Mawaziri waliopita wa viwanda na biashara leo wamekiri Bungeni kuwa walishindwa kufufua viwanda

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
Dodoma.

Mawaziri wa zamani wa viwanda na biashara leo Jumatano Juni 23, 2021 wamekiri Bungeni mjini Dodoma kuwa walishindwa kufufua viwanda.

Charles Mwijage ambaye ni mbunge wa Muleba Kaskazini na Joseph Kakunda (Sikonge) kwa nyakati tofauti wamewahi kuwa mawaziri wa wizara hiyo katika uongozi wa Serikali ya awamu ya tano.

Mwijage akichangia hotuba ya muswada wa fedha ameitaka Serikali kuachana na mpango wa kufufua viwanda kwani yeye alivishindwa.

"Mpango wa kufufua viwanda achaneni nao fikirieni vitu vipya, mimi nilijaribu katika wakati wangu lakini nilishindwa kwa hiyo msipoteze muda kufikiria ufufuaji wa viwanda," amesema Mwijage.

Wakati Mwijage akiendelea kuchangia, alisimama Kakunda kwa ajili ya kumpa taarifa ambapo mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu alimpa nafasi ya kuzungumza.

" Mwenyekiti nampa taarifa mzungumzaji (Mwijage) kuwa hata mimi nilijaribu kufufua kiwanda kule Lindi lakini nilishindwa, kwa hiyo mchango wake ni sahihi kabisa," amesema Kakunda
 
Wala sio siri. Usipojiuliza kwanini kiwanda kimekufa basi unapoteza hela zako kujaribu kukifufua.

Ni kama tu mwendazake alivyopoteza matrilioni ya fedha zetu kwenye kununua madege ili aifufue ATCL.
 
Ni watu waliopewa wizara bila kuangalia uwezo wao: zikawashinda! Tatizo liko kwenye uteuzi wa mawaziri siyo malengo ya serikali. Katika maisha kila tatizo lina solution yake; kama wao waliona tatizo, je walitoa solution gani? Kukimbia tatizo (ostrich philosophy) siyo kusolve tatizo hilo. Ningekuwa na appointing authority, hawa ni watu ambao singewatua katika nafasi yoyote ya serikali tena.

Katika sehemu ya maboresho ya Katiba, ningetaka Waziri asiwe mbunge kusudi rais ateuwe raia yeyote kuwa Waziri na ikiwezekana nafasi hizo zitangazwe kwa raia wote wanaodhani wanaweza kuzimudu na kumpa nafasi rais muda wa kuwadahiri.
 
KUWADAHIRI ndo Muda gani huo?
 
Sio kila tatizo lina solution

Mfano

Tatizo =kifo
Solution=???
 
🤣 🤣 🤣 🤣 ishu hawafanyi utafiti kujua nini kimefanya viwanda bya zameni vimefeli, wao wanadhani shida ni mitaji. Kumbe kuna masuala mengi yanayokabili viwanda kama vile teknolojia duni za viwanda, ushindani toka nje na mifumo yetu ya kodi ambayo mingi si rafiki kwa uwekezaji.
 
Sio kila tatizo lina solution

Mfano

Tatizo =kifo
Solution=???
Kifo, kama ilivyo kuzaliwa, siyo tatizo; ni njia ya asili ya maisha!

Kifo kinachotokea kwa sababu zinazoweza kuzuilika kina solution ya matibabu, ila elewa kuwa njia ya asili ya maisha huishia na kifo. Hakuna mtu anayeweza kuishi miaka 150!
 
KUWADAHIRI ndo Muda gani huo?
Basi inawezekana hujui kuwa rais wa Marekani baada ya kushinda uchaguzi November hutumia kama miezi mitatu akiwafanyia interview candidates wote anaotaka kuteua katika cabinet yake ambayo mara nyingi hukamilika mwezi March. It is possible sielewi swali lako hasa kama ni swali la kipuuzi na la kitoto!
 
Ni watu waliopewa wizara bila kuangalia uwezo wao: zikawashinda! Tatizo liko kwenye uteuzi wa mawaziri siyo malengo ya serikali. Katika maisha kila tatizo lina solution yake; kama wao waliona tatizo, je walitoa solution gani? Kukimbia tatizo (ostrich philosophy) siyo kusolve tatizo hilo. Ningekuwa na appointing authority, hawa ni watu ambao singewatua katika nafasi yoyote ya serikali tena.

Katika sehemu ya maboresho ya Katiba, ningetaka Waziri asiwe mbunge kusudi rais ateuwe raia yeyote kuwa Waziri na ikiwezekana nafasi hizo zitangazwe kwa raia wote wanaodhani wanaweza kuzimudu na kumpa nafasi rais muda wa kuwadahiri.

Good observation mkuu
 
🤣 🤣 🤣 🤣 ishu hawafanyi utafiti kujua nini kimefanya viwanda bya zameni vimefeli, wao wanadhani shida ni mitaji. Kumbe kuna masuala mengi yanayokabili viwanda kama vile teknolojia duni za viwanda, ushindani toka nje na mifumo yetu ya kodi ambayo mingi si rafiki kwa uwekezaji.
Hiyo inategemewa iwe sehemu mojawapo ya kazi za waziri na kutafuta solution yake.
 
Hakika.
Nimewasikiliza leo Waheshimiwa Charles Mwijage na Yosefu Kakunda waliokuwa mawaziri wa wizara ya viwanda na biashara enzi za JPM wakisema kazi ya kufufua viwanda waliishindwa wakiwa mawaziri wa wizara hiyo kwa vipindi anuwai. Malia umma kwa sasa wangeziacha ziwe mikononi mwa sekya binafsi ili wao (serikali) wawe na hisa na uangalizi tu kama ilivyo kwa NMB, CRDB na TBL.
 
Kitu cha kushangaza ni kuwa serikali ya JPM ilikuwa haijengi wala kufufua viwanda kwa kutumia hela za walipa kodi, bali ilikuwa inahimiza ujenzi wa viwanda. Viwanda vya serikali vilivyobinasfsishwa vikashindwa kuendelea wakati serikali bado ina nguvu navyo ndivyo ambavyo serikali ilikuwa ilikuwa inavichukua na kuviweka mikononi mwa wawekezaji wengine binafsi mfano kile cha ngozi Morogoro alichopewa Rostam Aziz.

Sasa hawa kwa kushindwa kazi zao wanataka kungeneza mazingira ya kumlaumu mtu ambaye hawezi kujitetea tena na kusahau kuwa records zipo. Serikali ya Mgufuli iliwekeza kwenye miundo mbinu (TANROADS), usafiri wa anga (ATCL), usafiri wa reli (TRC), usafiri wa maji (MSCL), na uzalishaji umeme tu (TANESCO); siyo viwanda.
 
Ni watu waliopewa wizara bila kuangalia uwezo wao: zikawashinda! Tatizo liko kwenye uteuzi wa mawaziri siyo malengo ya serikali. Katika maisha kila tatizo lina solution yake; kama wao waliona tatizo, je walitoa solution gani? Kukimbia tatizo (ostrich philosophy) siyo kusolve tatizo hilo. Ningekuwa na appointing authority, hawa ni watu ambao singewatua katika nafasi yoyote ya serikali tena.

Katika sehemu ya maboresho ya Katiba, ningetaka Waziri asiwe mbunge kusudi rais ateuwe raia yeyote kuwa Waziri na ikiwezekana nafasi hizo zitangazwe kwa raia wote wanaodhani wanaweza kuzimudu na kumpa nafasi rais muda wa kuwadahiri.

Naomba nijikite apo kwenye katiba juu ya waziri asiwe mbunge, tukumbuke mawaziri wanaiwakilisha serikali bungeni kuleta budget, sheria na kujibu hoja mbali mbali za wabunge kuhusu serikali sasa mtu asiyekua mbunge anakuaje sehem ya bunge? Tuseme wapewe uhalali na io katiba uoni kama kutaiongezea serikali mzigo wa watumishi? Kwani Mbunge akiwa waziri anafanya kazi zote peke yake si kuna watalam wa kutosha wizarani wanao shauri, kupanga budget na kutengeneza sera? Na kama kuna mtu yuko nje na mamlaka teuzi inaona anafaa si inamteua katika zile nafasi 10 za ubunge then inamteua kua waziri mbona imekua ikifanyika hvo siku zote?
 
Kifo, kama ilivyo kuzaliwa, siyo tatizo; ni njia ya asili ya maisha!

Kifo kinachotokea kwa sababu zinazoweza kuzuilika kina solution ya matibabu, ila elewa kuwa njia ya asili ya maisha huishia na kifo. Hakuna mtu anayeweza kuishi miaka 150!
Hata biashara kufa n njia ya asili vile vile
 
Kufufua viwanda vya zamani ni kupoteza muda.

Kiwanda kilichokuwa kikifanya kazi miaka ya 80, kimesimama kwa karibia miaka 20, unakifufua vipi?

Mitambobyenyewe nibyabteknolojia ya zamani, na itakuwa imechakaa kabisa. Kunatakiwa viwanda vipya.
 
Back
Top Bottom