Embu tuongee kidogo kuhusu Taifa Stars ya Kim | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Embu tuongee kidogo kuhusu Taifa Stars ya Kim

Discussion in 'Sports' started by Anselm, Jun 1, 2012.

 1. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ngoja leo nisiwaongelee kabisa Watani zangu,
  Leo tuweke unazi pembeni,tuongee kidogo kuhusiana na team yetu ya Taifa, Taifa Stars ambayo kesho tarehe 2 itateremka dimbani Jijini Abidjan kumenyana na Tembo wa Ivory Coast katika mchezo wa kundi C kutafuta ticket ya kushiriki Kombe la Dunia.
  Lazima niseme kati ya makocha wote waliowahi kuifundisha team ya Taifa ya Tanzania ni imani yangu kuwa Kocha wa sasa Kim Paulsen ndo "Kilaza" kuliko makocha wote waliowahi kupita pale,sijui TFF walivutiwa na nini mpaka wakamwajiri kwanza kuifundisha Ngorongoro Herois na baadaye kumkabidhi team ya wakubwa akimrithi m'denmark mwenzake Jan. Niliwahi kusema hapa na leo ninarudia tena nina mashaka makubwa sana na uwezo hasa unaotokana na taaluma ya fani hii ya soka wa Kim, ndo nagundua kuwa kuna kosa kubwa sana limetendeka katika kumkabidhi team hii ya Taifa ambayo ndo inabeba taswira nzima ya uwezo wetu kama nchi katika mchezo huo,nafikiri kama mustakabali wa kupata kocha mzuri ulikuwa unaonekana kuchukua muda mrefu ni afadhali tungemuacha Jan amalizie kipindi chake kuliko kumkabidhi huyu Bogas jukumu hilo,kwanza ingeepusha gharama ambazo TFF ipo njiani kuingia kwa kukatisha mkataba wake.
  .....labda nitasikia kutoka kwa wapenda soka wengine hapa lkn mimi binafsi sijawahi kuona kocha anachagua team ya Taifa let's say wachezaji 25 halafu all of the sudden wachezaji wa'4 tena wa kikosi cha kwanza na experienced wana'fall katika Majeruhi then kocha pasipo kufanya replacement zozote anabeba waliosalia na kwenda kucheza mechi dhidi ya 1 ya team ngumu kabisa Africa kirahisirahisi namna hiyo, Kocha gani anashindwa hata kuangalia wenzake kutoka kule barani kwake wanavyofanya kazi,leo hii nimesoma kwenye mtandao kuwa baada ya kuona Frank Lampard amepatwa na majeruhi tayari kocha wa team ya Taifa ya England ameshamuita kiuongo wa liverpool tena ambaye hakuwa na msimu mzuri mwaka huu Jordan Henderson kuziba pengo lake,sasa inakuwaje Kim awakose Ulimwengu,Boban,Nurdin na Cholo halafu bila kuchukua tahadhari yeyote,hivi kweli kina Toure,Kalou,Gervinho,Drogba na wengineo ni wa kuwabebea kina Msuva,Domayo na Jonas Mkude?
  Sikatai soka hujengwa na msingi wa soka la vijana lkn kama yeye ni mfuasi mzuri wa watoto kwanini asingeomba basi akabaki kule team ya watoto tukajua 1 kuwa anatuandalia team yenye akili ya baadaye,after all amekaa kule si chini ya miaka mi'2 amefanya nini na hao watoto wake katika mashindano waliyoshiriki?,hivi kweli kama kina Domayo walishindwa kufanya la maana kwenye mashindano yanayoshirikisha watoto wenzao ndo wataweza kwa kina Drogba kweli?
  Kwa mtazamo wangu watanzania sasa inabidi tuamke,tuache kuigeuza nchi yetu kuwa ni dumping area,kuchukua magarasa na kuwafanya ma'expert tunataka watusaidie kunua soka letu,Kim kwangu mimi ni kama walivyo Mwape,Asamoah,Sunzu,Kago na wengineo....Magalasa yasiyostahili kulipwa hata Tshs 100,000/= kama mshahara fedha za kitanzania achilia mbali hayo madollar wanayolipwa.
  Naweza ku'bet humu tena kwa pesa nyingi tu kuwa chini ya Kim na kwa style hizi alizoanza nazo hatuwezi kufika popote,labda abadilike otherwise tutafungwa na kufungwa na kufungwa mpaka tuchukie soka,yangu macho.

  Nawasilisha.
   
 2. leroy

  leroy JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 60
  ​Mimi niliachaga siku nyingi kuongelea soka la, Bongo...
   
 3. N

  Newvision JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe si mtaalamu au niambie unajua nini zaidi katika soka zaidi ya haya unayoongea. Hawa jamaa hufanya mambo kisayansi na utaona tunakokwenda
   
 4. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Umeona wamefungwa 2-0 na Ivory Coast waliojikusanya siku 1 nyuma umepata kiburi cha kuongea siyo?,ngoja nikuulize hivi kuchagua wachezaji kwa lengo la kuwatumia kwenye mechi muhimu ghafla wachezaji wa'nne wa kikosi cha kwanza wana'fall majeruhi nafasi zao hazizibwi nalo linahitaji PHD ya soka kujua kwamba haikuwa wise?,nyie ndo wale as long as mmeona ni Mzungu basi mnafikiria Mzungu hakosei,mtaolewa....shauri yenu,nyie washobokieni tu hao Wazee,watu wenyewe wamekuja huku bila familia(wake) zao.
   
Loading...