Mazda CX 5 inanifilisi!

Mazda CX 5 inanifilisi!

Mwana jamii mwenzetu ,Connections amepata changamoto ya gari yake Mazda, tumpe maneno ya faraja , pia kata b ima kubwa ( Complihensive) ili ikulinde kwenye majanga haya
 
Toyota rav 4 third gen
Toyota vanguard
Toyota Kluger
Toyota prado 3rd gen
Subaru forester 3rd gen
Mitsubishi outlander
Suzuki vitara second gen?

Nataja ambayo yapo mjini kitambo sidhani kama kuna ambalo nimetaja hapo juu kuna taa inafika 1.5
Nasema haya maana kama unalalamika 1.5 ya taa basi hukupenda usumbufu huo wa taa bei hizo
Sasa kilichokufanya ununue gari inayotrend ni nini na unajua bei zinaenda na upepo?
 
1. Wakuu niliagiza Mazda CX 5 ya 2015, 2,200cc (diesel) August 2024 baada ya mwezi na nusu ikawa imeshafika bongo.

2. Nikajipinda nilkaitoa bandarini. Mziki umekuja kwenye kui-maintain daah msala. December nilienda nayo kijijini sasa kule Barabara zetu sio nzuri siku ikanyesha mvua tope kama lote barabaran kulazimisha kupita gari ikaserereka hadi kwenye mti puu taa ya upande wa dereva ikapasuka, kuulizia bei 1.5m TZS! Mpaka leo taa nimeunga na gundi.

3. Service natumia oil Castro 5w30 gharama za kila kitu service nayo kizunguzungu huna laki 7 hujafanya service.

Nipo safarini ila ndinga hii inanifikirisha sana.
Kuna uzi nilishauri mtu anunue kirikuu au vitz wakaniona mshamba😂
 
Atakutana na DPF, Oil Dilution, Overheating, Oil Pressure rise.. unapungua kilo 5 kwa mwezi
Nasikia zinapiga stick kwelikweli, kuna jamaa yangu amefanikiwa kui-offload na ameagiza 2.5 liter Petrol powered engine nadhani hapa ata enjoy sana
 
Mtoa mada ni muongo asiye na aibu.
Service ya laki 7 kwenye Mazda ni uongo kabisaa!!! Hiyo Castrol Oli unayotumia ni Aina gani? Kama kumwaga oil na kubadilisha filter haiwezi kufika laki 7 pia tofautisha Kati ya kufanya service na kufanya matengenezo
huyu hana gari hyo castol oil 5w30 ni 170,000 + FILTERS 50,000 hyo laki saba ameitoa wapi , then taa za CX5 hata laki 3 haifiki hz gari tunazo ni mwaka wa 3 sasa na majanga tunapata lakini sio kwa hizo gharama anazozitaja
 
Back
Top Bottom