HATIMAYE: Mazda CX-5 imeingia Top 5 ya gari zinazoingizwa Tanzania kutoka Japan

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
19,095
49,895
Wakuu.

Mapenzi ya Watanzania kwa SUV pendwa Mazda CX-5 yanazidi kujionesha kwa Mtandao maarufu wa kuingiza Magari kutoka Japan kuiweka katika magari 10 yanayoingizwa sana Tanzania na kushika namba 4.
Screenshot_20240310-135700.png

Bado Subaru Forester, tako la Nyani na IST wako mbele yake ila inaonesha jinsi gari mwaka 2024 na 2025 inaweka kua ni mwaka mzuri kwa Mazda kujazana Tanzania.

Huyu Mazda CX-5 mwenyewe ni diesel SkyActive cc 2,200 SUV anaenda kama CIF $5,000 na kuendelea. TRA utacheki mwenyewe kwa kuangalia mwaka.

Hii ni fursa nzuri kwa mafundi wa magari kuanza kujiandaa kupambana na engine ya diesel ya uyu mjamaa, pia waingiza vipuri na wazee wa decorations wachangamkie fursa.

Mazda ata perfom vizuri zaidi akisaidiwa na Mazda Verisa, Mazda 2 (demio), Mazda 3 (Axela) na Mazda 6 (Atenza) na mdogo wake CX5 bwana CX3.
 
Mwanangu nipo nae kariakoo anauza foresta yake ili avute hiyo mashine. Hii gari hata Mimi nimetokea kuipenda Sana

Ukiona mpaka foresta imeshika namba moja Tanzania ujue Hali imebadilika hasa Kwa wanazi wa Toyota, huwa nashangaa watu wa hapa jamiiforum wakiponda gari za kijerumani lkn ukiingia barabarani zimejaa kibao watu wanasukuma Tu....uwoga ni kitu kibaya sana maishani
 
Hiyo gari ya Mazda CX-5 ina kitu gani special kiasi cha kupanda chat ya kununuliwa kwa wingi kwa hivi sasa hapa Tanzania?
Diesel engine na interior design yake ni Noma hauwezi kuipata Kwa Toyota alafu ni 6 speed transmission huku Kwa gari kama harrier ni 4 speed transmission.
Mad Max huyu anaweza kuongezea nyama maana yeye anamiliki hii chuma
 
Mwanangu nipo nae kariakoo anauza foresta yake ili avute hiyo mashine. Hii gari hata Mimi nimetokea kuipenda Sana

Ukiona mpaka foresta imeshika namba moja Tanzania ujue Hali imebadilika hasa Kwa wanazi wa Toyota, huwa nashangaa watu wa hapa jamiiforum wakiponda gari za kijerumani lkn ukiingia barabarani zimejaa kibao watu wanasukuma Tu....uwoga ni kitu kibaya sana maishani
Kuna kipindi JF ukisema nataka kununua gari kila mtu anakuambia Carina Ti
 
Diesel engine na interior design yake ni Noma hauwezi kuipata Kwa Toyota alafu ni 6 speed transmission huku Kwa gari kama harrier ni 4 speed transmission.
Mad Max huyu anaweza kuongezea nyama maana yeye anamiliki hii chuma
Aisee.. Umegusa mule mule. Diesel pia advantage kwenye mafuta. Unakuta engine kubwa 2.2L ila ulaji wa wese friendly.
 
Mwanangu nipo nae kariakoo anauza foresta yake ili avute hiyo mashine. Hii gari hata Mimi nimetokea kuipenda Sana

Ukiona mpaka foresta imeshika namba moja Tanzania ujue Hali imebadilika hasa Kwa wanazi wa Toyota, huwa nashangaa watu wa hapa jamiiforum wakiponda gari za kijerumani lkn ukiingia barabarani zimejaa kibao watu wanasukuma Tu....uwoga ni kitu kibaya sana maishani
Kwny hio top 10 ya be forward hapo juu umeona gari za kijerumani ngapi?
 
Back
Top Bottom