MkanyageniKijiji
New Member
- May 16, 2017
- 3
- 6
Mimi kama raia wa kawaida nisiye na chama chochote hapa Tz, napenda kuwashauri mawakili wa chama cha Chadema ambao wanamtetea Freeman Mbowe kwenye kesi ya ugaidi wajitoe mapema tu. Nimefuatilia sana hii kesi ya mbowe mwanzo mwisho nimegundua vitu vingi sana ikiwemo ukiukwaji wa mambo mengi sana na sarakasi nyingi zikiwa zinafanyika pale mahakamani. Kiuweli kabisa napenda kuwapongeza wanasheria wote wanaomtetea Mbowe kwa kipindi chotee lakini pia sio vibaya kama watafikilia na kuafikiana kwa pamoja kujitoa mazima kwenye kesi ya mbowe. Lengo kuu linajurikana kwenye kesi hii ni kumfunga Mbowe tu then kuja kumtoa kwa msamaha wa Raisi. Ndugu kibatala kama unasoma huu ujumbe nawaomba pumzikeni kwenye hii kesi ya ugaidi then serikali itajua nini cha kufanya. Mwishowe wa siku mtakuja kwa wananchi kuanza kulalamika wakati sisi wenyewe tunajua mwisho wa hii kesi ni nini. Watu wengi wanafahamu uwezo wenu ni mkubwa sana lakini hamtaweza kubadirisha kitu chochote hapo zaidi ya kuendelea kupotezana muda tu na kusumbua watu.