Kocha anaweza kuwa na asilimia 30 ya mafanikio katika timu. Hamjawahi kuona kocha anatimuliwa au anaondoka katika timu moja kwa "kukosa mafanikio" lakini akienda timu nyengine inafanya vizuri? Wachezaji pia asilimia 30, katikakuonesha umahiri wao, kujituma, maelewano na kocha n.k. Asilimia zilobaki 40 zinategemea mambo mengi kutoka kwa viongozi na uongozi: kuongoza bila majungu na ubinafsi, kujali maslahi ya wafanyakazi, wakiwemo wachezaji, kutafuta vyanzo vya mapato/ufadhili.Kuanzia jana vyombo mbalimbali vya habari hapa nyumbani vimekuwa vikitoa taarifa ya Maximo kuonyesha nia ya kurudi tena kuifundisha Taifa Stars. Amekaririwa akilaumu utaratibu wa kuacha chipkizi nz kujumuisha wakongwe kwenye kikosi. Sasa swali, je huo ndio muarobaini wa tatizo lenyewe? Je, Maximo ni bora kuliko Paulsen? Je, mbona hatuzungumzii mfumo mzima wa uendeshaji wa soka letu kwa ujumla wake?
Nawasilisha......
Habari mbaya kwa kaseja hii...
Habari zilizonifikia zinasema kuwa serikali inahaha usiku na mchana kuvunja mkataba wa kocha Poulsen ili kutengeneza njia kwa ajili ya Maximo. Taarifa zinasema kuwa Waziri wa michezo Emmanuell Nchimbi amekuwa akifanya mawasiliano ya chini kwa chini na Corinthians, timu ambayo kwa sasa Marcio Maximo ni mshauri wa ufundi. Habari zimeendelea kulonga kuwa hata ziara ya Pinda Brazil ni kwa minajili ya shughuli hiyo hiyo. Haya yote yanatokea baada ya JK kugundua kuwa alipata umaarufu mkubwa baada ya kumleta Maximo lakini kwa sasa hana kitu kingine cha kumsaidia aondokane na kudharaulika zaidi ya michezo.
Hatumtaki! Ila kwa nchi hii ilivyokuwa na viongozi hamnazo sitashangaa kuona amerudi.
Hiyo World Cup ya 2015 labda ya mchezo wa kiduku,Brazili wanaandaa World Cup ya mpira wa mguu (football) mwaka 2014Ni kwa sababu za kisiasa zaidi. Ikumbukwe kuwa hakuna mtaji mwingine wa kuisaidia CCM 2015 zaidi ya Taifa Stars kufuzu kwa World Cup 2015 Brazil wakijua kuwa wapiga kura wengi ni vijana na kwahiyo ni wapenda soka.
Ni kwa sababu za kisiasa zaidi. Ikumbukwe kuwa hakuna mtaji mwingine wa kuisaidia CCM 2015 zaidi ya Taifa Stars kufuzu kwa World Cup 2015 Brazil wakijua kuwa wapiga kura wengi ni vijana na kwahiyo ni wapenda soka.