Mazda CX 5 inanifilisi!

Mambo yasiwe mengi kifupi wewe bado huna uwezo wa kumilia aina hiyo ya gari.
 
Ndo maana bongo gari inachukuliwa kama anasa
Nilikua na pick up Ford bantam iliua alternator nikakimbia dukani nikajua bei kubwa watasema 1m daah nikakutana na 2.5m na sehemu zingine 3m nikaacha gari nilipoenda SA niliikuta kwa rand 3500 kwa kipindi kile ilikua sawa na Tsh 500,000 tu na baadhi ya seal nilinunua Tsh 50,000 tu sawa na rand 300 zote bei niliyokua naambiwa Arusha ni vitu laki kadhaa utacheka uende kwenye parts za land cruiser huko ndio bei kichaa zipo huko..
 

Unakaaje na gari Miaka 10? Labda pickup au ya Biashara, lakini ya kutembelea ? Hapana
 
Pole Mkuu vifaa vya gari navyo vikiwa ghali ni msala. Hata kama gari ulipewa zawadi lazima uchechemee kama umekanya mav
๐Ÿ˜„ ๐Ÿคฃ kama tajiri aliempa mama yake mjengo mkubwa, ila mama alikuwa smart, akamwambia mwambia " Mwanangu nani ataihudumia na kulipia matengenezo?

Always waza kesho
 
Sasa hapo kosa au shida ni gari au ni wewe mzee? Yaani userereke uingie kwenye korongo paah gari ivunje taa useme shida ni gari?๐Ÿค”
Mkuu, jamaa kwenye uzi wake hajasema kuwa gari lina shida ila amesema linamfilisi kwa kuwa vipuri vyake na service ni vya gharama sana. Mfano hiyo service, ni kama amewatahadharisha wengine wataotaka kununua CX5, wajue wanachokiingia
 
Tofautisha UBOVU na KUFILISI. Sijazungumzia UBOVU Bali ughali wa vifaa vya CX 5 (Taa kubwa ya mbele 1.5m tofauti na gari nyingi za ukubwa zinazofanana)
Pole kwa changamoto mkuu. Wabongo hawasomi details labda mpake iwe ni mtihani๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„
 
Bado hujasema, kama gari ni 30 million plus umeweza kuilipia. Sioni ugumu wa wewe kuweza kuinunulia taa ya 1.5M
Chombo chochote cha moto huwaga akuna ugumu wa kuinunua hata kama ni pikipiki. Linapokuja sual la service ndio watu huchanganyikiwa.

Nmeletewa hapa quotation nataka badili drive belt, nmesema ngoja nimalize chai ndio nijibu text yake, vingine na hii asira plus njaa naweza mtukana fundi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ