Mazishi ya wanapinduzi wa Nyamongo, TARIME

Nyami2010

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
227
50
Wanajamii

Jana kupitia vyombo mbalimbali vya habari tumesikia na kuona kuwa miili ya wapiganaji wetu ilitelekezwa baada ya kuibiwa Motuary na polisi usiku wa kuamkia jana. Ni maajabu kwelikweli!

Kwa yeyote mwenye taarifa atujuze status ya miili hiyo. Mazishi yamefanyika?

Wapiganaji na wanapinduzi waliofariki ktk kisanga hiki..R.I.P:A S-rose:
 
Any loss of life is regrettable. Inabidi kufanyika uchunguzi kujua mazingira ambayo watu hawa walifariki. Je, walipigwa risasi wakiwa ndani ya eneo la Barrick? Je, polisi walikuwa na jinsi nyingine ya kuwazuia isipokuwa kuwapiga risasi? Je, ni kweli walipigwa risasi mgongoni wakati wanakimbia?

Pia tukumbuke kuwa ule ni mgodi wa dhahabu, hivyo lazima ulindwe kama inavyolindwa benki au kampuni yoyote yenye mali. Sasa watu kama walivamia ndani ya mgodi kwa lengo la kuiba gold ore na wakapigwa risasi napata ugumu kuwatetea na kuwaita "wanamapinduzi."
 
wezi waitwa wanamapinduzi......! siasa bwana!

Hivi kumbe Nyamongo ni mali ya Barrick?? Na je wana Nyamongo waende wapi? Hivi kweli naweza kuja leo katika kiwanja chako na kuweka uzio wa chuma na jeshi na kusema yaliyomo ni mali yangu. Ushindwe na Barrick yako!!
 
wezi waitwa wanamapinduzi......! siasa bwana!

Acha kukurupuka Mahesabu nani kakuambia waliouawa ni wezi? hivi unajua kila mtu ni "innocent" kabla mahakama haijatoa hukumu? kwa mtu smart ulitakiwa useme "watuhumiwa" kwa hii post yako mimi nahisi wewe ni mwenda wazimu lakini sitokuita mwenda wazimu mpaka ushahidi wa kitabibu utolewe. Any way nilikuwa nakukumbusha tuu uwe makini na maneno yako ipo siku utakuwa na la kujibu.
 
hivi kumbe nyamongo ni mali ya barrick?? Na je wana nyamongo waende wapi? Hivi kweli naweza kuja leo katika kiwanja chako na kuweka uzio wa chuma na jeshi na kusema yaliyomo ni mali yangu. Ushindwe na barrick yako!!

tumechoka kuonewa, tumechoka kuchezewa, sasa tunataka mapinduzi. Mapinduzi yatakayorudisha heshima ya mtanzania. Mtanzania amepewa nchi hii na mungu si makosa kuzaliwa nyamongo. Ni nani anayekuwa na raslimali ambazo haki ya kuzifurahia ni ya wageni? Wananyamongo na watanzania wana haki ya kufaidi keki ya raslimali za taifa. Kama serkali imeshindwa kulisimamia hilo wananchi wafanyeje?
 
Eti 'WANAMAPINDUZI',kumbe ukiiba ckuiz unakuwa mwanamapinduz?you must be kiddin'

wale walikuwa sio wezi, walitaka kufaidi au kurudisha japo asilimia 0.001 ya utajiri wetu ulioibiwa na kupewa wazungu wakigawana na ccm. kwa maneno mengine waliata "ku-redistribute un-equally distributed resources".

watu kama hawa ni wanamapinduzi for sure. we unadhani mwanamapinduzi ni nani?? nape au? we unadhani mapinduzi ni kumtoa makamba mkubwa na kumweka makamba mdogo???
 
Ni majambazi sio wanamapinduzi. hivi nyie hamuijui mara kwa ujambazi?
Acha utani na roho za watu,sheria ipi inasema wezi wapigwe risasi tena za mgongoni wakiondoka hapo ? Jambazi mwenye silaha atakimbia ? Kama walikuwa na silaha mbona hata polisi mmoja hajajeruhiwa ?
 
wezi waitwa wanamapinduzi......! siasa bwana!

ndugu zangu tuwe na utu,kama ni wezi mbona serikali inawagombea na kutaka kuzilipa maiti?someni taarifa ya uchunguzi wa maiti mgundue kuwa walionewa kwani maiti zote zimepigwa risasi kwa nyuma.uonevu wa serikali kwa raia.r.i.p.
 
Any loss of life is regrettable. Inabidi kufanyika uchunguzi kujua mazingira ambayo watu hawa walifariki. Je, walipigwa risasi wakiwa ndani ya eneo la Barrick? Je, polisi walikuwa na jinsi nyingine ya kuwazuia isipokuwa kuwapiga risasi? Je, ni kweli walipigwa risasi mgongoni wakati wanakimbia?

Pia tukumbuke kuwa ule ni mgodi wa dhahabu, hivyo lazima ulindwe kama inavyolindwa benki au kampuni yoyote yenye mali. Sasa watu kama walivamia ndani ya mgodi kwa lengo la kuiba gold ore na wakapigwa risasi napata ugumu kuwatetea na kuwaita "wanamapinduzi."

Taarifa za vyombo vya Dola zilisema walikuwa watu zaidi ya 800, katika hali ya kawaida hakuna majambazi wanoweza kufikia idadi kama hiyo, maana wataonekana hadharani ilhali majambazi wanatakiwa kujificha ili wasionekane. Ni kweli kwamba mgodi unatakiwa kulindwa kama mabenki au Kampuni yoyote yenye vito vya thamani. Lakini katika historia ya nchi yetu hakuna benki iliyowahi kuvamiwa na majambazi 800 au zaidi.

Kulingana na uelewa wangu hawa waliouwawa Nyamongo, ningeweza kuwaita wavamizi, lakini pia najiuliza kulikoni hadi watu 800 wavamie eneo ambalo wanafahamu kuwa lina ulinzi mkali? Kumbuka kuwa mgodi wa North Mara unalindwa na makundi mawili la kwanza ni Askari Polisi/FFU na la pili ni Askari wa Mgodi tena nao wana sila wanaoitwa "Mobile".

Nilipotafakari mambo yote hayo, nikaona kwamba hadi kufikia watu 800 kwenda kuvamia sehemu kama hiyo hata kama walitaka kuiba, maana yake ni kwamaba wamekata tamaa na wanaenda lolote liwe. Kwa maana nyingine ni kwamba wamefikia kikomo cha uvumilivu na hali ya eneo hilo, hivyo, wanahitaji kusikilizwa na mabadiliko kufanyika. KUFIKIA HAPO, NAMI NIKAWAITA WANAMAPINDUZI.
 
Back
Top Bottom