Mkuu ndo umesha'cheat' hivyo...ila inasolvika kwa sababu hakun a ndo hapo bado....lol
aha!? ....very interesting!....
nilishaambiwa, "yaani darling najuta ...mwanaume mwenyewe si lolote si chochote ...kwanza alikuwa ananichafua tu!"
khaaa? mbu nikabakia nimelegeza kidevu nikiwaza nakuwazua yanayowakumba wake zetu huko kwenye maliwazo,
au alikuwa ananipiga changa la uso tu! mnh, ndoa hizi!
Bado naamini kuna serial cheaters ambao hawaangalii makunyanzi...Hao wanaokaa na kupiga tafakuri ni madenti wa hiyo business...Ma haluatani huwa wanapiga kwa kwenda mbele na wanaona ni sifa sana!
Hahahaha AshaDii umewaza mbali mpenz but ni ukweli mtupu! Laiti ingekuwa hivyo. Mimi nilishashuhudia mahusiano ambayo mmoja wa wanandoa alijikuta kwenye wakati mgumu,ambao mwenzie alikuwa anamfanyia visa vya kila aina yaani ile ya mashati kurudi na milipstick, handkerchiefs za kike n.k lakini Mdada yule hakurevenge may be kwa sababu alikuwa na guts za kuquit. But kwa yule ambaye hana guts hizo, kuna mbinu yoyote ya kumsaidia akamketisha mumewena kuongea nae?
Maana ni wazi hali ikiendelea vile bila matuimaini huyu mdada atakuwa vunerable na yeyote atakayempa attention na kuonyesha kumjali anaweza akamshawishi naye akashawoishika.
The same kwa mwanaume anayedharauliwa na mkewe na hana uwezo wa kumwacha pengine naye watoto au jamii inamzuia
Mamii kwahiyo unataka kuniambia huwa WANALAZIMIKA???
Sitaki kuamini kwamba wapo watu wanaoona/amini walil/wanazimika kucheat ,whatever the reason (or rather the excuse) behind it.
I mean naelewa kwamba hao watu nao wanamahitaji kama wengine ila kama ya umuhimu sana na imeshindikana kuyapata toka kwa wenzi wao hawawezi kwenda huko wanakoyapata moja kwa moja???Maana mtu mpaka afikie kutoka nje ya mahusiano yake na kujisikia huru kufanya hivyo mara kwa mara anakua ameyachoka hayo mahusiano..amemchoka mwenzi wake, haheshimu hayo mahusiano..hamhesimu mwenzake, hajali hatma ya hayo mahusiano..hajali hatma ya mwenzake...sasa kwanini aendelee kuwepo kwenye mahusiano ya aina hiyo na mtu ambae kamchoka/hamheshimu na wala hamjali???
Kama kweli wangekua wanaona wana haki (wanayojaribu kuonyesha kwa kupitia lawama na visingizio vihusuvyo watu wengine) ya kufanya wafanyayo kwanini wasifanye kwa uwazi??Kwanini wasiwajulishe na wenzi wao kabisa??
Pamoja na kwamba wakikamatwa wanaishia kulalamika na kulaumu bado wanajua wanachofanya sio sahihi na ndio maana wanaficha.
MJ1,
Hakuna cha mapungufu ya mke au mume katika suala hili. Mtu anaamua mwenyewe halafu anajipeleka mwenyewe na kudai amefurahia kuzini halafu anakuja kusema eti kasababishiwa na mwenzi wake!! Ni ajabu sana kusikia haya maneno!
Unajua, binadamu kaumbwa na magunia zaidi ya milioni moja ya tamaa! Na mbaya zaidi tumezidiana. Kuna wengine wana mafuso kibao yamejaa hizo tamaa zao wakati wengine wanaweza kujaza ka-bajaj kamoja tu!! Sasa huyo mwenye mafuso yake ya tamaa, hata mke au mume angekuwa malaika bado angeeda kuzini! Upo hapo.
Mengine ni mazungumzo baada ya habari!!
Nitarudi baadaye kidogo!
....mwj1 mahbouba....tatizo ninaloliona hapa tayari kuna fitna ya kutafutwa sababu ya kutoka nje kwa hali yoyote...
mosi, hivi hakuna solution nyingine yeyote ya mwanandoa kustahmili ndani ya hiyo ndoa bila ku cheat aka kutoka nje???
pili, una guarantee gani huko nje ndio itakuwa maliwazo tosha kufariji moyo, na uhakika atatoka na wangapi
akidhi kiu ya kupata kitu roho inapenda???
Kweli mkuu,
Hakuna liwazo lolote linaweza kupatikana kwa njia hii. Kama mtu kakwazika basi hakuna ujanja...Ajaribu kutimiza wajibu wake, but within limits!! i.e amkalishe mwenzake na kumweleza feelings zake jinsi asivyoridhika na hali inayoendelea..(ingawa najua watu wengi huwa na kiburi na hudharau vitu vya namna hiyo) na kama hali haipati suluhisho basi kila mtu aanze maisha yake!
Binafsi siamini kabisa katika ndoa ya hadi kifo...Samahani kama kuna mtu nimemkwaza......Freedom ya mtu na utu wake anayo mwenyewe. Hakuna sababu yoyote au uhalali wa aina yoyote unaweza kupatikana kwa kuumiza feelings zako eti unalipiza kisasi au kumkomoa mtu mwingine!!
Cheating ni tamaa tu na hakuna maelezo mengine!
Hapana sweetie najua unanifahamu vema jinsi nsivyojua kujielezea. Hii tafsiri haikuwa niloikusudia, si kuwa kuna mtu anataka kutoka la hasha, najaribu kufikiria extremes za wanandoa ambao kwa namna moja au nyingine wananyimwa hakizao za msingi ndani ya ndoa hiyo na kwa bahati mbaya hana uwezo wa kujitambua na kurebuke hiyo abusive relationship (Hapa nitazungumzia zaidi wanawake wale ambao hawana uwezo wa kutoka au kudai haki zao- wanawake ambao kama yanavyosema nukuu hizo kuwa wanalazimika kutoka ili kupata liwazo.
And ofcoz mwenye uwezo wa kusema kama analiwazika kweli au lah ni mtokaji, nikirejea ile thread ya MADAM T kuna wadada waliokiri kucheat na wakaonyesha kuwa wanafurahia and they do not regret darling , je huyu utasema hapati liwazo??
Kwa mtazamo na msimamo wangu, na kwakuwa nilishawahi kuishi kwenye mazingira ya kujifanya mume *****
mwenye uwezo wa kuyafikiria yote yanayoweza justify cheating...mwishowe niligundua ONCE A CHEATER ALWAYS A CHEATER!
...mwenzio akisha cheat mwanzo kwa sababu yeyote ile hataacha, bora kuachana tu!
hakuna mawasiliano aina yeyote yatayojenga na kurudisha trust iliyokwisha vunjika...
wakatabahu!
huyo kwa vile ulimgundua tu, ila wanawake huwaa tuna mapenzi ya kweli, na ikitokea umetoka ujue mambo ni mazito pamoja na kwamba jamii haiwezi kukuelewa ila ndio hali halisi inavokuwa, unavumilia mpaka unaona huwezi tena, na hapo kama ukipata washauri wabaya ni rahisi sana kuanguka dhambini aisee, huyo wako alikwambia kweli unachafulwa tu, sababu tendo lile kwa mwanamke linahitaji akili itulie na ujione uko safe, wasiwasi haukufikishi hata kimara kwa safari ya arusha, wakati wa tendo akili yake inazongwa na mambo mengi na mawazo......
Mie nawaambia wanaume wawapende wake zao na kuwahakikishia wako safe na kuwapa mapenzi yooote waone kama kuna mke atakayetoka, mpe mkeo muda wa kutosha, imagine kila siku mtu saa saba nane, kalewa, mara masimu yanaanza kuingia, msg ..maneno yote mazuri anaambiwa hawala
Uko sawa KipimaPembe natamani wengi wangekuwa na mawazo ya aina hii hasa wanaume wale ambao wanakuwa na nyumba ndogo kwa kisingizio cha mke hamjali, au wanaotembea na wasichana wa kazi kwa kuwa tu mke yuko buzy.
Mnachonishangaza ni pale mnaposhauriana kuwa mke akikudharau, akijifanya buzy huna haja ya kupigizana nae kelele,tafuta wa pembeni maisha yaendelee !! Ila linapokuja kwa mke akiwa ndie victim yeye hatakiwi kabisa kutafuta wa pembeni!! Hili hatulipingi na ndio maana nikaomba sasa tusaidiane namna ya kumsaidia victim wa hali hii ili asitoke nje, si mwanaume, si mwanamke.
Lizzy Baby, natamani hii ndio ingekuwa reality. Am telling you kuwa katika wanawake wanaocheat ndoa zao ni wachache sana ambao wanacheat kwa kupenda au pesa. But wengi wao hucheat kwa kutafuta faraja, ambayo imekosekana ndani ya ndoa zao. Ni kweli kabisa akikamatwa hata kama alicheat kwa kuwa alinyimwa unyumba na mumewe kwa miaka miwili mfululizo bado kosa litakuwa kwake ninakubali kabisa ndio maana ninauliza mbinu ya kurekebisha mambo. Ukiisoma vizuri nukuu ya muhanga utagundua kuwa ni needs za kibinadamu ambazo sometimes zinapelekea hiyo cheating sasa tunafanyaje kuzikizi hizi needs pale ambapo mawasiliano kati ya wanandoa hayapo kwa kuwa tu mmoja wao ameona hakuna haja ya kusikilizana na mwenzi wake. Mf. tuseme mwanamke kila akirudi analalamika kichwa kinauma, amechoka au leo nina hacra siwezi'toa huduma' bosi amemuudhi n.k kwa miezi mitatu mfululizo na bado hayuko tayari kuketi kitako na kusilikiza feelings za mwenzi wake. Huyu victim afanyeje ili asitoke nje??
Yah!Wa kwanza kulaumiwa ni mume kwa upande mmoja na upande mwingine ni mke mwenyewe!Ila kama ilivyo ada hakuna justifcation ya huu ujinga!
MJ1, kichwa cha habari yako kimebeba yote. Mawasiliano kwenye relationship. Through my experience, hii kitu haipo katika nyumba nyingi. Nimeona nyumba nyingi zinavunjika sababu ya kukosa kuwasiliana. Mwambie mwenzio unataka nini, what you feel, kipi bora kwako, kipi hakifai. Hii yote inatokana kuwa mmekua baba fulani na mama fulani, kaheshima kakipuuzi mnakajenga wenyewe. Unajikuta ukidhani kua nikimwambia baba fulani nataka aniguse hapa, sijui atanionaje. lakini nikikutana na wa pembeni, yule vile ni sweetheart, namwambie vile ninavyojisikia bila uoga. baba fulani nae nyumbani, he's too busy, mikutano the whole day, akirudi kabeba ma file kuna kazi za kufanya maana ana presentation first thing in the morning na mengine mengi. sasa hata tunda likiliwa ni ile style ya "kubali yaishe" hakuna mahanjam, ni bora liende. nikienda pembeni, tumeipainga, kila mmoja ana hamu na mwenzie mapenzi motomoto ananiridhisha. cheating itaisha kweli kwa maisha yetu haya ya kiafrika... watu wata cheat hadi mwisho wa dunia, unless mabadiliko yatokee.
lawama zinaweza kuwa kwa anaayecheat but kwa wanawake wengi wanasababishiwa na waume zao