tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 22,325
- 19,109
Nilipohoji kuhusu uvaaji wa mchungaji Tony Kapola kuna watu hususan wanawake walinivaa kwa ukali kwamba nina wivu niwaachie mchungaji wao, kwamba uvaaji wake ni wa kawaida, kwamba uvaaji wa kisasa kwa Watumishi wa Mungu sio tatizo. Binafsi niwaambie UTUMISHI WA MUNGU ni mgumu na unahitaji usiriaz kuliko wengi mnavyofikiri, Yohana alijinyima hadi kuvaa magunia na kula nzige jangwani mnafikiri utumishi ni mwepesi?
Tunarahisisha mno utumishi wa Mungu miaka hii ndio maana wahubiri nao wanahubiri injili mpya nyepesi ya kisasa iliyopakwa maneno matamu ya miujiza, utajiri na mafanikio, hawaihubiri ile injili pure ya Ufalme wa Mungu, ile ya kukemea dhambi kwa ukali wake.
Ndio maana tunaskia Watumishi wengine wanasema hata dukani sigara weka biashara sio ibada, wengine wanasema ndoa sikuiz sio mwili mmoja, wengine wameenda mbali na kusema pesa za majini sio haramu. Utumishi wa Mungu umeonekana ni simple tu hadi kina Irene Uwoya wanataka kufungua makanisa sasa huku bado miili imejaa tattoo.
Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi anahitaji Watumishi VIELELEZO KWAO WAAMINIO. Katika uvaaji, unenaji, utendaji na mwenendo mzima wa maisha kwa ujumla
Kwa Mungu hakuna usasa, sheria zake ni zile zile WAACHE DHAMBI NA KUNIABUBU
Mahubiri ya utajiri, pesa, miujiza na mahusiano yasitutoe kwenye mstari, Mungu sio mrahisi kama tunavyoaminishwa na Watumishi hawa wa kisasa
Tunapaswa kusali kwa imani, kutubu, kufunga na kuomba, Tunapaswa kumuogopa Mungu na kumuabudu kweli. Tunapaswa kuyaheshimu madhabahu yake. Tunapaswa kutambua Mungu ni mtakatifu hadhihakiwi wala kuchanganywa na aina yoyote ya uchafu
Nawasilisha.