Mawaziri wanane watakiwa kung'oka...!

Mawaziri wanane watakiwa kung'oka...!

samahani sana ngereja..umeprove failure toka mwanzo wala usilet ubishi wa kutka kukataa kuachia ngazi..
 
Waziri Mkuu anaondoka katika Mazingira Tatanishi licha ya kuwaita kwa nguvu waandishi wa vyombo mbalimbali ambao walitegemea angetoa Tamko kuhusiana na maamuzi mazito ambayo tayari yamekwishazungumzwa hapa JF, Bahati mbaya sasa anatoka yeye kupitia mlango wa uani na muda mfupi kidogo anatoka Jenista Mhagama na yeye anapotakiwa kutoa Tamko kama ilivyoagizwa awali anasema maelezo yote atayatoa mwenyekiti wao Waziri Mkuu ambaye kisha chepuka kama dk 15 zilizopita.

  1. Kimejiri Nini hakuna anayejua
  2. Atatangaza kesho asubuhi katika Bunge, Inaelekea hii ndo plan ili wasipre-empty kikao cha Bunge
  3. Au wanasubiri baraka za Vasco Da Gama, hakuna anayejua
Ila kwa kauli ya Jenista Mhagama Mawaziri saba wameamuriwa Kujiuzuru mara moja nyadhifa zao....Nakamata detail za mwisho kabla sijaondoka niwajuze wanajamvi

Kwa sasa hayo ndo yanajiri kutoka viwanja vya Bunge

Adios
 
Lukuvi kakataa kuzungumza, anasema taarifa itatolewa na katibu wa magamba, waandishi wanasubiri. Na sisi wapenda nchi tunasubiri popote tulipo hakuna kulala.

I hate this... I really hate this...I really really hate this! Itakuwaje taarifa ya kujiuzulu kwa kiongozi ndani ya serikali tena waziri aliyeteuliwa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano, itolewe na katibu wa magamba? Kwanza kwa nini wapewe heshima hiyo ya kujiuzulu badala ya kufukuzwa? Au ni yale yale ya kuvuana magamba CCM, eti watu wakajipime kwanza! Watanzania, nafikiri tuna tatizo kubwa kuliko tunavyofikiria na tusipoangalia tunaelekea kuzama kwenye deep deep shit, OMG! mchezo gani huu? Sasa hawa kama wanajiuzulu, then what!...aliyewateua je? ...na hao watakaochukua nafasi zao watateuliwa na nani?...watatoka wapi au humo humo kwenye dampo? Yaani wale wale waliokuwa wakiipigia kelele serikali lakini wakaogopa kumwaga sahihi zao jana ndio wawe wakombozi wa taifa hili? Hii ni zaidi ya ushenzi, Goddamn!
 
ITV/TBC1/Radio One/TBC Fm zote zinaendelea na vipindi vya ajabu tu! Hivi hii habari mpasuko imetoka wapi??
 
lete habari wakuu bado watu hatujalala. waliosombwa na gharika ya Zito ni akina nani?
 
Way to go, wakubwa walisema lisemwalo lipo kama lipo....
 
Siku ya leo imekuwa kama tarehe 01/04,semeni basi kitu cha uhakika ama kuna kukesha wengine hamjatujulisha.
 
pinda hana sababu ya kuendela kuwa wazir mkuu kama kundi kubwa hii linajiuzuru...wizara zote zimejaa majizi tu ..waondoke
 
hapa mavuvuzela akina Nape na Mukama wataanza kujisifu kwamba wamevua magamba, kumbe bado saana

CDM wawe smart zaidi, waongeze chumvi kwamba walio jiuzulu wafikishwe mahakamani na wafilisiwe.

Pia mkutano wa hadhara na kuweka thamani ya hela walizoiba, ili tuendelee kuwadai CCM na kuichimbia kaburi kabisa ifikapo 2015.

Wananchi tusilale, M4C iendelee kuwadai mawaziri hawa waliojiuzulu na Mkuu mwenyewe warudishe mali za watanzania
 
Hivi Dr Mponda anajisikiaje wakati huu maana madokta waliposema ajiuzulu watu wakasema anaonewa sasa kauli inatoka kwa wanasiasa wenzie na tuhuma nzito nzito za ubadhilifu wa mabilioni ya fedha ndani ya wizara yake ambayo madokta hawakusema nadhani atumie busara this time ajiuzulu mwenyewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom