Mkuu Bwanchu2, umeuliza swali la msingi sana, na sio Lawyers tuu wasioruhusiwa kujitangaza, bali hata madaktari, wahadhiri, maprofesa, hospitali, huduma za tiba, "madawa ya moto", mfano matangazo yote ya madawa utakayoyaona ni matangazo ya madawa baridi ambayo yanaweza kuuzwa duko lolote hata kwa Mangi au dukawala na sio medicine!.
Shukrani sana Pasco kwa kuona umuhimu wa swali langu na kujitahidi kueleza sababu kwa kadri ya uwezo wako. Binafsi naona kwa kweli hayo makatazo yamepitwa na wakati na ninaamini kabisa hakuna ubaya wowote ule kwa wakili, daktari, au mwingine yeyote yule kutangaza huduma anazotoa ili mradi wanafuata muongozo ambao utawalazimisha au utawafanya wasiseme uongo kwenye matangazo yao.
Tunaona kwenye nchi za wengine mawakili wakiwa wanatangaza huduma zao kwenye matangazo ya biashara kwa kuweka ama kanusho (disclaimer) au angalizo kuwa kila kesi ni tofauti na matokeo yanaweza yasilingane baina ya kesi na kesi. Kwangu kufanya hivyo ni uwajibikaji
Kwa kufanya hivyo kunakuwa hakuna ubaya wowote maana tayari wanakuwa wameshaji-CYA (Cover Your Ass). Hata katika matangazo mengine tu ya biashara nayo huwa na miongozo yake, hususan katika nchi zilizoendelea, na mtu hawezi tu kutengeneza tangazo linalosema uongo. Kuna biashara nyingi tu ambazo zimewahi kushitakiwa kwa kosa la kutangaza uongo.
Tanzania tunafuata mfumo wa sheria wa common law wa Uingereza aomba tuliokopy neno kwa neno (pari matiriale), toka sheria za India. Yaani ile siku Wajerumani wamenyanganywa koloni lao la Tanganyika na kupewa Waingereza, there was no time kutunga sheria yoyote, kilichofanyika ni kuzichukua sheria za India, neno kwa neno na kuzifanya ndizo sheria za Tanganyika!.
Mambo ya monkey see, monkey do hayo! Kaazi kweli kweli.
Lengo la kuzuia matangazo huduma za uwakili, udaktari na madawa ni kuepusha watu kufuata huduma fulani kwa influence ya Tangazo, mfano Mimi nijitangaze PPR is Best Legal Firm for Criminal Cases, then mtu akaja PPR Law Firm kwa matumaini ya kupata the best services kama tulivyojinadi, akishindwa kesi, atajihisi alidanganywa!.
Lengo la kutangaza wala si baya. Lengo la kutangaza ni kutanabahisha umma kuwa unatoa huduma kadha wa kadha. Na kama mtu akitumia lugha ambayo si subjective au isiyo huru kutafisirika kwa namna nyingi, basi hayo mengine ni rahisi sana kuepukika.
Mambo ya kusema sijui 'mimi ni the best lawyer in town' na blah blah kama hizo, ni mambo ya opinion. Na kwenye matangazo, kama kuna miongozo iliyo thabiti basi lugha au maneno ambayo yako opinion-oriented yanakatazwa. Manake ukisema wewe ni 'the best lawyer in town' when it comes to criminal cases, hiyo ni opinion yako. Mwingine anaweza kuwa na mtazamo tofauti kabisa.
Lakini ukisema wewe ni wakili mwenye tajiriba ya miaka 30 kwenye mambo ya kesi za jinai, na unapatikana sehemu fulani, sioni opinion yoyote hapo maana, kama kweli umeanza shughuli zako za uwakili miaka 30 iliyopita, basi kilichopo kwenye tangazo ni cha ukweli. Na kama unapatikana mtaa wa Makunganya na kweli ofisi zako zipo mtaa huo, hicho nacho ni ukweli vilevile. Na ukitoa namba ambayo wateja wanaweza kuipiga kuwasiliana na ofisi yako na hiyo namba kweli ni ya ofisi yako, huo nao ni ukweli.
Sasa, hapo utaona kabisa kuwa kilichotangazwa ni taarifa za ukweli, hakuna chumvi wala binzari. Ila, kama mtu mwenyewe baada ya kuona kuona kwenye tangazo kuwa una tajiriba ya miaka 30 halafu aka-infer yeye mwenyewe kuwa utakuwa na tajiriba ya kutosha na hivyo labda uwezekano wa yeye kushinda anachokitaka akija kupata huduma kwako, basi hilo litakuwa hitimisho lake yeye based on your facts.
Kwa mfano, kama mimi ni lawyer na nimebobea zaidi kwenye mambo ya kifamilia (talaka, matunzo ya watoto, na kadhalika), sioni ubaya kama nikitangaza huduma ninazotoa bila kutia chumvi na kama mteja anataka kujua rekodi yangu na mengineyo kama hayo, basi tutazungumza akija ofisini au popote pale tutakapokutana.
Kwa hiyo nadhani lengo linakuwa baya tu pale ambapo kunakuwa hakuna udhibiti wowote wa matangazo kama hayo hususan kama watu wataachiwa waweke kila aina ya chumvi kwenye hayo matangazo. Lakini kama ni matangazo yaliyo basic tu yenye lengo la kutanabahisha umma, sioni ni kivipi yanaweza kushawishi watu watu wafuate huduma fulani wakiwa na matumaini hewa waliyoyapata kutoka kwenye tangazo.
Lengo ni ni kwa huduma za kisheria, hospitali na madawa kujitangaza kwa results oriented matangazo. mfano Wakili Murtaza Lakha alivyotetea kesi nyingi za mader na kushinda, ndie alihesabika wakili best number 1 Tanzania na kupewa utetezi wa watuhumiwa number 1 na 2 kwenye kesi ya Uhaini ya kina Macghee.
Sasa kama lengo ni huduma zijitangaze kwa matokeo yake, umma utajuaje sasa kama mtu ana rekodi ya ushindi katika kila kesi anayoisimamia au kuitetea? Watu tutajuaje kama wewe hujawahi kushinda kesi hata moja?
Hata hivyo huko India sheria hiyo ya kutojitangaza iliishafanyiwa marekebisho kitambo, sasahivi legal firms zinajitangaza vizuri tuu haswa baada ya ujio wa Utandawazi
I wonder why that is......?
Pia yale matangazo ya Ofisi za Mawakili siku hizi ni matangazo tosha, Mijengo ya Ofisi za Mawakili ni matangazo tosha!, website zao, blogs zao, na wengine wana collude na media hivyo cases zao kupewa limelight!.
Hivyo vibao vinavyoonyesha hapa ni ofisi ya uwakili wa fulani havina reach kubwa. Kwanza hizo ni signage tu zinazotambulisha kuwa hii ni ofisi ya kitu fulani. Havina kabisa tofauti na kibao cha shirika la chakula na lishe pale mtaa wa Ocean Road (sijui ndo unaitwa Obama siku hizi)
Mfumo mzuri wa matangazo ni mabango ya kueleza wanatoa huduma gani?, au specific law firm ime team up na kina nani, huko yale statutory matangazo ya magazeti wakiyalipia up to full page!.
Mfumo mzuri wa matangazo ni, kwanza waruhusu watu watangaze huduma zao, halafu ndiyo wapanue wigo. Kwa wenzetu huko majuu, kwa mfano, watu hununua hata space kwenye mabasi ya abiria ya umma na kuweka matangazo yao ubavuni mwa basi, treni, na kadhalika.
Hata kwenye TV watu hutangaza pia. Kwenye redio nako hivyo hivyo. Na kwa kufanya hivyo wanakuwa wanafikia watu wengi zaidi.