Dr. Nami sijawa jasiri kuwa wazi lakini siku itafika. Maana hata malaika wanaotusimamia hatuwaoni kwa macho ila kwa imani tu. Inauma sana unaposoma watu wasiojali maisha ya watu utadhani wataishi milele. Kejeli zinazotolewa zote zinaonesha kwamba Watanzania hatuna kitu kinachoitwa tanzia, bali ni wanyama kamili wasio na busara tuliyopewa na Mwenyezi Mungu. Nguruwe anaweza kumla nguruwe mwenzie hajui kuwa anakula nguruwe mwenzie. Sijaamini na sitaamini kuwa CHADEMA wanaweza wakatumia njia mbaya ya kutoa uhai wa watu kutaka uongozi. Japo simfahamu Judith lakini la moyoni, najisikia uchungu sana, sioni hamu ya kuitwa Mtanzania. Watu wengi wana imani na CHADEMA, nilipata moyo kusikia mbunge mmoja wa CCM aliyekiri kusikitishwa na haya na kusema kuwa haya yote yanasababishwa na watu wachache ambao hawataki kutoka madarakani kwa sababu ya uovu waliofawanyia watanzania. Poleni sana wana Arusha. Nakosa cha kuandika DR. Inauma sana. Inakera sana. Iliyoitwa Geneva imegeuzwa Machinjioni?