wamekuwa wanawatumia waafrika kuwaanganiza waafrika wenzao. Hii ni kwa sababu mwafrika ni mtu mvivu na mpenda vya dezo na yupo tayari kuua mwafrika mwingine yeyote mradi dezo aliyozoea iwepo.
 
Nitunzieni Hao wahusika Wote Nikiingia Madarakani Hukumu yao itakuwa kama ya Saadam Hussein Hata kama Watakuwa ni Wastaafu... Adhabu yao Haitawapitia Pembeni... Lao wafanye wasitoke Madarakani... Hivi Ubalozi wa CANADA upo wapi watutolee hili kampuni Jinamizi liuaji Dharimu Fisadi Linalohonga bila kushtakiwa..

Tundu Lissu Kawashtaki hao mahakama ya kimataifa akiwemo Shephen Halper Waziri wao Mkuu Canada Shame of them..
 
Nauliza tu -- hivi bila shaka kuna watu walikamatwa katika tukio lile la watu kuvamia mgodi wa Tarime wakiwemo waliojeruhiwa na wasiojeruhiwa. Hivi hawa wamefikishwa mahakamani kwa kosa la uvamizi huo kwa lengo la kutaka kuiba?

Nauliza hivyo kwa sababu kama hawajafikishwa mahakamani basi serikali inasimamia wapi katika tukio lote hilo.
 
Tangu tukio la mauaji lilipotokea kila mtu amajiuliza ni kwa nini Polisi wanakuwa ’makini’ kiasi hicho kuhakikisha kwamba Barrick haisogelewi!

Habari mbaya kabisa niliyoaambiwa toka Ukuryani ambayo inaonekana ni taarifa toka ndani ya Barrick wakikerwa na uhusiano wao na wananchi wanaowazunguka ni kwamba, Mauaji hayo yanachochewa na mishara inayotolewa na Mgodi kwa mkuu wa Mkoa, Mkuu wa polisi wa Mkoa, Mkuu wa wilaya na OCD. Yawezekana na wengine weeengi.

Hawa watu yasadikiwa wana mgawo kila mwezi ikiwa ni shukrani kwa ulinzi wanaoutoa ktk mgodi.

Lakini pia Pale Musoma mjini, Mkuu wa polisi anatoa nafasi kwa askari kwenda kulinda Nyamongo kama zawadi maana kila anayekwenda kulinda pale anapewa shiling 40,000 kwa siku. Pesa hizi hutolewa na mgodi. Tofauti na malindo mengine ambayo askari huambulia mkono mtupu au kwa faida kidogo ya shilingi 20,000 au 25,000.

Sasa kumbe amani ktk eneo la Nyamongo inaondoa uhalali wa askari kwenda kuvuna pesa mgodini na njia pekee ya kuweka mazingira ya umuhimu wao kuwa mgodini ni wao kupiga raia, na sasa kuuwa ili mgodi uone umuhimu wa wao (askari) kuwa pale na hatimaye wakuu wao waendelee kupata kipato cha ziada toka mgodini.

Naweza amini. Taarifa hii inanifanya nianze kuunganisha matukio ya nyuma mpaka leo hii;
-Kwa nini Mh. Sitta alikuwa makini kiasi kile ktk kumumdhibiti Mh. Cheyo wakati akichangia mjadala wa matukio ya tindikali ya mgodi wa Barrick?
-Kwa nini tarrifa ya kamati ya Bunge iliishia uvunguni bila hata muelekeo?
-Kwa nini Waziri wa mambo ya Ndani, Kagasheki anashindwa kuwa makini kuieleza hali halisi ya ubovu wa maamuzi ya askari uliopelekea mauaji hayo?
-Kwa nini Rais na waziri Mkuu wake wako bubu bila hata la kuonyesha masikitiko ktk tukio hili?

Watu wanaolipwa na Barrick ktk nchi hii wanaweza kuwa ni wengi na hasa kwa kuzingatia matukio mabaya ya Barrick yaliyowahi kutokea ktk Dunia hii.

i smell truth
 
Jamani TZ tunatafuta laana siasa hizi zitatumaliza tunauwana wenyewe tena na polisi waliyovalia bendera ya TAIFA hivi hii nchi ilipata uhuru kweli au walipewa uhuru kundi fulani tu la watu na sasa imefikia mahali maiti wanatumika kutekeleza matakwa ya wanasiasa.uko wapi? utu wa WTZ.
 
Na polisi wanahangaika sana mwili wa mwizi uzikwe!!!!! Tusisupport vitu vingine bila kuwa na data. Mwanzisha thread hana data kamili juu ya kilichotokea Nyamongo.
wezi wanapewaga milioni tatu kila mmoja na jeshi la polisi???
 
Na sio Nyamongo tuu, Mh. Tundu Lissu si jana wala juzi anafahamika Geita na Kahama vile vile kwasababu ya harakati zake za kutetea unyanyasaji na unyonyaji wa hawa wanoitwa "wawekezaji" . Way back, alikua maarufu kabla CHADEMA haijawa maarufu hivyo huko migodini. Hebu soma hapa:

http://www.miningwatch.ca/en/tanzan...eaking-out-against-world-bank-group-gold-mine
Je zile nazo zilikua siasa? Unafahamu kuwa wafiwa wa Tarime ndio waliomuomba akawasaidie kisheria baada ya kuona haki imepinda katika saga hili?
Wasomi wa kitanzania wananishangaza sana. Hata hawa wanaoona mchango wa CDM katika ishu nzima hii kuwa ni merely ya kisiasa,for the sake of it,wengi wao ni walewale WAKANDAMIZWAJI,WANYONYWAJI na WALIWAO!Wala sio wa-CANADA....ni watanzania tuu,tena wasomi! Inakera mnoo!
<br />
<br />
We makalio kweli,Tundu lisu amehangaika sana na nyamongo.na watu wanamjua sana nyamongo,sasa wewe cjui unachukulia tukio la jana ndo kisa? Kwanza hamna mkurya Mwenye MAWAZO LEGEVU kama yako. We umenunuliwa,af huna sifa za kukaa majukwaa kama haya mana maneno yako yanalijazia jukwaa nzi,na kama unavojua feni zimezima kutokana na mgao wa umeme kwaiyo ni vizuri ukalale au ukatafute gazeti la udaku usome.
 
Waachaneni wezi wawazike wezi wenzao CDM nendeni mkawazike wanamapinduzi wenu. Na hapa mtaani kwetu kuna vibaka wawili wamechomwa moto kuanzia mgongoni Mbowe na wenzako njooni muwazike wanatuharia hewa tu.
 
Wewe Mahesabu kuna siku moja utanyang'anywa mkeo na watoto harafu utaogopa kupigana kisa utaki kuitwa mwizi au Jambazi. Kupigania mali yako ni vita ya haki na Mungu atakuwa pamoja na watu wote wa aina hiyo. Ole wao waoga na wasaliti kama akina mahesabu.
 
Back
Top Bottom