Mawio newspaper permanently banned with effect from January 15th, 2016

Hili ndio tatizo la magufuli kuchagua wanasiasa kwenye baraza lake,wakati yeye anajigamba sio mwanansiasa..

Nape hawezi kubadilika,ameshazoea sifa za kipuuzi na ubabe wa kitoto..
 
Sioni ajabu kwasababu huyu anasumbuliwa na ushabiki na ukada wa chama chake kuliko maslahi mapana ya wananchi wote.Inafaa arudishwe kwenye chama akafanye propaganda
Tena apewe kitengo cha propaganda.
 
Nape anasahau kua kuna Mwanahalisi? Hajafanya lolote hapo
 
Hata hao mwanahalisi wakiandika habari za kipashkuna na wao watafungiwa vile vile. Maadili ya kazi yapo, ukijifanya una kiburi unakutana na mkono wa serikali ambao una kiburi mara mia moja kukuzidi. Ukanjanja wa habari hauwezi kudumu, watu wanataka professionalism ionekane ikifanya kazi.
 
Habari kwenu wakuu

Lile gazeti chochezi la saed kubenea , mzee wa elimu ya hapa na pale aliyesoma vyuo vya hapa na pale lafungiwa rasmi Jana 15/01/2015
Ushahidi huu hapa
kubenea ni mbunge tu, nape ni mbunge na ni waziri, tupe kiwango chake cha elimu!
 
SERIKALI YALIFUTA GAZETI LA MAWIO

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kulifuta kutoka katika Daftari la usajili wa magazeti, gazeti lijulikanalo kama MAWIO?. Amri ya kulifuta Gazeti hilo imetolewa kwa Tangazo la Serikali Na. 55 lililotolewa tarehe 15 Januari, 2016. Uamuzi huo umetolewa kwa mjibu wa Sheria ya Magazeti Sura ya 229, kifungu 25(1).

Hatua hii pia inazuia gazeti la Mawio kuchapishwa katika njia nyingine yoyote ikiwa ni pamoja na mitandao (Online publication) kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta Sura ya 306.

Serikali kwa masikitiko makubwa, imechukua uamuzi huu kutokana na mwenendo wa uandishi wa gazeti hilo usioridhisha wa kuandika na kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na kuhatarisha amani, utulivu na usalama wa nchi yetu.

Aidha, hatua hii ya kulifuta gazeti hilo imechukuliwa baada ya Msajili wa Magazeti kufanya juhudi kubwa za muda mrefu kuanzia Juni, 2013 hadi Januari, 2016 kumtaka Mhariri wa gazeti hilo kubadili aina ya uandishi wa habari na makala katika gazeti lake, bila mafanikio.

#Msajili wa magazeti kwa juhudi zake alifanya mawasiliano na mhariri wa gazeti hilo mara nane kwa lengo la kutaka afanye marekebisho ya mtindo wa kutoa habari zake lakini mhariri wa gazeti hilo hakuzingatia ushauri mzuri aliopewa na Msajili wa Magazeti.

Ninatoa wito kwa wamiliki, wahariri, waandishi na watangazaji wa habari kuzingatia sheria, Kanuni na taratibu za taaluma ya uandishi wa habari ambazo zikizingatiwa hakutakuwa na migogoro yoyote. Aidha Serikali inasisitiza kwamba inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari unaozingatia maadili, weledi na Sheria za nchi na kwamba Serikali itaendelea kushirikiana navyo

#Kwa upande mwingine ninatoa pongezi kwa vyombo vyote vya habari nchini vinavyozingatia maadili, weledi na Sheria zinazosimamia taaluma ya habari na sheria nyingine za nchi. Kwa namna ya pekee Serikali inawapongeza wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari ambavyo vinapofanya makosa vikielekezwa hujirekebisha na kutoa ushirikiano kwa Serikali na pia kubadili mwenendo wao; hawa ni pamoja na wahariri wa magazeti ya;

Mwananchi Tanzania
Mtanzania
The East African
Magazeti ya Daily News na Habari Leo
Uhuru na mengineyo

Ninapenda kusisitiza kwamba Serikali inapenda kujenga uhusiano mzuri na wa kirafiki kati yake na wadau wa sekta ya habari. Aidha ninasisitiza tena wadau wa sekta hii kuzingatia Sheria ili kujenga heshima ya tasnia ya habari na kulinda amani ya nchi yetu.

MWISHO

Imetolewa na
Nape M. Nnauye, |MB|-
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Dar es Salaam, leo tar, 17 January, 2016
 
Wanachama Wa chadema wanafiki sana hawataki kuambiwa ukweli.

Yani hawaoni makosa ya chama chao ,Nyumbu wanaona makosa ya vyama vingine tu.

Huu upuuzi Wa kulindana haukubaliki dunia ya Leo ukweli lzm usemwe..

Mbowe kila siku anapiga dili lkn chama hata kujenga ofisi tu wameshindwa
 
Tatizo letu Watanzania tumeendekeza sana siasa hadi kwenye vitu serious, tukiambiwa ukweli tunaanza kusema u-CCM na u-CHADEMA. Ila yakitutokea kama mauaji ya Kimbali ndo tunaweza kujifunza.
 
SERIKALI YALIFUTA GAZETI LA MAWIO

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kulifuta kutoka katika Daftari la usajili wa magazeti, gazeti lijulikanalo kama MAWIO?. Amri ya kulifuta Gazeti hilo imetolewa kwa Tangazo la Serikali Na. 55 lililotolewa tarehe 15 Januari, 2016. Uamuzi huo umetolewa kwa mjibu wa Sheria ya Magazeti Sura ya 229, kifungu 25(1).

Hatua hii pia inazuia gazeti la Mawio kuchapishwa katika njia nyingine yoyote ikiwa ni pamoja na mitandao (Online publication) kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta Sura ya 306.

Serikali kwa masikitiko makubwa, imechukua uamuzi huu kutokana na mwenendo wa uandishi wa gazeti hilo usioridhisha wa kuandika na kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na kuhatarisha amani, utulivu na usalama wa nchi yetu.

Aidha, hatua hii ya kulifuta gazeti hilo imechukuliwa baada ya Msajili wa Magazeti kufanya juhudi kubwa za muda mrefu kuanzia Juni, 2013 hadi Januari, 2016 kumtaka Mhariri wa gazeti hilo kubadili aina ya uandishi wa habari na makala katika gazeti lake, bila mafanikio.

#Msajili wa magazeti kwa juhudi zake alifanya mawasiliano na mhariri wa gazeti hilo mara nane kwa lengo la kutaka afanye marekebisho ya mtindo wa kutoa habari zake lakini mhariri wa gazeti hilo hakuzingatia ushauri mzuri aliopewa na Msajili wa Magazeti.

Ninatoa wito kwa wamiliki, wahariri, waandishi na watangazaji wa habari kuzingatia sheria, Kanuni na taratibu za taaluma ya uandishi wa habari ambazo zikizingatiwa hakutakuwa na migogoro yoyote. Aidha Serikali inasisitiza kwamba inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari unaozingatia maadili, weledi na Sheria za nchi na kwamba Serikali itaendelea kushirikiana navyo

#Kwa upande mwingine ninatoa pongezi kwa vyombo vyote vya habari nchini vinavyozingatia maadili, weledi na Sheria zinazosimamia taaluma ya habari na sheria nyingine za nchi. Kwa namna ya pekee Serikali inawapongeza wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari ambavyo vinapofanya makosa vikielekezwa hujirekebisha na kutoa ushirikiano kwa Serikali na pia kubadili mwenendo wao; hawa ni pamoja na wahariri wa magazeti ya;

Mwananchi Tanzania
Mtanzania
The East African
Magazeti ya Daily News na Habari Leo
Uhuru na mengineyo

Ninapenda kusisitiza kwamba Serikali inapenda kujenga uhusiano mzuri na wa kirafiki kati yake na wadau wa sekta ya habari. Aidha ninasisitiza tena wadau wa sekta hii kuzingatia Sheria ili kujenga heshima ya tasnia ya habari na kulinda amani ya nchi yetu.

MWISHO

Imetolewa na
Nape M. Nnauye, |MB|-
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Dar es Salaam, leo tar, 17 January, 2016

ALIYEKUTANGULIA ALIFUTA GAZETI LA MWANAHALISI MATOKEO YAKE SERIKALI INATAKIWA ILIPE FIDIA YA BILIONI ZA TSHS
SERIKALI HAIJAFUTA BALI NAPE NA ITIKADI ZAKE ZA CHAMA ILA UNATAKA KUINGIZA SERIKALI KWENYE HASARA TU
 
Kubenea bado anadhani ni utawala wa kikwete huu

asipoangalia na kubadilika hata mwanahalisi litapigwa tena chini, atabaki kushinda mahakamani
 
Kwani mushinda mahakamani kwenye utawala WA mh magufuli ni kosa?
 
Yaani kulifungia hilo gazeti kisa ni kuweka picha ya Rz1 akifungwa kamba za viatu na Makonda au kuna jingine?
Hivi kuna ubaya gani kuweka picha ambayo ni halisi hiyo picha siya kutengeneza ni halisi
 
Back
Top Bottom