Maximo aomba kurudi Stars

Mrimi

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,691
633
Kuanzia jana vyombo mbalimbali vya habari hapa nyumbani vimekuwa vikitoa taarifa ya Maximo kuonyesha nia ya kurudi tena kuifundisha Taifa Stars. Amekaririwa akilaumu utaratibu wa kuacha chipkizi nz kujumuisha wakongwe kwenye kikosi. Sasa swali, je huo ndio muarobaini wa tatizo lenyewe? Je, Maximo ni bora kuliko Paulsen? Je, mbona hatuzungumzii mfumo mzima wa uendeshaji wa soka letu kwa ujumla wake?

Nawasilisha......
 
mkuu mbona umerudia cheki uzi wa morocco vs tanzania utaiona hii ishu..
 
Kuanzia jana vyombo mbalimbali vya habari hapa nyumbani vimekuwa vikitoa taarifa ya Maximo kuonyesha nia ya kurudi tena kuifundisha Taifa Stars. Amekaririwa akilaumu utaratibu wa kuacha chipkizi nz kujumuisha wakongwe kwenye kikosi. Sasa swali, je huo ndio muarobaini wa tatizo lenyewe? Je, Maximo ni bora kuliko Paulsen? Je, mbona hatuzungumzii mfumo mzima wa uendeshaji wa soka letu kwa ujumla wake?

Nawasilisha......
Kocha anaweza kuwa na asilimia 30 ya mafanikio katika timu. Hamjawahi kuona kocha anatimuliwa au anaondoka katika timu moja kwa "kukosa mafanikio" lakini akienda timu nyengine inafanya vizuri? Wachezaji pia asilimia 30, katikakuonesha umahiri wao, kujituma, maelewano na kocha n.k. Asilimia zilobaki 40 zinategemea mambo mengi kutoka kwa viongozi na uongozi: kuongoza bila majungu na ubinafsi, kujali maslahi ya wafanyakazi, wakiwemo wachezaji, kutafuta vyanzo vya mapato/ufadhili.

Kwa ufupi, Tanzania hata akaja Maurinho, Fugerson, Maradona, Guardiola, Cruyff...orodha haishi, bado tutaendelea kupiga kwata katika maendeleo ya soka kwa sababu asilimia 70 ya uwezo imo mikononi mwetu na hatutaki kujinasua.

Udaku tu: Wazanzibari huwa wanakula urojo na mbirimbi ndio wakawa "laini", hivi Watanzania wote tunakula nini? Isijekuwa vyakula vyetu ndio sababu ya utepwetepwe wa wachezaji wetu?
 
Habari zilizonifikia zinasema kuwa serikali inahaha usiku na mchana kuvunja mkataba wa kocha Poulsen ili kutengeneza njia kwa ajili ya Maximo. Taarifa zinasema kuwa Waziri wa michezo Emmanuell Nchimbi amekuwa akifanya mawasiliano ya chini kwa chini na Corinthians, timu ambayo kwa sasa Marcio Maximo ni mshauri wa ufundi. Habari zimeendelea kulonga kuwa hata ziara ya Pinda Brazil ni kwa minajili ya shughuli hiyo hiyo. Haya yote yanatokea baada ya JK kugundua kuwa alipata umaarufu mkubwa baada ya kumleta Maximo lakini kwa sasa hana kitu kingine cha kumsaidia aondokane na kudharaulika zaidi ya michezo.
 
yeah jamaa alikuwa fine ila ila ya kuingia kwenye bongo muvi ndio ilimshushia stim kwa wabongo
 
Habari zilizonifikia zinasema kuwa serikali inahaha usiku na mchana kuvunja mkataba wa kocha Poulsen ili kutengeneza njia kwa ajili ya Maximo. Taarifa zinasema kuwa Waziri wa michezo Emmanuell Nchimbi amekuwa akifanya mawasiliano ya chini kwa chini na Corinthians, timu ambayo kwa sasa Marcio Maximo ni mshauri wa ufundi. Habari zimeendelea kulonga kuwa hata ziara ya Pinda Brazil ni kwa minajili ya shughuli hiyo hiyo. Haya yote yanatokea baada ya JK kugundua kuwa alipata umaarufu mkubwa baada ya kumleta Maximo lakini kwa sasa hana kitu kingine cha kumsaidia aondokane na kudharaulika zaidi ya michezo.

Afadhali strategy hii (michezo) huwa inatuunganisha...kuliko ile nyingine ile sijui ya 'udini', ilikuwa inatuchonganisha! Au Mwita ndio unataka kukusanya maoni hapa JF ukamshauri mheshimiwa 'atoke vipi'?
 
pinda na maximo.jpg

inawezekana ni ukweli na picha yao ni hiyo hapo.
 
Hatumtaki! Ila kwa nchi hii ilivyokuwa na viongozi hamnazo sitashangaa kuona amerudi.
 
View attachment 38776

inawezekana ni ukweli na picha yao ni hiyo hapo.

Asante Mamdenyi, kuna taarifa kuwa Pinda amefikia hoteli ambayo iko nyuma ya Hoteli anayoishi Maximo. Isitoshe nasikia Maximo ndiye aliyeratibu (na Waziri wa Kilimo wa Brazil) juu ya ziara ya Pinda ingawa (Maximo) si mtu wa Serikali. Kitu ambacho kimeleta utata mkubwa kwa serikali ya Dilma Rousselff kutoka kwa wapinzani.
 
Hatumtaki! Ila kwa nchi hii ilivyokuwa na viongozi hamnazo sitashangaa kuona amerudi.

Ni kwa sababu za kisiasa zaidi. Ikumbukwe kuwa hakuna mtaji mwingine wa kuisaidia CCM 2015 zaidi ya Taifa Stars kufuzu kwa World Cup 2015 Brazil wakijua kuwa wapiga kura wengi ni vijana na kwahiyo ni wapenda soka.
 
Hiyo World Cup ya 2015 labda ya mchezo wa kiduku,Brazili wanaandaa World Cup ya mpira wa mguu (football) mwaka 2014
 
Ni kwa sababu za kisiasa zaidi. Ikumbukwe kuwa hakuna mtaji mwingine wa kuisaidia CCM 2015 zaidi ya Taifa Stars kufuzu kwa World Cup 2015 Brazil wakijua kuwa wapiga kura wengi ni vijana na kwahiyo ni wapenda soka.

ha ha! Tanzania Kufuzu world cup, hilo kamwe halitawezekana hata akija morinho.
 
It is too late,timu isambaratike halafu ndo wafikirie kumrudisha,morali ya mpira imeshaisha kwa wachezaji na washabiki na ule moyo wa utaifa kwa washabiki na wapenzi wa mpira umeshapote tena,sasa hilo hata kama ni kweli sina hope kwamba litakuwa na positive outcome,it is too late wandugu.
 
Leodgar Tenga kazi imeshamsinda,alianza vizuri sasa naona kazi imemshinda nafikiri tunahitaji kiongozi mpya TFF
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom