Timu yaTaifa ya Soka ya Tz (Taifa Stars) ni JIPU. - Tuige Mfano wa Uganda (The Crens)

gasto genaro

JF-Expert Member
Oct 15, 2014
780
554
Salaam wakuu,
Karibu tena katika chambuzi za mchezo huu adhimu wa Soka. Na leo, Tutaizungumzia Timu ya soka ya taifa ya Tanzania inayoenda kwa jina la Taifa Stars.

Kama umekua ni mfuatiliaji mzuri wa soka, hususani Timu za Taifa, ni dhahiri shahiri kuwa, unafahamu kiundani mwenendo wa timu yetu ya taifa ya soka - Taifa Stars.

Taifa Stars imekua na muendelezo wa matokeo mabovu mno kwa miaka miwili iliyopita, na katika miaka miwili hiyo, Stars haijashinda hata game 10 kati ya zote ilizocheza.

Ubovu huu wa timu ya Taifa, ni unasababishwa na sababu lukuki.

Kwanza uongozi mbovu wa TFF. Tangu Jamal Malinzi apewe mamlaka ya kuiongoza TFF, ndipo hapo hapo timu ya taifa imekua ikipiga hatua moja mbele na kurudi tano nyuma. Uongozi wa Malinzi hauna policies (sera) nzuri wala mikakati mizuri yenye tija ya kuiinua timu ya Taifa.

Tumeona Jamal Malinzi alipoingia tu madarakani, Alimfukuza kazi aliyekua kocha mkuu wa Timu ya Taifa wakati huo Kim Paulsen bila sababu yoyote wakati timu angalau ilikua ina mwelekeo. Kim ambaye wamemrudisha kisiri siri kuinoa Serengeti boys ambayo inafanya vizuri. Katika uongozi huu wa malinzi, tumeona timu ya taifa kutojiandaa kwa muda wa kutosha na kwenda kucheza mechi ya kimataifa!.

Jamal Malinzi pia ameonesha dhahiri kuwa haegemei sana kwenye TFF kwa ujumla bali klabu yake penzi YANGA. Jamal Malinzi amekua aki tweet hata Table za VPL zenye leble za Yanga. Kwa namna hii, huyu hawezi kuwa na uchungu na Timu ya Taifa.

Pili, wachezaji wanakosa motivation. Kimsingi, wachezaji wa soka ukiwapa motivation, ni lazima watapigana zaidi kushinda. Wachezaji wanapokosa motisha, basi nao pia watacheza as they are playing for nothing.

Tatu, wachezaji wenyewe kutokujituma. Kuna baadhi ya games za taifa stars, wachezaji hawajitumi na wala hawaoneshi ule uzalendo... Hence, negative results..

Serikali pia kwa kutoruhusu uraia wa nchi mbili, kunaigharimu timu ya taifa. Hii ni kutokana na ukweli kua, kuna wachezaji wengi wa soka wenye asili ya kitanzania, ambao wapo ughaibuni ila, wanashindwa kuja kuichezea Stars kutokana na sheria za nchi yetu kubana. Hii ingebadilishwa, basi ingesaidia kuiinua timu yetu ya taifa ya soka.

Kutokuwekeza pia katika soka la Vijana pia kunaiathiri Stars. Tumeona dhahiri katika nchi zilizoendelea kisoka hapa Africa kama Ghana, Ivory Coast, Nigeria and the likes, zimewekeza katika soka la vijana weny umri mdogo. Kelechi Iheanacho, Alex Iwobi, Onyinye Ndidi (Nigeria), Eric Bailly (Ivory Coast), Sadio Mane(Senegal).. Hawa wote ni under 22 waliokwisha kuwa mastaa wakubwa wa soka. Lakini tukija katika soka letu Tz, sithani kama kuna mchezaji wa Timu ya Taifa mwenye umri wa hata miaka 26 ambaye anafikia kiwango cha Kelechi Iheanacho wa Manchester city na Nigeria. Hivyo soka la vijana ni lina mchango wa 95% ktk kulikuza soka letu kama tukiwa serious.

Kimsingi nisiandike sana maana maneno hayatoisha.

Tuige Mfano wa Timu ya taifa ya Uganda (The Crens)

Katika miaka mitano au minne iliyopita, Taifa Stars ilikua ni timu bora ya taifa Africa Mashabiki. Lakini leo hii, stars inapitwa hadi na Rwanda.. Seriously?

Timu ya Uganda pia ilikua nyuma yetu ila, kwasasa ipo mbele yetu mara 1000.

Uganda imefuzu kucheza AFCON , michuano itakayoanza January 14 mwaka huu. Uganda pia imeshinda tuzo ya timu bora ya taifa ya mwaka 2016. Huu ni mfano wa kuigwa mno. Kimsingi soka la Tz halina uvumilivu! Kuanzia klabu hadi timu ya taifa. Tukumbuke kuwa, kocha anayeinoa Uganda (Michu) , ni alifukuzwa na Yanga miaka ya nyuma. Stars ilikua na mwelekeo enzi za Maximo ambaye alitimuliwa kwa sababu ya kutowaita wachezaji waliokua na utovu wa Nidhamu kama Juma Kaseja na Haruna Moshi 'Boban'. Endapo kama tungemvumilia Maximo, hakika tungekua mbali kwa sasa. Uganda wamemmvumilia Michu, na sasa matunda wameyaona.

Ifike pahala tutambue kuwa, soka sio tukio la kukurupuka, ni maandalizi ya muda mrefu.

Ukitizama ligi ya VPL, ni ligi yenye mvuto zaid Africa Mashabiki,. Wachezaji wengi Africa Mashabiki hutamani kuja kucheza soka hapa hususani ktk timu za Simba na Yanga. Tutumie hilo ktk kukuza timu yetu ya taifa.

Uganda inaundwa na wachezaji waliolelewa na VPL na kupikwa wakaiva.. Kama vile Juuko Murshid na Hamis Kiiza.. Hii inadhihirisha kuwa tunaweza pia ligi yetu ina uwezo mkubwa wa Kutengeneza timu imara ya taifa.

Nimalizie kwa kusema kwamba, pamoja na sababu za udhaifu wa timu yetu ya taifa ya soka kuwa nyingi, sababu kubwa kabisa ni ubovu wa TFF. Tff ikipata uongozi imara wanaojua soka, basi haya matatizo mengine yanaisha automatically..

________________________________

Genaro..
 
Mkuu hadi leo bado unaifatilia hiyo taifa starz???? Soka la bongo "miyeyusho", wenzio tulihamia epl zamani sana. Soka la bongo "pasua".
 
kina iwobi wamewekezwa na wazazi wao, sisi watoto wetu tunawaandaa kuwa maprofesa, hivi kina mengi hawana watoto wakawapeleka kwenye academy hizo za barcelona?
 
wakuu nimecheka sana hiyo michango yenu,utasikia mimi sijaribiwa!!ningeandika mengi lakini!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom